Hellow!
Kuna agizo kabisa Kutoka Kwa Mungu kupitia vinywa vya manabii na vitabu vya kiimani kuwa tunapaswa kuzitii mamlaka, Kwa kuwa mamlaka hizo zimeruhusiwa na Mungu.
Sasa matukio yafuatayo na simulizi ndani ya vitabu vyetu kiimani, zinanipa maswali kuwa, Inawezekana upo ukomo katika kuzitii mamlaka za WANADAMU.
Twende pamoja kupitia matukio haya.
1. Baada ya Wana wa Israel kuongezeka sana nchini mirsri, Pharao anapitisha amri kuwa, muisrael akizaa mtoto wa kiume, mtoto huyo auwawe, yaani mzazi amuue mtoto wake Kwa mikono yake mwenyewe, utii wa mamlaka umekaaje hapo,
Na ikiwa wazazi wa Musa wangetii mamlaka kama ilivyo, Musa angewezaje kuwakomboa Wana wa Israel?
2. Nchi ya Israel inazingirwa na maadui washami, inapitishwa amri malango ya nchi yafungwe, hakuna kuingia Wala Kutoka, wakoma wanne wanakosa chakula sababu watu wamejifungia, wanaamua kuvunja utii wa mamlaka na Kutoka nje ya mipaka ya nchi kutafuta chakula, Mungu anawatumia kuikomboa Nchi Yao. Je utii wa mamlaka uko vipi hapo?
3. Herode anapata habari kuwa king Jesus amezaliwa Bethlehemu, Herode anaamuru watoto wote wa kiume under 5 year wauwawe, Malaika anamtokea Yusuf na kumwambia akimbilie Misri kumwokoa mtoto asiuwawe, wangetii mamlaka, Ukombozi wa WANADAMU ungekuwaje,Je utii wa mamlaka umekaaje hapo?
4. Petro na Paul na wanafunzi wengine wa Yesu wanazuiwa na Amri iliyowekwa na mamlaka kwamba ni marufuku kuhubiri na kulitaja Jina la YESU, Paul na wenzie wanaapa kamwe kutotii Amri hiyo wakidai kuwa Nao wameamrishwa na Mungu wao kuhubiri hivyo hawaezi kutotii Amri ya Mungu Kwa kutii amri ya WANADAMU, utii wa mamlaka za WANADAMU ukoje hapo?
5. Kuna wafanyakazi wanaolipwa kulinda Amani na kusimamia haki, hao hao wanashiriki kubambikia watu kesi za uongo, wakishiriki kuingiza kura fake kwenye Sanduku la kura, Nchi inaingia katika ombwe la uongozi, Kisha matendo maovu yanatamakaki, je upo ukomo kutii mamlaka za aina hii?
Swali: Ni Kwa kiwango Gani ,Kuna ukomo wa kutii mamlaka?
Karibuni 🙏