Je, kuna uhusiano gani kati ya kwenda hijja na harakati za uganga ama tiba za kisuna?

naona wewe unaongelea wale wanaojisomea nyumbani
ungeniuliza kwanza, nimesomea wapi hiyo Quran na kwa miaka mingapi na nimegraduate level gani ?
Bila kusahau kuniuliza na Biblia nimesoma Level gani
Nafikiri utaweza kujua kuwa unayebishana naye anaweza kuwa mfasiri wa hiyo Quran
 
Ukweli ubaki kuwa ukweli , hakuna binadamu anaweza elewa Koran bila tafsir , hili tumemaliza
 
kama wewe ni mkristo umeshawahi kuwaza kwanini wakristo wanaabudu masanamu? Tena yapo hadi makanisani,
hao sio wakristo ni wapagani tu kama waislamu, UKRISTO HALISI UNAKATAZA SANAMU

Kutoka 20:4-6​

Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
 

Mk 16:16 SUV​

Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
Mkuu nje ya mada ww msabato?

Ila mimi binafsi naona dini zote zina mapungufu yake, hakuna iliyokamilika. Tuishi kwa upendo na tusizisemee zingine vibaya. Dini zenyewe tuliletewa tu.
 
Hapana, jina la Kiislaam ni jina lolote zuri, lenye maana nzuri. Siyo jina ambalo hata kulitamka mbele ya watu ni kazi. Mfano mtu anaitwa M'boro. Inahusu nini.

Kuna Waarabu ambao siyo Waislam.
Nimependa maelezo yako.
Sawa mfano Eric lina maana nzuri niliwahi kusoma maana yake kwa wenye lugha yao. Je, ni la kiislam pia? Itafaa kwa muislam kumuita mwanae hivyo? Msaada tafadhali
 
Mkuu nje ya mada ww msabato?

Ila mimi binafsi naona dini zote zina mapungufu yake, hakuna iliyokamilika. Tuishi kwa upendo na tusizisemee zingine vibaya. Dini zenyewe tuliletewa tu.
Hilo ni neno la MUNGU ndugu,si maneno yangu,mm nimenukuu tu
 
Sio "twasema". Wewe kabla ya kubatizwa ulikuwa dini ipi?

Unajuwa maana ya Uislam?
Mwasema hivo, mimi ni mkristo hata kabla sijabatizwa coz niliishi kwa kufata misingi ya dini hiyo.

Uislam ni dini kama ulivyo Ukristo.
 
Mwasema hivo, mimi ni mkristo hata kabla sijabatizwa coz niliishi kwa kufata misingi ya dini hiyo.

Uislam ni dini kama ulivyo Ukristo.
Swali la kwanza, unajidanganya kuwa uliishi "Kikristo". Hakuna kuishi Kikristo kwa kuwa Ukristo sio mfumo wa maisha.

Wewe ni mkristo wa "kanisa" lipi?

Nimekuuliza nini maana ya neno "Uislam". Huwezi ufananisha Uislam na Ukristo kwani hata maana ya maneno hayo mawili ni tofauti kabisa kama mbingu na ardhi. Labda hata maana ya neno Ukristo huielewi. Kama unaielewa tufahamishe uelewavyo.
 
"Kuna uhusiano gani kati ya kufanya hijja na uganga" hii ndio mada.

ila kwa bahati mbaya watu wameshindwa kujikita katika mada na wameamua kuzipambania dini zao.

Anyways!,jibu ni kua uislamu umekataza mtu kufanya shirki,Na mtu ambaye atafanya shirki uislamu unasema kua huyo mtu makazi yake ni jehnamu(Motoni) katika siku za mwisho za hesabu.

Endapo mtu akitoka hijja halafu akafanya shirki,huyo mtu atakua amefanya hivyo kwa mlengo wake binafsi na sio muongozo wa dini,Ni sawa na padri akizini haitobadilisha chochote ukatoliki.
 
Kuishi kikristo ni kuish kadri ya vitabu vya dini ya kikristo vinavyoelekeza.

Uislam ni kama ukristo zote ni dini tu.
Mnadanganyana tu huko kujifanya soo special zaidi ya wengine na hiyo ni mbaya kwa afya ya akili zenu.
 
Ingia hapa nenda kafute , na uwaletee noma kwa nini wameandika hivyo
 
Nimependa maelezo yako.
Sawa mfano Eric lina maana nzuri niliwahi kusoma maana yake kwa wenye lugha yao. Je, ni la kiislam pia? Itafaa kwa muislam kumuita mwanae hivyo? Msaada tafadhali
Sifahamu maana ya Eric. Kwanini liwe Eric? kuna mashujaa wa Kiislam wengi sana na wana majina mazuri mazuri. Eric maana yake nini na lina historia ipi?
 
Hiyo ni divide and rule. U sunni na Ushia ni siasa tu, sio mafundisho ya Kiislaam. Katika Uislam hakuna Shia wala Sunni, ni majina ya kujipachika watu tu hayo. Uislam unafundisha mtu kuwa "Muislam".

Unafahamu maana ya Uislam?

Wewe wa kanisa lipi?
 
Sifahamu maana ya Eric. Kwanini liwe Eric? kuna mashujaa wa Kiislam wengi sana na wana majina mazuri mazuri. Eric maana yake nini na lina historia ipi?
Eric maana yake forever ruler limetokana na Ujerumani ya kale.
 
Dini zina mapungufu sabab ni matokeo ya binadamu kujiamulia kwa utashi wake namna ya kuntafuta Mungu.

Skuona mahali kwenye biblia Mungu alimpa dini mwanadamu.
Dini NI biashara ( unyang'anyi ) nafkiri Yesu alikuja kuharibu bizness za watu wakaona wasimkawize.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…