Kwetu karibu sote tumekuwa na tabia ya kukata kucha kwa meno japo inafika kipindi inapungua na kama mimi nimeacha kabisa. Sijui kitaalam ikoje ila
Sababu zake
Sijui hasa sababu ni nini ila kwetu hii hali huwa inakuja tu yenyewe automatically. Sababu ya kuendele(z)a ni pale utakapogusa ukaona kuna kama kukwaruzwa fulani na kucha basi unajikuta unataka kumaliza kabisa hiyo hali
Madhara yake ni
1.kung'ata/ kula mchanga ambao utapelekea kuumiza meno na madhara mengine ya mchanga
2.maradhi ya tumbo kutokana na kula uchafu mwingine wa kwenye kucha
3.maumivu makali sana kwenye kingo za kucha kwa kando. Saa zingine inafikia mpaka kuvimba sehemu hizo kutokana na kuvuta vingozi vidogovidogo vilivyopo sehemu hizo (hii nimeexperience sana)
Tahadhari za kuchukua
1.kama unajijua una hali hiyo basi zingatia usafi wa kucha muda muda wote
2.using'ate (usizivute/usizikate)kucha kupitiliza mpaka ukavuta vile vinyama vya kando (japo mimi hii nilishindwa kujizuia kabisa)
3.japo ni ngumu ila jizoeshe kidogokidogo kutumia wembe mpaka utazoea tu na utaacha kabisa kung'ata kucha tu