Je, Kuna Taasisi ya ovyo Kabisa Nchini Kuizidi TANESCO?

Shirika limejaa mateja 95% unategemea tija itoke wapi
 
Mama yangu Samia Kama utapita hapa please Niko chini ya miguu yako. Ombi nalitoa kwako binafsisha TANESCO.
 
Huwa nazikwepa Sana thread za Tanesco maana hawa ni mapepo pasee, ukianza kuwataja hapohapo ulipo wanawakatia umeme uwaseme vizuri.

Ndio sababu hakuna thread sitakagi kabisa kuchangia kama hizi hasa Leo jumapili nimepumzika home hawakawii kukuharibia siku.
 
CCM, baba kazaliwa kakua kasoma kamaliza katafuta mchumba kaoa wamezaa mtoto anatembea, bado mama, baba na mtoto wao wanakwenda mbugani kuchota maji kwenye gema ambalo tembo alichimba kwa ajili ya matumizi yake na mwae, eti mama ameupiga mwingi.

Na ndiyo maana kipindupindu kina mkataba wa kudumu na Serikali ya CCM.
 
Katika serikali iliyoongozwa na JPM walikuwepo baadhi ya mawaziri waliozitendea haki wizara ngumu walizopewa dhamana ya kuziongoza. Mojawapo alikuwa ni Mh. Lukuvi ambaye kwa kiasi kikubwa aliitendea haki Wizara ya Ardhi na kuweza kufanikiwa kutafuta ufumbuzi wa migogoro mingi ya ardhi nchini.

Sijui hata ni kwa nini mkongwe kama huyu hakuweza kuaminika na kisha kupewa unaibu waziri mkuu na uwaziri wa nishati ili aweze kuuadabisha uongozi na wafanyakazi wa TANESCO!?

Hivi katiba inamruhusu ex-CAG Mussa Assad kuteulwa kuwa mwenyekiti wa bodi katika shirika hili!? Mtu kama huyu kwa hakika angaliweza kufanya mageuzi makubwa katika shirika lenye utata mwingi kama hili.
 
Tatizo nchi yetu, Raia tunalalamika, utakuta kiongozi mkubwa naye analalamika. Tanesco kinachowasumbua wanatumika sana kisiasa, ilibidi watolewe kwenye monopoly waruhusu ushindani kutoka makampuni binafsi.

Linawezekana ila wanajua wakiwekwa kwenye ushindani watapotea kama ttcl
 
Na Watanzania kwa kuzoea matatizo imekuwa jadi yetu tunaona sawa tu kukaa siku nzima bila umeme.

Hii mentality ndio inapelekea baadhi ya viongoz kutuchkulia poa , they dont care kwa sababu hata waki underperform hamna lolote mtawafanya, mtavumilia as usual
 
Hiyo mitambo ni ya kisasa, ikihisi hatari inajizima, na haiwaki mpaka hatari iishe, watu wanataka iendelee kuwaka wamulike vitambi vyao walivyoshiba magimbi at the risk ya mitambo kuungua
Mitambo hiyo hiyo ndio imefungwa ujerumani, uingereza na china. Mbona huko haijuzimi?
Tafuta sababu nyingine.
 
Relax na jitahid atleast uwe normal,

wanadamu tumeumbwa kusahau na zadi sana kujipa umuhimu nkubwa na wa taofauti sana na binadamu wengine...

bila mihemko na ghadhabu ndipo unaweza kuelewa na kujifunza jambo..
vinginevyo ntasema mfano huu juu ya hoja ile, utaacha hoja utadandia mfano kwa maswali yasio muhimu na matokeo yake ni kupoteza wakati bila sababu...

mwenye maskio aliskia mikakati ya serikali kuhusu tataizo la umeme na wenye uelewa waneketi tuli wakisubiri ilichoahidi serikali juu ya jambo hili...

nyie wengine wa negativity hakuna namna tunaweza wasaidia katika muondokane na hiyo negativity....
 
Tanesko na Dada yake Nida wanaoboa mno Ila Tanesko hapa mpinzani, Tanesko ni kijana/mzee wa Hovyo.
 
Tanesko na Dada yake Nida wanaoboa mno Ila Tanesko hapa mpinzani, Tanesko ni kijana/mzee wa Hovyo.
Kama wazee wanawaacha wake zao nyumbani na kwenda kufanyiwa massage Sinza na kuacha laki huko.
 
Na wanalipwa mishahara na posho! Za kazi Gani sasa. Tanesco ifutiliwe mbali tuanze upya
 
Hiyo mitambo ni ya kisasa, ikihisi hatari inajizima, na haiwaki mpaka hatari iishe, watu wanataka iendelee kuwaka wamulike vitambi vyao walivyoshiba magimbi at the risk ya mitambo kuungua
Utakuwa mmoja wao bosi.
Hatar ya aaje kwamfano jombaa
 

Acha kuzuga wewe ni mfanyakazi wa Tanesco na uko kitengo cha imejensi, nani asiyekujua.
 
Sasa kama akili zinawaza ngono 24/7 Unafikiri akili ya kuwaza maendeleo na nia ya dhati ya kuyapigania itatoka wapi?
 
Umeme usingekuwa tatizo mpaka leo kama wasingevuruga uchaguzi, wanaficha lkn ukweli ndio huo.
 
Shida kubwa sio shirika,bali nidhamu katika mtiririko wa kimajukumu.
Nchi hii mwanasiasa ana maamuzi kuliko mtaalamu.
Nchi hii pia,hata uwe na PhD ya kitu flani
Lakini amini usiamini std 7,4m4 mwenye cheti Cha veta aliyepenya kwenye siasa na kumpata cheo ndo huyo huyo atakaetaka mawazo yake yafanyiwe kazi na sio utaalamu.

Mpangilio huo hakuna wa kulaumiwa zaidi ya Ccm inayokataa mchakato wa Katiba mpya.

Kama democrasia inafana,mbona Marekani yenye wananchi zaidi ya 200m wana vyama viwili na pia Katiba Yao ni kwamba,haijalishi unatokea malengo gani.ila ukifika White House. Unakutana na sela za Nchi,na sio sela za chama Wala za kwako binafsi.

Kwetu tumejaza vyama mfu rukuki ambavyo havina tija Kwa taifa ambavyo mnufaika ni huyu jinamizi CCM.

Viongozi wa kisiasa wamekuwa ndo wenye sauti kuliko wataalamu.

Hivyo,usikute tatizo la Tanesco linaanzia Kwa wanasiasa.

Watumishi mtawasurubisha bule,ila tatizo lipo kemwenye vyeo vya KISIASA.Na sio kwenye vyeo vya kiutendaji.
 
Sisi wengine tinaangalia zaidi vitendo kuliko hadithi.

1) Makamba alisema kuwa umeme umekuwa wa shida kwa sababu wakati wa kipindi cha awamu ya 5, hakukuwa na service ya mitambo, hivyo mitambo sasa hivi inafanyiwa matengenezo, baada ya matengenezo, mgao utakuwa historia. Je, tatizo la umeme lilikuwa historia au ni maisha ya kila siku?

2) Baadaye Makamba alisema kuwa, kuna upungufu wa maji. Tatizo la mgao litaisha mabwawa yakijaa maji. Je, tatizo la mgao wa umeme limeisha?

3) Mvua zilipoanza kunyesha, hadithi ikabadilika, ikawa tatizo la umeme linasababishwa na miundombinu, hasa nguzo kuoza. Wakasema tatizo litaisha baada ya kukamilisha ubadilishaji wa nguzo kutoka za miti na kuwa za zege. Baada ya hilo zoezi kukamilika maeneo mengi, kumekuwa na utofauti wowote?

4) Sahizi hadithi imebadilika na kuwa linasubiriwa bwawa la Nyerere, kuanzia mwezi wa pili tatizo la umeme litakwisha, tena hiyo ni kauli ya Rais. Mwezi wa pili ni wiki tu hii ijayo, wewe unaona kuna hata dalili?

Matatizo humalizwa kwa kutenda siyo kwa ngonjera za mdomoni. Kuna watu Serikalini na huko TANESCO wanataka kumaliza tatizo la umeme kwa hadithi za mdomoni!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…