Je, kuna ubaya Tanzania ikavikwapua na kuvifanya visiwa vya Comoro sehemu ya Tanzania?

Je, kuna ubaya Tanzania ikavikwapua na kuvifanya visiwa vya Comoro sehemu ya Tanzania?

Hapo walipo wapo ndani ya muungano na wana Rais mmoja wa muungano japo kila kisiwa kina Rais wake.
That is very good, hyo federal president ndio atawawakilisha katika Muungano, hao wengine watakuwa wakuu wa mikoa sasa(ma - RC) kama Makonda tu..
 
Tukishavikwapua comoro, na utaleta uzi mwingine tukwapue na shelisheli haiko ivo mkuu ndio mana tumemdunda iddi amin.
 
KWA KUWA RAIS WAO ALISHAOMBA MARA NYINGI TU TUUNGANE NAO SIONI TATIZO ISIPOKUWA MAMBO HAYA YAFANYIKE HATUA KWA HATUA,HUKU JESHI LAO LIKISATENDA MAMLAKA KWA JWTZ,TANZANIA ITAKIWA KUBWA NA IMARA NA SOKO LETU PEKEE LITAKUWA KUBWA MNO.
 
Muulize kilichomkuta Sadam baada ya kuivamia na kuikalia kijeshi Kuwait.Kwa nguvu gani iliyonayo Tanzania ukawaza hayo?
 
Ndoto nzuri. Lakini kama tumeshindwa kutatua "kero za muungano" na visiwani kwa miaka yoooote, tukijiongezea visiwa vingine si ndio tutakuwa tumejiweka vibaya kabisa?
Ameshataga huyo sasa kakolea anataka kuzaa kabisa!
 
KWA KUWA RAIS WAO ALISHAOMBA MARA NYINGI TU TUUNGANE NAO SIONI TATIZO ISIPOKUWA MAMBO HAYA YAFANYIKE HATUA KWA HATUA,HUKU JESHI LAO LIKISATENDA MAMLAKA KWA JWTZ,TANZANIA ITAKIWA KUBWA NA IMARA NA SOKO LETU PEKEE LITAKUWA KUBWA MNO.
Mkuu una hakika na hili ulisemalo?
 
Huwezi "kukwapua" kidiplomasia. Huo ni ujinga.

Halafu eti tutatuma wanadiplomasi. Ulikuwa hata huelewi kuwa tuna diplomats tangu zamani sana huko Comoro na wala huelewi kuwa tuna mahusiano na mikataba ya ushirikiano. Hivi huwa mnalala mnaota au mnakuwa mmevimbiwa maharage na dona?

Stupid ideas.
Naona unataka kumzidi kete ndugu yangu nitavalia njuga huu mjadala unikimbie ajuza shauri yako
 
KWA KUWA RAIS WAO ALISHAOMBA MARA NYINGI TU TUUNGANE NAO SIONI TATIZO ISIPOKUWA MAMBO HAYA YAFANYIKE HATUA KWA HATUA,HUKU JESHI LAO LIKISATENDA MAMLAKA KWA JWTZ,TANZANIA ITAKIWA KUBWA NA IMARA NA SOKO LETU PEKEE LITAKUWA KUBWA MNO.
Sasa kama aliomba kuungana tunasubiri nini???!, umoja ni nguvu, si unaona Zenji walivyo powerful? Leo hii hata wale waarabu wa Oman hawatii pua pale.., wako very safe.
 
Zitumike mbinu za kidiplomasia, ikishindikana kwa ustaarabu basi liundwe zengwe na vikwapuliwe kwa nguvu, maana wanasema umoja ni nguvu, ni kama Zanzibar tu ikivyonyakuliwa. Nasema hivi maana kuna kitu cha ajabu sana nimekigundua baada ya kuencounter wacomorro kadha wa kadha katika mizunguko hasa ya Kariakoo.
Kiukweli hawa watu wanajiina ni waTanzania kamili kabisa, na wanataka haki zote sawana mTanzania mwingine yeyote yule. Yaani uFaransa anatoka alikotoka kisha anakuja uwani kwetu kumiliku kisiwa, huu ni upunguani wa wapi huu?

Tunaomba tupewe historia ya Commoro kwanza ili tujue tulikwama wapi?

Moja ya manufaa makubwa sana ambayo nimeyaona kwa integration tuliyoifanya na Zanzibar ni 'huge economic, social & political cooperation', fikiria ni kwa urahisi kiasi gani Tanesco imeweza kuuza umeme mwingi sana visiwani bila vikwazo vyovyote, fikiria namna wanafunzi wanapokuja kusoma vyuo vikuu vya bara na kupata mikopo minono ya Heslb bila hiyana wala vikwazo vyovyote vile, pia ona jinsi watu toka visiwani wanavyokuja kupata ajira na kufanya biashara bara bila usumbufu, fikiria jinsi bara tunavyoagiza maziwa toka Zanzibar bila shida yeyote ile, faida ni lukuki.

Lakini ninachokisikia kwa chini ya kapeti ni kwamba kisiwa kimoja wapo cha Comoros kinachomilikiwa na wazungu kinatumika vibaya kutunyonya na kututikisa, mfano eti kuna wakati walikuwa wananunua ng'ombe maelfu kwa maelfu, wanapelekwa hapo kisiwani, wanachakatwa kisha nyama kupelekwa paris, lakini kiutaratibu walipaswa watengeneze kiwanda cha kuchakata hizo nyama hapa nchini kisha zisafirishwe kwenda paris tokea hapa na mapato stahiki ya kodi ya baki hapa, huo ni mfani tu.
Kingine ni Tax evasion techniques kama zile zinazofanyika visiwa vya Seychelles, ni kwamba kampuni inacheza sarakasi kwa kutumia mamlaka za visiwa zilizopo karibu na nchi yako, hivyo wanakuja kufanya biashara kwako lakini base yake anaiweka uwani kwako ambapo huwezi kumfikia sababu ni mamlaka ya mtu mwingine, hii michezo ilitaka kufanyika kwa kuitumia Zanzibar hasa katika uagizaji wa sukari na spea za pikipiki, lakini kwakuwa tuna-control na Zenji ilikuwa ni rahisi kwetu kudhibiti hali hiyo.

===============================

===============================

Likes 15 tayari [emoji3][emoji106][emoji122][emoji123]


Zanzibar na mafia zimewashinda mnataka Comoro? Mafia hakuna usafiri wa uhakika , Zanzibar ni aksante Barekhsa.
 
Nyerere angekuwa makini kidogo,Uganda lingekuwa koloni letu,nchansi ya kuingiza jeshi mle ilikuwa golden chansi,wazungu wachina wakitua mahala jeshi hawaondoki kirahisi.Hivi tulishindwa kuikalia Uganda walau miaka 10.Tungevuna Kodi kufidia vita.Hilo kosa lisije kujirudia tena iwapo tutapata kachansi ka kuingiza jeshi mahala.On a wenzetu Kenya wanajivunia tu Kule Somalia sisi tulishindwa nini Comoro hali nchi tuliitwaa ndani ya Siku mbili.Islaeli wakifanikiwa kushinda vita wanaikalia ardhi milele,sisi tunashindwa wapi? Tukumbuke Afrika inabidi iwe moja na haiwezi kuwa kwa mwendo was sasa Ila inahitajik ubabe uje utumike.
 
hapo zenjiber tu kamas zinatutoka ndio ije kuwa comoro?pale wana visiwa vitatu kama zenji vyenye wakaazi,kutokana na fujo zao za uchaguzi sasa wameamua hakuna kupiga kura ila wanafanya zamu ya kutawala kila kisiwa kinatoa mtu wao .
miaka michache nyuma mmoja wa rais wa kisiwa kimojawapo aligoma kuachia kiti ndio akatimuliwa na wanajeshi wa tz bila hata risasi kuruka wafuasi waliposikia zogo la nyimbo za kuhamasisha kuto kwa wajeda wetu kakikimbia mbio tena kajifanya demu asinyakwe
Kwanza ni mzigo,ni kisiwa ambacho siyo productive,ardhi kubwa ni matumbawe hailimiki,ni tabaka la watu wavivu wanaotegemea ndugu zao waliopo ufaransa.sasa tuwachukue wa nini?tupambane na kina hami j wetu
 
Back
Top Bottom