Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna mzee alikuwa anapenda sana Tango ya Mandy na Dimpoz. Akifika baa anasema weka wimbo wa tango.Wakuu, Nataka kujua tu.
Hivi kuna aina za nyimbo mwanaume akizipenda ataonekana kama mtu asiyejielewa na pia kuna nyimbo mwanamke akizipenda ataoneka wa ajabu au asiyejielewa pia?
Kwa mfano chukulia umeenda gheto kwa mshikaji labda ana mke na watoto labda na kipara kwa mbali ameweka huu wimbo na anaimba
[emoji443]Nipo chuchu nipo Nyonyo aaah nimejaa teleee....[emoji3][emoji3][emoji443]
Au kuna Mdada kaolewa na ana watoto lakini au hana na anapenda nyimbo kama huu
[emoji443]Gusanisha hasi na Chanya mamaa weeee,Mabaharia toka buza tulifika.....waweke fresh tunarukaga ukuta....[emoji3][emoji443]
Tukuchulie wote hawa bado wako kwenye umri wa ujana,
Kwa kawaida kila mtu anapenda anachopenda huwezi kumpangia lakini kimtizamo je kuna nyimbo wanaume hawapaswi kuzishabika na pia kuna nyimbo wanawake hawapaswi kuzishabikia kwa sababu tofauti tofauti?
Karibu kwa maoni yako.