Je, kulikuwa na ulazima gani Tanzania kuchukua wimbo wa Afrika Kusini na kuufanya wimbo wa Taifa? Kwanini tusingetunga wa kwetu?

Je, kulikuwa na ulazima gani Tanzania kuchukua wimbo wa Afrika Kusini na kuufanya wimbo wa Taifa? Kwanini tusingetunga wa kwetu?

Tulishiriki Idea ya wimbo wao wakatunga mashairi na kuimba.

Uhuru wa S.Afrika tumehusika pakubwa.

By the way waasisi Nia Yao Hasa wimbo Ule uje kuwa wimbo wa Africa nzima maana tulidhamiria kuanzisha Dola moja ya Afrika.
Wimbo ulitungwa miaka ya 1800, nyie mlishiriki wapi?
 
Ukiangalia sana Technically hakuna wa kwetu au wa kwao wote ni wale wale tu Binadamu.....

(Hata Kusini wote unaweza ukasema sio Watanzania ni Waafrika Kusini) au unaweza kusema Dunia nzima Binadamu wametokea kwenye hii ardhi ambayo kwa sasa inaitwa Tanzania

In short lolote zuri lifanywe sababu ya uzuri wake na sio kufanya kila kitu sababu ni unasema ni cha kwetu hata kama ni inferior....

By the way Kipindi kile cha PAN Africanism na kuonyesha Solidariy kuwaunga mkono wale ambao tulitaka kuwakumboa kwa kutumia huu wimbo kulisaidia....

Ni kama tu kwenye wimbo wa TANU yajenga nchi kila kitu ni kama KANU yajenga nchi
 
Nyimbo ilitengenezwa mwaka 1897 na enock sentonga... ni miaka miaka 12 tu tangu bara la afrika ligawiwe kutoka berlin conference so note kwamba hakukua na nchi inaitwa tanganyika au tanzania zimbabwe au botswana mana hao tajwa ni baadhi ya nchi zinazotumia wimbo huo... ukanda wa kuanzia Tanzania kushuka chini ulifahamika kama south africa na wajerumani waliigawa hii south africa katika majimbo au states za kama rhodesi msumbiji ya sasa, Coast of east africa ambayo ni tanzania ya sasa...zulu land ambayo ni ukanda wa lesotho mpaka south na vi nchi vya jirani...hatukua wavivu bali ulikua ni wimbo wetu wa taifa tangu zamani tulibadili kwq kiswahi tu kwa sababu tunazungumza kiswahili ila tulikua states tofauti ila tulikua chini territory moja ya kikoli iliyoitwa southen africa land hivuo technically tulikua nchi moja tuu..swali kwani ule wimbo wa tazama ramani ni wimbo gani? Wa taifa au wa nni
 
Huenda ni uvivu tulionao ndio unasababisha umasikini wetu na tumebaki kutafuta visingizio visivyo na idadi.

Swala nyeti kama wimbo wa taifa, ambao ndio kitambulisho chetu, iweje tuukwapue wimbo wa Afrika Kusini na kuufanya wetu?

Je kwanini hatukuufanya wimbo wa Tazama ramani utaona nchi nzuri, uwe wimbo wa taifa letu?

Nadhani sasa ni wakati wa kurudi kwenye asili yetu, tutunge wimbo wetu wenyewe au tuufanye wimbo wa TAZAMA RAMANI uwe ndio wimbo wa taifa.
wewe kijana umezaliwa mwaka jana nini?
 
Wimbo ulitungwa miaka ya 1800, nyie mlishiriki wapi?
Sijaona HOJA ya kutafuta wimbo mwingine Kwa kigezo kuwa alotunga alikuwa msauzi.

Mbona wimbo wa MALAIKA ulitungwa na mtz bt Miriam makeba akauimba tena na ukawa maarifu duniani,

Sikusikia S.Afrika wakidai Miriam atunge wimbo wake tofauti na aloukopi bongo???
 
Tazama ramani mrefu kinoma, ni kheri tuache hivyo hivyo maana hizo kamati sijui wanakway wa kutunga, kuhariri na kupata wimbo wa taifa watakula pesa zaidi ya pesa ya sensa. Mkuu Bujibuji Simba Nyamaume waambie waache tu hasara ni kubwa kuliko faida.
EEEE? ZAIDI YA ZA SENSA ETI 😀
😀😀😀
 
Afrika kusini ndio waliiga wimbo wetu wa taifa. Ni sawa na leo Burundi waufanye wimbo wa Diamond wa nyegezi wimbo wao wa Taifa halafu baadaye Tz na sisi tuufanye wa taifa.
 
Wimbo wa maana wenye hisia za ndani na uzalendo ni "Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote" Huu ndio wimbo wakati wote tangu utotoni kila nikiusikia na kuimba naguswa kabisa.
 
Ni vema muandishi afanye homework ya kujua mkutano wapigania amani kusini mwa jangwa la sahara uliofanyikia Zambia ulizaa kitu gani.
Nyimbo hizi zimeanza kuimbwa kabla nchi zote (Tanganyika, Zambia na SA) hazijapata uhuru.



 
Il

Naomba huo uhalisia, mimi elimu yangu inaniambia nchi huru ya Africa kusini ilianzishwa miaka ya 90 ,kabla ya hapo South ilikuwa na Rais mkaburu aliitwa Botha
Kajisomee japo kidogo uitafute uipate historia ya Republic of South Africa (RSA), badala ya kung'ang'ania vya kulishwa tu.
 
Tazama Ramani ni WA kutoka China
Mtunzi ni huyu hapa
1665137336911.png
 
Kwani TANZANIA na South Afrika, ipi Hasa ilianza kupata Uhuru???

Tuanzie hapo .
Ndugu yangu kajisomee basii na wewe ufanye uchambuzi 'tondoti

History of South Africa From Wikipedia, the free encyclopedia

..............................................................................Following the defeat of the Boers in the Anglo–Boer or South African War (1899–1902), the Union of South Africa was created as a self-governing dominion of the British Empire on 31 May 1910 in terms of the South Africa Act 1909, which amalgamated the four previously separate British colonies: Cape Colony, Colony of Natal, Transvaal Colony, and Orange River Colony. The country became a fully sovereign nation state within the British Empire, in 1934 following enactment of the Status of the Union Act. The monarchy came to an end on 31 May 1961, replaced by a republic as the consequence of a 1960 referendum, which legitimised the country becoming the Republic of South Africa.
From 1948–1994, South African politics was dominated by Afrikaner nationalism. Racial segregation and white minority rule known officially as apartheid, an Afrikaans word meaning "separateness", was implemented in 1948. On 27 April 1994, after decades of armed struggle, terrorism and international opposition to apartheid, the African National Congress (ANC) achieved victory in the country's first democratic election. Since then, the African National Congress has governed South Africa, in an alliance with the South African Communist Party and the Congress of South African Trade Unions.........................................................
 
Pia kuna mwingine tulikuwa tunaimba shule ya msingi, huu ni wa kuisifia zaidi unaimbwa hivi;

"Tanzania Tanzania, nchi yenye mali nyingi... Watu wengi wa ulayaaaa wanaililia sana, niliona ndege wengi...chini wametia fora...walinipendeza mlio kama mtoto wa nyumbani...Ngooorongoro ile ngoorongoro ile ngoorongoro ileee ngoorongoro ileee.."

Sijui ndo hivi
Hapana.

Huo mimi sijawahi kuusikia.
 
Tazama ramani ni bonge la wimbo! Na una sifa zote za kuwa wimbo wa Taifa la Tanganyika! Sema tu unatakiwa pia kufanyiwa maboresho kwenye mashairi yake! Kusiwepo mstari wowote ule wa kutaja majina ya viongozi! Sijui Nyerere, sijui Karume!!

Tena kama huyo Karume ndiyo hatakiwi kabisa kutajwa! Maana tayari Zanzibar wana wimbo wao wa Taifa.

Kiukweli hui wimbo wa sasa hauna mvuto! Eti Mungu ibariki Afrika! For what!! Wimbo wa Taifa uiongelee Tanzania tu na watu wake.
Mimi ninasikitika tu kujuwa mtunzi wa wimbo huo kuwa na mbegu mbovu iliyopo sasa, tofauti kabisa na wimbo wake.
 
Unaendeshwa na roho za mapepo wachafu wewe. Kwa hiyo tuutumie wimbo mtumba, huoni huo ni umasikini kabisa wa fikra?
Kwa hiyo we kwa akili yako unadhani tukibalisha wimbo ndo Mungu atasikia na kujibu maombi yetu? What a hectic! Wimbo wa Taifa sio km bongo fleva kwamba baada ya mda fulani unatoa remix.
 
Huenda ni uvivu tulionao ndio unasababisha umasikini wetu na tumebaki kutafuta visingizio visivyo na idadi.

Suala nyeti kama wimbo wa taifa, ambao ndio kitambulisho chetu, iweje tuukwapue wimbo wa Afrika Kusini na kuufanya wetu?

Je, kwanini hatukuufanya wimbo wa Tazama ramani utaona nchi nzuri, uwe wimbo wa taifa letu?

Nadhani sasa ni wakati wa kurudi kwenye asili yetu, tutunge wimbo wetu wenyewe au tuufanye wimbo wa TAZAMA RAMANI uwe ndio wimbo wa taifa.
Kwani kuna tatizo? Tumekopa mambo mangapi kutoka kwa wenzetu?
 
Kwa hiyo we kwa akili yako unadhani tukibalisha wimbo ndo Mungu atasikia na kujibu maombi yetu? What a hectic! Wimbo wa Taifa sio km bongo fleva kwamba baada ya mda fulani unatoa remix.
Haha hahah kumbe wimbo wa taifa ni dua? Nani alikuwambia?
 
Back
Top Bottom