Je, kuna safisha safisha ya kisiasa inayoendelea nchi? Political purge!

Je, kuna safisha safisha ya kisiasa inayoendelea nchi? Political purge!

Je, kuna safisha safisha inayopita kushughulikia kwa namna mbalimbali?
Inaitwa 'purge' mkakati wa dola kulazimisha viongozi waachie ngazi.

Purge : Usafishaji wa safu za juu kisiasa unarejelea kuondolewa kwa lazima au kuondolewa kwa watu wanaochukuliwa kuwa wasiohitajika kutoka kwa taasisi ya kisiasa, kama vile serikali au shirika, na wale walio mamlakani.

Hii inaweza kuhusisha hatua mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kunyongwa, kufungwa gerezani, uhamisho, au kuondolewa tu kutoka kwa nyadhifa za ushawishi.

Usafishaji mara nyingi hutekelezwa ili kuunganisha mamlaka, kuondoa wapinzani, au kutekeleza upatanifu wa kiitikadi.

A political purge refers to the forced removal or elimination of individuals considered undesirable from a political entity, such as a government or organization, by those in power. This can involve various measures, including execution, imprisonment, exile, or simply removal from positions of influence. Purges are often implemented to consolidate power, eliminate rivals, or enforce ideological conformity.


Dr. Philip Isidori Nzabhayanga Mpango makamu wa rais kuamua kupumzika siasa.


Makamu wa Rais Dr. Philip Isidori Nzabhayanga Mpango, siasa basi naenda kuwa mkulima
1765469101630.jpeg


Na ndugu Kassim Majaliwa Majaliwa waziri mkuu naye kuamua kupumzika siasa


View: https://m.youtube.com/watch?v=x1OXBuo9sMg

Hakika mwaka huu 2025 viongozi wa juu kuamua kupumzika siasa, na kubakia bosi wao Dr. Samia Suluhu Hassan. Zile tetesi kuwa kuna mabadiiliko makubwa yanakuja

Je tutegemee pia mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano naye anaazima ya kuachia ngazi ndiyo maana ya kurefusha ukomo wa bunge had 03 Agosti 2025 bila kuelezwa sababu?

CCM MPYA CHINI YA UONGOZI MPYA KUONGOZA AJENDA YA NO REFORMS NO ELECTION

Kwa kuangalia kwa hali ya siasa Tanzania inaonesha uongozi wa juu kabisa kumekuwepo kutokukubaliana juu ya ajenda hii, na hivyo mmoja mmoja kuamua kuachia ngazi ili wote watatu wakipisha hoja za wanaotaka mabadiliko na kutoa nafasi uongozi mpya kuendesha mabadiliko.

Tumeona mwanadiplomasia, mwanasiasa aliyekulia ndani ya Umoja wa Vijana ya Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete siyo UVCCM ya John Pombe Magufuli wala ya Dr. Samia Suluhu Hassan ambapo UVCCM hao chini ya awamu ya 5 na 6 wamekuwa vijana wahafidhina machawa wasiotaka mabadiliko, waendekeza siasa za kibabe na kuchagua siasa chafu.

UTITIRI WA WAKUU WA MIKOA, MA-DC ambao ni wahafidhina, walazimishwa kuchukua FOMU za ubunge, waondoke kwenye mhimili wa dola :

1765469041428.jpeg

Photo : Paul C. Makonda

Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mahafidhina, legasi ya awamu ya 5 na 6 ambao kupitia kofia zao nyingi za kiuongozi kama wenyeviti wa Kamati za Siasa , Ulinzi na Usalama wanaonekana kuwa wanaweza kuwa kikwazo kwa dola kuongoza mabadiliko, hivyo waoneshwa mlango wa kutoka kupisha mabadiliko kwa kuambiwa wakagombee ubunge kwenye mhimili bunge usio wa dola. Hii inaitwa wavute karibu hata wape unaibu waziri, uwathibiti.

NINI KIMEFANYA CHAMA KONGWE KUJITATHMINI NA KUFANYA MAGEUZI NDANI YA MFUMO, ILI KIWEZE KUBAKI MADARAKANI
Uchaguzi wa mwaka jana nchini Mozambique (2024) ambapo chama rafiki cha CCM chama cha FRELIMO kiliamua kutoka kwenye utaratibu wa mazowea na kumteua Daniel Chapo kuwa mgombea, kada aliyetoka nje ya MFUMO uliozeeleka .

CCM baada ya kujithamini kutokana na wimbi kubwa la kudai mabadiliko ndani ya chama, na pia kutoka nje kwa watanzania wasio wana CCM imeona sasa ijivue 'gamba' kiukweli ingawa 'mnyama' huyu atabaki yuleyule katika muonekano mpya wa ari ya kupenda mahitaji ya umma wa waTanzania wa kipindi cha sasa.

HALI HALISI NDANI YA CHAMA KONGWE

MWENYEKITI CCM WILAYA ANASWA AKIMTETA MWENYEKITI WA TAIFA, MWENYEWE ARUKA MITA MIA"​


View: https://m.youtube.com/watch?v=jMSRjSDTZvk
mazungumzo haya yaliyonaswa ni miongoni ya mazungumzo mengi yanayoendelea katika vijiwe, minada, magulio, mwalo na pwani za uvuvi, sokoni na katika majumuiko ya watanzania.

Hapo utasikia raia bila kujali vyama vyao vya kisiasa wakioneshwa kutoridhishwa na mengi yanaendelea katika siasa, usalama, uchumi, haki na maendeleo ya watu


Bila kusahau watu wasiojulikana wanaoonekana, kuwakera viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama kwani wasiojulikana wamekuwa nje ya mfumo rasmi wa vyombo hivyo.

Vikundi hivyo tayari vinaweza kutishia usalama wa nchi kwa kuonekana kuwa na nguvu kuliko vyombo rasmi vinavyo tambulikana kikatiba
 
Ingekuwa vyema kumuuliza mhusika, sisi tunajuaje? Tumekuambia sisi kitu?
 
Mkuu wa nchi alitamka mbele ya wazee Dar. Kuwa kuna watu walitaka kuangusha dola hiyo tar 29 Oktoba. Hii kauli imenishutua sana. Na mpaka leo huwa natafakari.

Kwamba kulikuwa na watanzania waliotaka kuingia Ikulu na kukamata dola kwa kutumia vijana na watu waliondamana wakidai kuchoshwa na ufisadi na upendeleo wa mafidi wa CCM.

Kwa mantiki hiyo kuna Watanzania na wanasiasa ambao hawamtii na hawakubaliani na utawala wa Rais Samia.

Je, kuna safisha safisha inayopita kushughulikia kwa namna mbalimbali?
Kichwa cha mada; na maelezo yake yote ni batili.

Uchafu utajisafishaje uonekane umetakata?

The topic is not properly thought out for usefull discussion.

Hizi mada nyingi zinatungwa na kuletwa zijadiliwe bila ya kuzipa fikra za kutosha.

Utaniwia radhi kwa maoni hasi haya; lakini ndio uamini wangu juu ya mada yako hii

Samia anao usafi gani wa kusafisha wengine?
 
Kichwa cha mada; na maelezo yake yote ni batili.

Uchafu utajisafishaje uonekane umetakata?

The topic is not properly thought out for usefull discussion.

Hizi mada nyingi zinatungwa na kuletwa zijadiliwe bila ya kuzipa fikra za kutosha.

Utaniwia radhi kwa maoni hasi haya; lakini ndio uamini wangu juu ya mada yako hii

Samia anao usafi gani wa kusafisha wengine?
Naomba utulie na kisha ufanye utafiti kwa kina. Hakuna mahala nimesema Rais Samia ni msafi
 
Sio kweli. Fanya utafiti. Tulia fanya utafiti juu ya political purge inayofanyika
Basi inawezekana ulikuwa na lengo tofauti na jinsi ulivyowasilisha mada yako..

Kichwa cha mada kinasema :"...Safisha safisha ya kisiasa..."; na huko ndani ya maelezo yenyewe kunaelezea 'purge' ya wasiokuwa "safi" kisiasa au wasiokuwa safi kivipi?

Kama nilivyoandika mwanzo, hii mada hukuipa tafakuri stahiki ulipoamua kuileta hapa ukumbini.
 
Back
Top Bottom