Je, kuna uhusiano gani kati ya kwenda hijja na harakati za uganga ama tiba za kisuna?

Hivi ni "kuamrisha" au kuelekeza?
Nguzo ya Kuhiji katika Uislam ni amri ambayo Kiislam huitwa "faradhi", sio elekezo. Kumbuka hilo.

Uislam una nguzo tano, mojawapo ni Hijja. Zifahamu nguzo tano za Uislam...

Nguzo tano za Uislamu (kwa Kiarabu: أركان الإسلام arkan al-islam, pia أركان الدين arkan ad-din yaani nguzo za dini) ni ibada au matendo yanayoaminiwa kuwa ya kimsingi katika Uislamu. Zimepata hadhi maalumu kwa sababu zinatajwa katika "hadith ya Jibril". Kwenye masimulizi ya hadith ile malaika Jibril alimwuliza Mtume Muhammad "Uislamu ni nini?" na huyu alijibu kwa kutaja matendo matano yafuatayo.

Kwa kawaida hizi nguzo tano zinafundishwa katika madhehebu ya Wasunni jinsi inavyoonyeshwa hapo chini.

Washia hawahesabu shahada kati ya nguzo tano wakiona shahada pamoja na imani ya Kiislamu ni msingi wa nguzo tano, halafu wanaongeza "wilayat" yaani kukubali uongozi wa Maimamu kama nguzo ya tano.

  1. Shahada: (Kiarabu: الشهادة) Nguzo ya kwanza katika Uislamu hujumuisha kutoa kauli mbili: Hakuna Mola apasaye Kuabudiwa ila Allah na Muhammad ni Mtume wake. Kauli hizo hutolewa pale mwanadamu anapoingia Uislamu.
  2. Salat: (Kiarabu: صلاة‎) ni sala inayofuata utaratibu maalumu mara tano kila siku: Asubuhi, mchana, alasiri, jioni na usiku. Kabla ya kuingia katika ibada hii Mwislamu anapaswa kufanya wudhu ambayo ni tendo la kutakasa mwili kwa maji au -kama hakuna- kwa kutumia vumbi badala yake. Salat ina maneno yake na pia namna ya kusimama au kujinama. Salat hii ni tofauti na dua (دعاء) au sala ya kuomba kwa hiari.
  3. Zakat: (Kiarabu: زكاة‎‎) Nguzo ya tatu ya Uislamu nayo ni ibada inayomuelekeza Mwislamu kuwaangalia Waislamu wenzake kwa hali na mali, na kushughulikia mahitaji yao ya maisha, kwa kutoa fungu la mali yake asilimia 2.5 kila mwaka kwa mwenye uwezo na kuwapa wale walio maskini na wasiojiweza ili nao waweze kuishi vizuri.
  4. Funga/Saumu: (Kiarabu: صوم) Wakati wa mwezi Ramadani kila Mwislamu anapaswa kufunga chakula na kinywaji chote kuanzia asubuhi hadi jioni. Watoto na wagonjwa hawapaswi kutekeleza wajibu huu. Waislamu wanaona maana ya ibada hii kumkurubisha Mwislamu na Mola wake na kumfanya amche na kumuogopa zaidi, kwani saumu humsaidia Mwislamu kufahamu shida na taabu ambazo wale wasiokuwa na uwezo wanazipata wakiwa na njaa na hawana cha kukila, na kwa hivyo, huingiwa na huruma na kuwa na moyo wa kutaka kuwasaidia na kuwaondoshea shida hizo.
  5. Hajj (Kiarabu: الحجّ alhajj): Kila Mwislamu mwenye uwezo anatakiwa kwenda hijja Maka mara moja katika maisha yake wakati wa mwezi Dhul-Hija. Nguzo hii inawapa fursa Waislamu ulimwenguni kukutana na wenzao na kujua hali zao na kupata nafasi ya kuomba maghfira na msamaha kwa madhambi yao katika mkutano mkubwa kabisa wa wanadamu ulimwenguni.
 
Unathibitishaje kuwa Qur'an imeshushwa ilihali waakina Abbakari waliiunganisha unganisha hatimaye tukapata kitabu kamili?
Unaweza kutoa ushahidi nje ya Qur'an kwamba ilishushwa?
 
Shukrani.
Nitakuuliza swali muda si muda.
Ngoja nitafakari haya uliyonipa.
 
Unathibitishaje kuwa Qur'an imeshushwa ilihali waakina Abbakari waliiunganisha unganisha hatimaye tukapata kitabu kamili?
Unaweza kutoa ushahidi nje ya Qur'an kwamba ilishushwa?
Ya kuambiwa changanya na yako, una uhakika uliyemsoma au aliyekuambia hayo ya "kuunga unga" kuwa alikwambia kweli?

Umeisoma Qur'an kwa kutaka kuelewa ina ujumbe upi? Ukiisoma Qur'an utaona kuwa yenyewe inasema kuwa imeshushwa kwa ajili ya watu wote, je, wewe haumo katika viumbe watu vya Mwenyezi Mungu? Soama:

Ujumbe wa Qur'an kwa Binadamu

Je, Qur'an ni muhimu kwa Waislamu tu? Vipi kuhusu ubinadamu.

Je, Qur'an ni kwa ajili ya Waislamu tu? Ikiwa Mwenyezi Mungu ni Mola wa walimwengu (Qur'ani 1:2) na Mtume (s.a.w.w.) anaelezewa kama mjumbe wa walimwengu (Quran 21:107) na Qur'an inatambulishwa kama ukumbusho kwa walimwengu, (Quran 68:52) basi ni nini umuhimu wa ujumbe wa Qur'ani kwa ulimwengu? Jinsi gani dunia, Waislam na wasio Waislam, sawa, wanaweza kufaidika na ujumbe wa ulimwengu wote wa Mungu wa ulimwengu wote na wenye huruma? Je, wasio Waislam wanaweza kufanya mazoezi ya maadili yaliyofunuliwa na Mungu bila kutambua chanzo chao cha asili na bila kufuata wito wa jumla wa Mungu?...

Itaendelea.
 
Quran imeshushwa kwa miaka 23 kidogo kidogo.
Maana yake ni kuwa kwa muda wa miaka 23 vilikuwa vinashushwa vipande vipande,
Maana yake kuna mtu alikaa akaunganisha ili kupata kitabu kimoja. Kwa hiyo mdau hapo juu yuko sawa aliposema kuna mtu aliunganisha.
Miaka 23 yote hiyo ina maana Mungu alikua anatoa ujumbe nusu nusu ilikuaje,alikua anasahau au ?
 
Hujajibu swali hapo Bibi angu!!!
 
Uarabu sio sawa na Uislamu, unajichanganya sana na unajaribu sana kuchanganya watu.
 
Umeisoma Qur'an?

jumbe wa Qur'an kwa Binadamu
Je, Qur'an ni muhimu kwa Waislamu tu? Vipi kuhusu ubinadamu.
Je, Qur'an ni kwa ajili ya Waislamu tu? Ikiwa Mwenyezi Mungu ni Mola wa walimwengu (Qur'ani 1:2) na Mtume (s.a.w.w.) anaelezewa kama mjumbe wa walimwengu (Quran 21:107) na Qur'an inatambulishwa kama ukumbusho kwa walimwengu, (Quran 68:52) basi ni nini umuhimu wa ujumbe wa Qur'ani kwa ulimwengu? Jinsi gani dunia, Waislam na wasio Waislam, sawa, wanaweza kufaidika na ujumbe wa ulimwengu wote wa Mungu wa ulimwengu wote na wenye huruma? Je, wasio Waislam wanaweza kufanya mazoezi ya maadili yaliyofunuliwa na Mungu bila kutambua chanzo chao cha asili na bila kufuata wito wa jumla wa Mungu?...
Itaendelea.
 
Kwa mtazamo wangu wa kawaida na wa kibinadamu.
Kule ni miongon mwa sehemu za kuchuma dhambi sasa namna zichumwavyo ndo sijajua ila ntafuatilia na ntakuja na mada hiyo one day.
Weng wakija wanakuja na majina mapya then wanakuja na uganga juu yake. Kiufupi wanaenda kama kumkiri shetaniii vlee maana kama unaenda then unarud ukiwa mganga naona linaweza kuwa jibu sahihi sana.
Wana wa adamu tunapotezwa sana tena sanaa tamaa na vitisho vya shetan ndivyo vinnatuharibia maisha ya ufalme wa mbinguni
 
Mtekwaji Ataongea ya Mtekaji. Ww kama Umetekwa na Waarabu utaongea ya Waarabu na Kama Umetekwa na Wamisionari Utaongea ya Wakoloni
Wewe umetekwa na nani? Au peke yako ndio hujatekwa, upo huru kushambulia waliotekwa?

Soma Qur'an, imekuja kwa ajili ya watu wote.
 
Mungu akubariki umeongea vizuri kabisa
 
Pole sana kwa kukalilishwa ujinga,usilolijua sawa na usiku wa Giza,Hiyo Hijja mwanzilishi wake ni Nabii Ibrahimu Waisilamu wanaendeleza tu,inawezekana Yesu naye angekuwa anauwezo wa kifedha naye angeenda kuhiji
 
Fact mkuu ila kwann weng wakirud wanakuwa nan tabia za dhambi ambazo mtoa post kasema?
 
Pole sana kwa kukalilishwa ujinga,usilolijua sawa na usiku wa Giza,Hiyo Hijja mwanzilishi wake ni Nabii Ibrahimu Waisilamu wanaendeleza tu,inawezekana Yesu naye angekuwa anauwezo wa kifedha naye angeenda kuhiji

Hivi suleiman nae alienda kuhiji mecca
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…