naam sasa mmeanza kuelewa kwamba falsafa ya dini ndiyo inayoleta maendeleo na utu wa binadamu, mfumo unaotawala Dunia leo hii ni western christianity hivyo yoyote ambaye hafwati christianity ( western) way of life hawezi kuendelea.
na ndio maana nchi zinafwata uislamu afrika ni shida tupu kuanzia somalia, chad, maurtania na kwingineko pakistani, irani au hata yemeni.
HAPANA. UKRISTO HAUTAWALI ULAYA.
Jamii yoyote ile huongozwa na falsafa.
Ulaya kwa miaka mingi imekuwa na vita za kidini hadi miaka ya 1600 wakati wa Makubaliano ya Amani ya Westphalia. Enzi ambazo ukristo umetawala Ulaya, MAUJI YALISHAMIRI Mf Kanisa liliua sana wasio wakristo(wapinga kanisa), wayahudi waliua ulaya yote sababu ya Ukristo, HAKI ZA BINADAMU ZILIKUWA CHINI SANA, UBAGUZI WA KIJAMII, WANASAYANSI WALIOPINGANA NA UKRISTO WALIUA, MAGONJWA YALISHAMIRI ULAYA KWA SABABU YA 'UJINGA ULIOLELEWA NA DINI' Mfano Black Plague Kanisa lililazimisha watu wajifungie makanisani kusali na kusingizia Wayahudi eti ni wachawi ndio walioleta ugonjwa huo n.k n.k!
Ni hadi kufikia Miaka ya 1600 ndipo Ulaya ikaanza kubadilika:
• Hadi leo bado
Warumi 13:1-4 inasema Mamlaka hutoka kwa Mungu na Tiini Mamlaka—waliachana na Tawala zinazodaiwa kuwekewa na Mungu (Divine Right to rule) mf za kina king Louis XVI wa ufaransa; na kuanza kuhoji tawala zao, kuziwajibisha, kinyume kabisa na Ukristo unavyosema, Wazungu wakasema Mamlaka hayatoki kwa Mungu bali wananchi. Ndio imewapa Uwajibikaji wa Viongozi, Kupambana na Rushwa hivyo DEMOKRASIA NA UTAWALA BORA kwa Ujumla.
•
Hadi leo bado 1 Timotheo 2:12 haijabadika na Ukristo unakataza wanawake kuongoza, kupewa mamlaka au kuwa sawa mbele ya wanaume,
lakini Wazungu wanasimamia usawa na kijinsia na Haki za wanawake na Kina Margaret thatcher, Theresa May, Merkel wamekuwa watawala ingawa Ukristo hauruhusu.
•Biblia bado iko vile kwenye
Walawi 20:13 hivyo ukristo hadi leo hii Mashoga, Wasagaji wanapaswa kuuawa, lakini
Wazungu wamewapa haki jamii hii na hadi leo wanaona, viongozi mashoga wapo, Luxembourg Mke wa Waziri Mkuu miaka ya 2016 alikuwa ni Shoga.
So,
Ulaya imendelea sana pale raia 'walipomnyanganya Mungu wa Kikristo' madaraka ya kuongoza na kuyaweka Mikononi mwao wananchi wenyewe.
Falsafa za Kina Immanuel Kant za kutumia Fikra, Sayansi na Utu— HUMANISM [Enlightenment era], ndio ziliwafanya waanze kuhoji watawala badala ya kutii DEMOCRACY, waanze kutaka usawa wa kijamii badala ya kupangiwa matabaka HUMAN, POLITICAL & CIVIL RIGHTS, waanze kuchunguza nini kinatokea kwenye miili ya binadamu badala ya kukubaliana maandiko na imani juu ya magonjwa DEVELOPMENT OF MEDICINE.
Ukristo ulaya imepitia zama za Mwangaza, lakini Uarabuni falsafa hizo hazikufika. Ndio maana hadi leo bado nchi hizo zinatawaliwa na kuwa katika hali ya 'giza'. Jamii yoyote inayoongozwa na Dini [Revealed knowledge] kamwe haiwezi pata maendeleo.