Tatoo inaleta shida Gani haswa?
Sipendi kuchora tatoo lakini sidhani kama inamletea mchoraji dhambi yoyote labda kama hiyo tatoo anaichora ikihusiana na matendo maovu.
Yaani mtu achore picha yake au msalaba au ya mwenza wake halafu awe kafanya dhambi? Sasa dhambi hapo ni nini yaani kabisa.
Nadhani wahafidhina wa dini Huwa hawapendi vitu vipya vinavyotokea na mwanzo Huwa wanavipinga sana ila vikizoeleka inaonekana kawaida.
Hata wanawake walipoanza kuvaa suruali Ilikua changamoto ikionekana hadi ni dhambi lakini ilipozoeleka imekua ni jambo la kawaida kabisa.
Tuna amri moja tu upendo, jambo lisilo na madhara kwako na mwingine kuitwa dhambi ni ulimbukeni.
Mambo mengine sio ya kiimani wala dini ni utamaduni wa mahali.
Kwa mfano mwanamke akivaa sketi fupi akaingia kanisani kijijini Mpitimbi itaonekana ni shida haswaa, lakini mwanamke huyohuyo akivaa hivyohivyo akaingia kanisani kuu la Mtakatifu Paulo London haitakua shida hakuna atakae jali kwasababu ya utamaduni wa mahali.