Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Anayehubiri Upendo kwa Mungu na kwa jirani hawezi kuwa mwongo katika hilo.View attachment 3206930
Wanabodi, hakuna haja ya kuzungusha.
Hakuna ubishi.
Waanzilishi wa Ukristo na Uislam ni Yesu na Muhammad.
Hakuna ubishi kuwa hakuna anayejua namna hawa waanzilishi walivyofanana wala kuwa.
Hakuna ubishi, wakristo wana picha feki za wazungu waliomuigiza Yesu.
Hakuna ubishi, waislam hata walificha picha zote za Muhammad kwa vile anajulikana alizaiwa lini na wapi.
Hakuna ubishi kuwa dini mbili, licha ya kutoka sehemu moja na kuhubiri jambo moja, zote zina kila dalili za uongo kuhusiana na uwepo na malengo yake.
Je kuna haja ya mabilioni ya watu kuendelea kuamini dini hizi wakati ni ongo na zimejengwa kwenye uongo mtupu?
Siku hizi dini hasa imani ya kikristo ni kuwalisha watu mihadarati ya kiimani na kuwapumbaza watu akili ili wakupe pesa. Ni janga kubwa linalochangiwa na ubovu wa afya ya akili. Kila siku kuna mtume, nabii au mwalimu mpya anaibuka. Jina la Yesu limegeuka kuwa PANGO LA WEZI. Watakupiga soga zao za miujiza watafune pesa zao. Hakuna muujiza wowote wa kweli upuuzi mtupu. Nimeshauliza huyo Yesu wanayemhubiri hawezi kuponya amputees? Hakuna mhubiri yeyote aliejibu kwa hiyo nikisema miujiza yote wanayohubiri ni viini macho au otherwise they are scientifically curable ailments basi wakubali. Waiteni amputees kwenye matangazo yenu ya miujiza wakirudishiwa viungo vyao nitawaamini.Anayehubiri Upendo kwa Mungu na kwa jirani hawezi kuwa mwongo katika hilo.