Okwaaa
JF-Expert Member
- Dec 3, 2020
- 1,332
- 2,963
Wasalaam wakuu,
Kwanza poleni na kazi kwa ambao michongo imegoma mpaka sasa, na pia hongereni na kazi kwa ambao michongo imeenda sawa.
Wakuu, mm ni mhanga wa kukosa ajira, zaidi mhanga wa maisha magumu. Siku hizi nimeshaanza kuzoea mlo mmoja😁, sijisifii ila ukweli upande wangu hali ni ngumu. Nahofia vidonda vya tumbo.
Binafsi nishamove home saizi najitegemea kigeto zaidi. Ila geto langu ukiona utacheka, hali imekuwa ngumu hadi natamani kuuza vitu hivyo hivyo vichache vya geto kama ndoo za maji na kimeza ili nipate mlo😆
Sitanii jamani hali ni ngumu, nimejaribu kuwaomba watu waliopo humu connection but imekuwa ngumu, nimetangaza kuuza simu yangu hii nayotumia ili nibalance maisha na mtaji, bado sipati mteja, wengi tunashindwana kwa sababu ya umbali. Nimejaribu kuparangana kutafta hela lakini naambulia patupu.
Siku yote naparangana kupata 2000 na yenyewe inanipiga chenga. Hii inanikumbusha kipindi nipo chuo niliwahi shuhudia wabeba mizigo wakichomana bisibisi stend kuu kisa sh mia (100) nikastaajabu sana, ila saizi naona inawezekana kabisa 86%.
Sasa niwaulize wajuzi wa mambo, huu ugumu wa maisha ulikuwepo tangu enzi na enzi au? (tusije mlaumu mtu bure). Au huu utawala wa JPM ndo umezidisha huu ugumu wa maisha?
Mlioanza kujitegemea tangia utawala wa JK tupeni mrejesho basi wakuu?
Mwisho. Sijachoka kutafta kazi halali ya kunipatia kipato kidogo, maana ndoto yangu kubwa nimsaidie bi mkubwa wangu maana umri unaenda na mimi sina kitu (ni aibu).
Pia nauza simu ili nijiajiri, unaweza kunipa msaada tu hata kwa kununua simu yangu Samsung A10 kwa 215,000/=, hiyo hela cash ina maana kubwa sana.
0746866631.