Mathias Raymond Nyakapala
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 2,181
- 1,493
Duh umenipa kazi nimeanza research rasmi nikimaliza ntakuja na majibu na mifano...
Sent using Jamii Forums mobile app
Wanabodi,
Hii ni thread ya swali
Jee Kuna Uhusiano Wowote Kati ya Dini na Majeshi?. Jee Kuna Watu wa Dini Fulani ni Wazuri Zaidi Jeshini Kuliko Dini Nyingine?.
Kufuatia Mkuu wetu wa Majeshi wa sasa kufanya kazi nzuri iliyotukuka Jeshini kuliko wakuu wengine wote waliotangulia, inawezekana huu uchapa kazi wake unatokana na kutoka kabila la wachapakazi?.
Katika kuwadurufu Wakuu wa Majeshi waliotangulia, kuna kitu strange nimekinote.
Wakuu hawa ni Jenerali Mirisho Sarakikya, Jenerali Abdalah Twalipo, Jenerali David Musuguri, Jenerali Ernest Mwita Kiaro, Jenerali Robert Mboma, Jenerali George Waitara, Jenerali Davis Mwamunyange, wa sasa Jenerali Venance Mabeyo.
Wote wana majina ya kiashiria ni watu wa dini fulani, isipokuwa mmoja tuu, Generali Abdalah Twalipo. Tena huyu Twalipo, mimi nilisoma darasa moja na binti yake akiitwa Flora Twalipo ambalo pia jina la kishiria cha dini fulani, usikute hilo jina la Abdalah ni jina tuu kama Anna Abdalah, au Jaji Ramadhani?.
Swali ni je kuna uwezekano watu wa dini fulani ni wakakamavu zaidi kuliko dini nyingine ndio maana wengi huko majeshini ni watu wa dini fulani?, kama jeshini tuna watu wa dini zote, inamaana wanao panda hadi kufikia top rank ya majenerali, kwa nini wengi wawe wa dini fulani hiyo hiyo?, kwani hao wa dini nyingine kwa nini hawawi majenerali?, jee wapo lakini hawana sifa za ujenerali au wapo na wanasifa lakini wanabaguliwa hivyo majenerali wengi kuwa watu wa dini moja?.
Jee ukakamavu nao una uhusiano na dini ya mtu?
.
Na tukija kwenye makabila, jee pia kuna makabila wachapakazi wanaoweza mitulinga ya Jeshini, na makabila mengine kazi za Jeshini ni kituo cha polisi?. Kwa nini watu wa makabila fulani fulani ndio wajae majeshini na kupata hadi kuwa majenerali?. Yaani Majenerali wote ni watu wa makabila ya bara tuu, yaani watu wa Pwani na visiwani hawawezi kupanda na kuwa majenerali?.
Nauliza hivi makusudi ili baadae huko mbele ya safari, tusije kulaumiana, kati ya majenerali wote 8 wa jeshi letu, tangu tumepata uhuru, majerali watutu, sio tuu walitoka mkoa mmoja, bali ni watu wa kabila moja, sasa kuna unaya wowote, na mimi nikibahatika kuwa CinC wa majeshi yetu, nami nikatafuta angalau generali wa kabila langu, hata kama rank yake ilikuwa chini, nikamuongezea muda kidogo wa kustaafu jenerali aliyepo ambaye muda wake umekwisha, kisha nikampandisha vyeo chap chap jererali wa kabila langu, lakini kufuatia good track record ya utekelezaji wake wa mambo makubwa, ikaamuliwa kuanzia sasa, majerali wawe kutoka kabila fulani angalau hata watatu kama lile kabila jingine, wakati huo tukifanya affirmative action jeshini kwa kuwapandisha vyeo chap chap watu wa dini nyine ambao hawajapata majenerali, na kuwajaribisha watu wa makabila mengine kwenye vyeo vya juu, ili Jeshi letu la Wananchi wa Tanzania, liwe ni jeshi la wote kuweza kuwa majenerali?.
Nawatakia Jumapili njema ya matawi.
P
Sent using Jamii Forums mobile app