Wewe punguani kwelikweli huyo anaetajwa kwenye Yeremia 17 ni Yesu? Kawadanganye wengine...
Sasa unafikiri ni nani? Yesu hajatajwa kama bwana sehemu moja nikianza kuleta mistari aliyoitwa bwana tutakesha, alianza kutabiriwa kuanzia kitabu cha mwanzo (Genesis)
Punguani mama yako.
Soma juu kidogo hapo aya ya 5...
5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
Naaam wala hujakosea bi ajuza naona umemtaja Yesu kabisa (BWANA)
.
Yesu si mwanadamu ila alikuja kwa njia ya mwanadamu nalilikuwepo kusudi kwanza tuanze kujua mahala kwingine alikoitwa bwana.
.
Warumi 12:19-20 maandiko yana sema, Wapenzi, msijilipize kisasi, Bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; Mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyavyo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
.
Kamjadala kalikuwa mimi nina mabwana nikakataa nikakuambia nina bwana nae ni huyu (Yesu Kristo aliyehai)
.
Haya turudi kwenye hiyo Yeremia 17:5 kwamba amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu hii ilikuwepo kabisa kumbuka Yeremia ni kitabu cha Torati watanisaidia na wengine siandiki mengi.
(Torati=Sheria za Musa kwa wana wa Israel walikataa uzima Mungu akawapa sheria ya mauti)
.
Yesu si mwanadamu ila alikuja kwa vazi la kiuanadamu ili kusudi la Mungu litimie na kusudi lake lilikuwa nini?
Bibilia inasema:"Yule amwaminiye Mwana ana uzima wa milele: na yule asiyemwamini Mwana hatauona uzima; ila ghadhabu ya Mungu hukaajuu yake.” (Yohana 3:36
.
Kusudi.
🌻🌻🌻
10:1 Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.
10:2 Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi?
10:3 Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka.
10:4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.
10:5 Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema,
Dhabihu na toleo hukutaka,
Lakini mwili uliniwekea tayari;
10:6 Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo;
10:7 Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa)
Niyafanye mapenzi yako, Mungu.
10:8 Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati),
10:9 ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili.
10:10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.
10:11 Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.
10:12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;
10:13 tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake.
10:14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.
10:15 Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia; kwa maana, baada ya kusema,
10:16 Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana,
Nitatia sheria zangu mioyoni mwao,
Na katika nia zao nitaziandika;
ndipo anenapo,
10:17 Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.
10:18 Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.
.
Tusiharibu uzi twende jukwaa la dini