Je, kuna mtu mwenye ushuhuda wa bati za chengachenga zilizowahi kupauka?

Je, kuna mtu mwenye ushuhuda wa bati za chengachenga zilizowahi kupauka?

King JiluX

Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
62
Reaction score
42
Kumekuwa na maoni kadhaa kuhusu ni bati kutoka kampuni ipi hasa ya kutumia wakati wa kupaua ukizingatia tofauti ya bei kutoka kampuni hizo, huku kukiwa na maneno kuwa kuna baadhi ya kampuni zinauza kwa gharama ya juu kisa jina tu la brand ila katika ubora kuna kampuni zenye mabati bora ila kutokana na kutokuwa na majina makubwa zimekuwa zikiuza bati kwa bei nafuu.

Kama ilivyo kasumba ya kiafrika kuwa chenye bei ndogo basi kitakuwa na quality ndogo, jambo ambalo siliamini hilo.

Leo nimekuja kwenu wana jamvi kuuliza iwapo kuna mwenye ushuhuda wowote kuhusu hizi bati zenye muonekano wa vigae na chengachenga kama kuna bati kutoka kampuni yoyote aliyowahi kuona ikiwa imepauka, maana nimezunguka binafsi sijawahi kuona bati za aina hiyo zilizopauka. Naalika ushuhuda kutoka kwenu. AHSANTENI.
 
Yaani mkuu unauliza utadhani wote tulifanikiwwa kujenga eehhh....
By the way mibado naishi home kwetu kama yesu pia bado anaishi kwa baba yake..😎
Suala la kujenga, kuishi nyumbani na kutoa ushuhuda wa kuona bati ya chengachenga kama huwa inapauka vinahusiana vipi great thinker??
 
Sasa mkuu siungeombaa ushauri dukani wanapo uza mabati yenye chenga...🙄🙄
Nini maana ya jukwaa kama nitaenda dukani ambapo utofauti pekee watakaorefer ni bei ya bati tu??
 
Nilifikiri haipauki, maana sio kwa hiyo bei, bahati nzuri nikaikuta njiani nikiwa safarini.... Inapauka mbaya mbovu. We jipange tu
 
Kama zina rangi lazima kuna kupauka!

Hao wanaoponda za bei juu (ALAF) kwa hoja ya kuwa wanauzia jina tu ni umasikini tu unasumbua.

Nikiangalia mapaa ya majirani hapa waliopauwa kwa bati za kichina,hali ni mbaya.
 
Kumekuwa na maoni kadhaa kuhusu ni bati kutoka kampuni ipi hasa ya kutumia wakati wa kupaua ukizingatia tofauti ya bei kutoka kampuni hizo, uku kukiwa na maneno kuwa kuna baadhi ya kampuni zinauza kwa gharama ya juu kisa jina tu la brand ila katika ubora kuna kampuni zenye mabati bora ila kutokana na kutokuwa na majina makubwa zimekuwa zikiuza bati kwa bei nafuu. Kama ilivyo kasumba ya kiafrika kuwa chenye bei ndogo basi kitakuwa na quality ndogo, jambo ambalo siliamini hilo.
Leo nimekuja kwenu wana jamvi kuuliza iwapo kuna mwenye ushuhuda wowote kuhusu hizi bati zenye muonekano wa vigae na chengachenga kama kuna bati kutoka kampuni yoyote aliyowahi kuona ikiwa imepauka, maana nimezunguka binafsi sijawahi kuona bati za aina hiyo zilizopauka. Naalika ushuhuda kutoka kwenu. AHSANTENI.
Mkuu pia ungeangalia sunshare wako vzuri
 
Kama zina rangi lazima kuna kupauka!

Hao wanaoponda za bei juu (ALAF) kwa hoja ya kuwa wanauzia jina tu ni umasikini tu unasumbua.

Nikiangalia mapaa ya majirani hapa waliopauwa kwa bati za kichina,hali ni mbaya.
Shukrani kwa ushauri.
 
Shukran kwa ushauri mkuu, ngoja nijaribu kuangalia hizo pia. Japo ALAF inaonekana ikipewa maua yake sana. Japo kuna wanaosema wanatumia jina.
Mkuu hata hao bei yao imesimama fulani. Bati zao hata gauge 30 iko poa we nunua fundi atakwambia.
 
Kama una mpango wa kupaua nakushauri tumia ALAF tu, tulionenga kwa bati za mchina Kila mmoja hakuna anaetamani kuliangalia paa lake, hasa kama unajiweza na ulifanya ukaidi.
 
Back
Top Bottom