Huenda ni uvivu tulionao ndio unasababisha umasikini wetu na tumebaki kutafuta visingizio visivyo na idadi.
Suala nyeti kama wimbo wa taifa, ambao ndio kitambulisho chetu, iweje tuukwapue wimbo wa Afrika Kusini na kuufanya wetu?
Je, kwanini hatukuufanya wimbo wa Tazama ramani utaona nchi nzuri, uwe wimbo wa taifa letu?
Nadhani sasa ni wakati wa kurudi kwenye asili yetu, tutunge wimbo wetu wenyewe au tuufanye wimbo wa TAZAMA RAMANI uwe ndio wimbo wa taifa.
Sasa kuwa na wimbo wa asili ya kizaramo,kinyakyusa,kichaga,utasaidia nini katika mustakabali wa Taifa,kiuchumi,Elimu,sayansi??wimbo wa Taifa sio kikwazo,vijana wa siku hizi mbona mnawaza kinyume nyume?
Bora ungejiuliza,ulimwengu,ulaya/ujerumani uliilipa Israel kutokana na mauaji ya wayahudi milioni moja!
Waafrika milioni 36!walikufa kwenye biashara ya utumwa,ukoloni,lakini Afrika haijawahi kuomba fidia kwa nini?
Swali kingine kwanini Afrika hatuna tekinolojia ya kuchimba madini,mafuta,gesi,mitambo ya kuchimba yote hutoka ulaya,pale Nigeria mafuta yanachimbwa,yanasafirishwa kwenda USA kusafishwa,harafu yanarudishwa kuuzwa Nigeria,na Nigeria ndio ina watu waliosoma sana Afrika!!
Afrika ina watu milioni zaidi ya 759,je kwanini hatuna brand ya simu,gari,pikipiki,tv,ilitengenezwa Afrika?
Katika brand hizi,Toyota,Suzuki,ford,bmw,nk Brand iliyovumbuliwa na Mwafrika ipo wapi?
Kwa nini tunaagiza Sukari,mafuta ya kura kutoka nje,kwa nini hatuzalishi hapa?kwanini tunasubili wajapan waje kutufundisha kulima mpunga wakati tuna chuo Cha kilimo SUA,na maprofesa kibao?
Kwanini wabongo Richa ya kugandamizwa na ccm,hawahandamani,hawapigi kelele,wapo bize na mpira na habari za wake za wstu kuchepuka,hakuna kituo kinachoongelea mauaji ya polisi.
Hsyo ndio maswali ya kujiuliza,sio kuwaza vitu raini kama uji