patience96
JF-Expert Member
- Aug 19, 2011
- 1,353
- 574
Je Kujikuna ni Zawadi Itolewayo na Ubongo?
Je Ni Kwanini Unahisi Raha na Adha Unapojikuna?
Salaam Wadau!
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada.
Unapohisi muwasho kwenye mwili wako ni dhahiri kuwa utatamani ukune (scratch) sehemu husika.
Hata wanyama wengine hufanya hivi pia.
Muwasho (itch) hujulikana kitaalamu kama pruritus, ni hisia ya jumla inayotokana na kuwashwa kwa seli za ngozi au seli za neva zihusianazo na ngozi.
Je hisia za kuwashwa kwa ngozi hutokana na nini hasa? Kwa kifupi, hisia za kuwashwa kwa ngozi hutokana na kuchochewa kwa pruriceptors ambazo ni neva receptors zenye uwezo wa kuhisi muwasho. Pruriceptors daima huwa katika ngozi; Fikiria iwapo ungehisi muwasho kwenye bandama lako wakati huna uwezo wa kulifikia na kulikuna!
Sayansi inasemaje kuhusu tendo la kujikuna?
Misuli, joints na viungo vingine vinaweza kuumia kutokana na sababu mbalimbali, lakini ngozi yako ndiyo sehemu maalumu ya mwili wako inayoweza kuhisi maumivu na kuwashwa pia. Ngozi yetu ndiyo safu yetu ya kwanza ya ulinzi ambayo daima huweza kugusa the outside world (baridi, joto nk.)
Nini visababishi vya muwasho?
Muwasho unaweza kusababishwa na kitu chochote kilicho nje ya mwili wako. Mfano: kemikali, pilipili, baadhi ya mimea (majani, mizizi, utomvu, magamba ya miti), gesi ya kutoa machozi, sumu, kuumwa na wadudu, tetekuwanga, sunburn, nickel, saruji, shampoo, maji, magonjwa, perfumes, sabuni nk.
Muwasho pia unaweza kusababishwa na kitu kinachotokea au kuingizwa ndani ya mwili wako
Mfano: sumu, mzio (allergies), madawa (mfano; chloroquine, morphine), magonjwa (leukemia, cirrhosis, lymphoma..), kuzeeka kwa ngozi (alloknesis), matatizo ya neva (shingles, multiple sclerosis nk)
Je ni kwanini unapata raha na maumivu unapojikuna?
Unapojikuna unapata raha fulani hivi amazing yenye mchanganyiko wa maumivu.
Kwa kifupi, seli za neva hutuma signals za maumivu kupitia neurons za uti wa mgongo kwenda kwenye ubongo wako kwamba kuna kitu kinaumiza sehemu fulani ya mwili, ubongo naye hutafsiri hizo signals na kurudisha jibu kuwa sehemu husika ikunwe ili mwili upate relief, wakati mkuno ukiendelea, ubongo kupitia kitengo cha motor control, hutoa zawadi ya raha ktk sehemu husika kama pongezi kutokana na mchakato uliofanyika. Zawadi ya raha hutoka ktk kisaketi cha raha kiitwacho “reward circuit” baada ya premotor cortex (PM) na primary motor cortex (PMC) kupiga mzigo.
Utafiti uliofanywa na Hideki Mochizuki, PhD - Profesa Msaidizi wa Dermatology wa TUSM, unaeleza ni kwa nini ukunaji ngozi hutoa hisia zenye kufurahisha na za kupendeza kwa wagonjwa walio na ukunaji sugu wa miwasho. Kwa kutumia advanced functional Magnetic Resonance Imaging (fMRI), aliangalia shughuli za ubongo kwa wagonjwa sugu wa miwasho na shughuli za ubongo kwa watu wengine wasiokuwa na tatizo la miwasho.
Aliona maeneo ya ubongo yanayohusika na motor control pamoja na reward processing ambayo yalikuwa active sana wakati wa kujikuna kwa wakunaji sugu. Utafiti huu umesaidia kuelezea kwa ufasaha adha ya kujikuna wanayopata wale watumiaji wa madawa ya kulevya. Pia kutafuta namna ya kudhibiti ukunaji sugu wa ngozi.
Ni raha kujikuna japo husababisha hisia za maumivu makali kwenye ngozi yako.
Unapoendelea kujikuna mwili wako hutema zaidi kemikali ijulikanayo kama serotonin.
Pamoja na kuzuia maumivu, serotonin huamsha neurons za GRPR (Gastrin-Releasing Peptide Receptor) kupitia vipokezi (receptors).
Neurons zilizoamilishwa (activated) hufanya hisia ya muwasho ziwe mbaya zaidi!
Itaendelea.
''there is nothing quite so satisfying as scratching an itch"