Je! kuna uhusiano wa akili (intelligence) ya mama na mtoto?

Je! kuna uhusiano wa akili (intelligence) ya mama na mtoto?

Kichwa Ndio Mtu

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2014
Posts
3,079
Reaction score
1,711
Habari.

Niwatakie mapumziko mema ya uhuru wa nchi yetu pendwa Tanganyika,

Turudi kwenye mada,nataka kujua kama kuna uhusiano wa akili (intelligence) mama na mtoto,yaani kama uwezo wa akili wa mama unaweza kua na madhara(effects/impacts) kwa mtoto atakae mzaa.

Kuna binti niko nae kama rafiki,uwezo wake wa darasani ulikua mdogo sana,akili ya darasani ni ndogo sana lakini ni mzuri sana kwa umbile na mwenendo/tabia..

Je anaweza akaja kuzaa watoto wenye akili ndogo darasani kama yeye au watakua tofauti?

Karibuni.
 
Uhusiano unaweza kuwepo na usiwepo.

Na si kwa mama tu, hata baba, babu, bibi, mjomba, shangazi na wengineo.

Mtu unaweza kurithi akili za babu yako kutoka vizazi kadhaa vilivyopita na unaweza kurithi moja kwa moja toka kwa wazazi.

Ni mambo yasiyotabirika kirahisi ingawa uwezekano wa kurithi kutoka kwa wazazi ni mkubwa zaidi kuliko wazazi wa vizazi vilivyopita.
 
Kisayansi ndio...
Japo watu wanaweza kupinga...
Unajua kuna wanawake wana akili lakini hawakuwa na access na shule...
Hivyo usiseme mimi nina akili lakini mama yangu si msomi...

Nilisoma article nyingi tu zina prove kuwa akili ya mtoto inatoka kwa mama...
 
Je ni haki kutumia matokeo ya darasani/shule kama njia pekee ya kujua intelijensia ya mtu?

Hapo inaweza kutumika kuelezea uelewa wa mtu sio craming capacity mana hiyo inatosha kumuelewa huyu mtu ana uwezo gani kuelewa hata mambo madogo hata kujielezea kawaida kwenye normal issues za maisha utaelewa tu kama ka shindwa kwenye vitu vidogo usitarajie vikubwa ataviweza
 
Hapo inaweza kutumika kuelezea uelewa wa mtu sio cramping capacity mana hiyo inatosha kumuelewa huyu mtu ana uwezo gani kuelewa hata mambo madogo hata kujielezea kawaida kwenye normal issues za maisha utaelewa tu kama ka shindwa kwenye vitu vidogo usitarajie vikubwa ataviweza

Hiyo nini maana yake?
 
ku kremu si kitu kibaya...kunaonyesha kuwa mtu ana good memory...
Mara nyingi watu huanza na ku kremu afu ndio wanakuja kwenye kuelewa...
 
Haina ubishi...kama darasani umeenda afu perfomance yako zero...ni ngumu kunishawishi eti una akili...
Hapa utetezi uwe kwa wale walionyimwa elimu kabisa tokana na ubaguzi kijinsia au umasikini...

umeona eeeh mtu kama mambo ya darasani yanampiga chenga huwezi kusema ana iq nzuri
na hata hao wasioenda shule kuna mambo flani flani lazima wanakuwa na utambuzi wa hali ya juu kuthibitisha iq zao
 
Back
Top Bottom