Je, kuna ukweli kuwa mtu anaweza kumbadilisha mtu mzima?

Je, kuna ukweli kuwa mtu anaweza kumbadilisha mtu mzima?

Blue G umemissika, uko poa mumie?
Tabia ya mtu ina asili mbili
-Kuzaliwa
-Kujifunza
Kuzaliwa ni ile tu uko ulivyo ndo umezaliwa hivyo na ndo Mungu alitaka uwe hivyo.
Kujifunza kunatokana na mengin, mazingira, uchumi, mapenzi, taaluma, kazi, na mengine ya aina hiyo!

Kuhusu mtu kumbadilisha mwingine hasa kwenye mapenzi nawezekana iwapo tu huyo mtu anataka kubadilika!
mf:Mtu una tabia ambayo kila siku inafanya mnakuwa na ugomvi na mhusika, hii inaweza kuwabadilisha hata ile Amani mliyo nayo!
Very likely utataka kuondoa hiyo hali, as unampenda huyo mtu na hutaki kumkwaza na kufanya wewe uwe chanzo cha ukorofi!
Mostlikely utabadilika!
Ila kinyume na hapo,!
Subutuuuuuuuuuuuuuuuuuu!
Nipo poa mamie sijui wewe snowhite ,mi nipo tu my dear sema vijimambo tu vya hapa na pale vinanifanya napotea na kuibuka kama hivi humu JF

asante sana kwa ufafanuzi mzuri my dear,sina nyongeza kwa kweli

ila hapo mwisho nilipobold umenicehekesha kwa kweli sio kwa msisitizo huo hahahahahahahahaha
 
nope

mkuu kila mwa MMU hii mada inamhusu

basi u niliwamiss hao wahenga wenzangu nikaamua kuwamention

karibu ufunguke mkuu mchango wako muhimu sana,ushawahi kubadilishwa au kumbadilisha mtu mkuu? uliwahi kufikiria?uliwahi kushindwa? uliwahi kukabili changamoto zipi kama uliwahi?
Mimi naamini unaweza kubadilishwa(Baadhi ya vitu) na mtu iwapo tu huyo mtu ana nafasi kubwa kwenye maisha yako...mfano rafiki wa karibu,mke n.k
 
Kwenye mahusiano inawezekana haswa mwenza wako akiwa anakufeel na kukuheshimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
asante kwa jibu lako my dear yna2 sasa mamie kwa wale ambao wameshindwa kubadilika hata ndani ya mapenzi mazito ni nini huwa kinatokea? umewahi kumbadilisha mtu au kumfanya abadilike au wewe kubadilishwa na mtu?
 
Mimi naamini unaweza kubadilishwa(Baadhi ya vitu) na mtu iwapo tu huyo mtu ana nafasi kubwa kwenye maisha yako...mfano rafiki wa karibu,mke n.k
ah okay sawa sawa mkuu Darmian asante kwa kushare hilo na sisi,lakini nina maswali kwako,umeweka kwenye mabano baadhi ya vitu,unaweza kutuambia ni vitu gani hivyo mkuu? umeshawahi kutaka kumbadilisha mtu na ukafanikiwa katika hilo,umeshawahi kuwa na mtu anayetaka kukubadilisha? umewahi kuona kwa mtu yeyote Rafiki,jirani au ndugu ambaye amewahi kufaulu kumbadilisha mtu?
 
nmewahi kubadilishwa, Nikawa navaa nikabu mpaka tulipoachana , imenifanya watu wengi wadhani mimi ni muslim,maana sometimes navaa sana majuba
Ila wanaume hawabadilikagi kirahisi na sijawahi kutaka kumbadilisha mtoto wa mtu.. Let asshole be asshole you will sleep better.
Pole sana inamaana hadi leo bado upo Single
 
asante kwa mchango wako mujarabu kabisa mkuu Mzimu wa Kolelo,kwa hiyo wewe mwenzetu unakubali kuwa inawezekana kumbadilisha mtu ila ni baada ya muda mrefu na kwa hatua ndogo ndogo,hivyo unaweza kukubali kuingia katika ndoa na mtu unayeona kabisa ana shida Fulani ambazo wewe binafsi huoendezwi naye ukiamini hatua kwa hatua na baada ya muda unaweza kumbadilisha mwenzi huyo?

inategemea na tabia gani ndoa haimbadilishi mtu isipokuwa inatakikana kujiuliza huyo unaetaka muoa umemlaghai sana ili umuoe
kwa mana ya kwamba umeonesha jinsi gani unampenda unamjalli ili tu akubali umuoe
au umetumia pesa kumshawishi sana kumuonesha unataka kuingia nae katika ndoa
ama lah umempanga sana kwa maneno matamu kuonesha jinsi gani unavyotaka kuanza nae safari ya maisha na mipango kedekede ya maendelo mpk akavutiwa kuingia katika ndoa na wewe
kama jibu ndiyo katika hayo au yanayofanana na hayo ikitokea ikaenda sivyo ndivyo na ulivyomuahidi ni ngumu kumbadilsha hvyo itakuwa si ndoa bali ni ndoano 7bu utakuwa unaishi na mtu ambaye hukubakiani na tabia zake inamaana upendo hutapungua chuki zitaanza hisia za mapenzi zitapotea tendo la ndoa halitakuwa na thamani utampanda kutimiza wajibu utatafuta mchepuko migogolo itaanza mahusiano yatavunjika km mtakuwa mmezaa itabaki kulea watoto mwisho mnaweza achana kabisa

lkn km huyo mtu wako km ni yeye ndo amehamasika na ndoa yaan kuna mambo mengi sana amefanya au kukufanyia ama kuonesha anataka NDOA na wewe mpk na wewe ukatamani kumuoa lkn kuna tabia chache zinakutatiza kuingia nae ndoani Advantage ya kumbadilisha ipo kwa kiasi kikubwa ikiwa utang'amua kipi au jambo gani hasa limempelekea mpk yeye kuitaka ndoa kwa sasa au na wewe
mathalani umri labda ama kuhitaji mtoto ama kutaka kujenga maisha ya kifamilia au tu kuonekana naye ameolewa kutokana na maneno ya marafiki ndugu na jamaa au amechoka maisha anayoisha ya kutangatanga eidha kuchumi yupo hovyo.

ama kimapenzi km kutopata mtu sahihi na anataka mtu wa kutulia
sasa km utakuwa umemuelewa na ukampa hitaji lake ni rahisi kumbadilisha na inawezekana kumbuka tu kufuata prosija na inapendeza kuwa katika mahusiano kwanza kabla ya ndoa lkn yale mahusiano ambayo kuangalia je itawezekana haya hvyo ni vema kumtambua na kujaribu kumpa hitaji lake katika nia ya kutaka kufikia malengo yake au yenu kwa ujumla ili kurahisisha hilo jambo la kumfanya kuwa na tabia bora na nzuri ikakupendeza
 
Pole sana inamaana hadi leo bado upo Single
hahahahahahahaha mkuu swali lako banah

haya tunaomba experience yako kama ushawahi kukutana na hili au kuliona mahali
 
hahahahahahahaha mkuu swali lako banah

haya tunaomba experience yako kama ushawahi kukutana na hili au kuliona mahali
Mie bado sijawahi kukutana nalo hilo jambo
 
inategemea na tabia gani ndoa haimbadilishi mtu isipokuwa inatakikana kujiuliza huyo unaetaka muoa umemlaghai sana ili umuoe
kwa mana ya kwamba umeonesha jinsi gani unampenda unamjalli ili tu akubali umuoe
au umetumia pesa kumshawishi sana kumuonesha unataka kuingia nae katika ndoa
ama lah umempanga sana kwa maneno matamu kuonesha jinsi gani unavyotaka kuanza nae safari ya maisha na mipango kedekede ya maendelo mpk akavutiwa kuingia katika ndoa na wewe
kama jibu ndiyo katika hayo au yanayofanana na hayo ikitokea ikaenda sivyo ndivyo na ulivyomuahidi ni ngumu kumbadilsha hvyo itakuwa si ndoa bali ni ndoano 7bu utakuwa unaishi na mtu ambaye hukubakiani na tabia zake inamaana upendo hutapungua chuki zitaanza hisia za mapenzi zitapotea tendo la ndoa halitakuwa na thamani utampanda kutimiza wajibu utatafuta mchepuko migogolo itaanza mahusiano yatavunjika km mtakuwa mmezaa itabaki kulea watoto mwisho mnaweza achana kabisa

lkn km huyo mtu wako km ni yeye ndo amehamasika na ndoa yaan kuna mambo mengi sana amefanya au kukufanyia ama kuonesha anataka NDOA na wewe mpk na wewe ukatamani kumuoa lkn kuna tabia chache zinakutatiza kuingia nae ndoani Advantage ya kumbadilisha ipo kwa kiasi kikubwa ikiwa utang'amua kipi au jambo gani hasa limempelekea mpk yeye kuitaka ndoa kwa sasa au na wewe
mathalani umri labda ama kuhitaji mtoto ama kutaka kujenga maisha ya kifamilia au tu kuonekana naye ameolewa kutokana na maneno ya marafiki ndugu na jamaa au amechoka maisha anayoisha ya kutangatanga eidha kuchumi yupo hovyo
ama kimapenzi km kutopata mtu sahihi na anataka mtu wa kutulia
sasa km utakuwa umemuelewa na ukampa hitaji lake ni rahisi kumbadilisha na inawezekana kumbuka tu kufuata prosija na inapendeza kuwa katika mahusiano kwanza kabla ya ndoa lkn yale mahusiano ambayo kuangalia je itawezekana haya hvyo ni vema kumtambua na kujaribu kumpa hitaji lake katika nia ya kutaka kufikia malengo yake au yenu kwa ujumla ili kurahisisha hilo jambo la kumfanya kuwa na tabia bora na nzuri ikakupendeza

Sent using Jamii Forums mobile app
asante mkuu lakini itakuwaje ikiwa mtu huyu atapata hitaji lake unadhani ataendelea na tabia ile uliyombadilisha nayo,say alitaka watoto kawapata,say alitaka aondoe gundu just kwa kulivaa shela,kalivaa unadhani ataendelea kuwa aliyebadilika?
 
Tabia ya kuzaliwa nayo(inborn) sio rahisi kumbadilisha mtu ila tabia ambayo mtu anakuwa nayo kutokana na mazingira(acquired) unaweza kumbadilisha mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
asante kwa ufafanuzi yakinifu mkuu swahiba92 umeeleza vizuri sana mkuu

japo nimekuwa nikifikiria kitu kama chako ila kitofauti kidogo,sikuzote nimekuwa nikiamini tabia zipo za aina kama nne hivi(naomba nisahihishwe nitakapokosea),zipo zile za kurithi,zipo zile ambazo mtu mwenyewe ndivyo alivyo ndani yake yaani make up ya mtu huyo labda ukarimu,uongozi n.k zipo zile zinazoathiriwa na malezi ya mtu na zile ambazo zinaathiriwa na jamii iliyomzunguka mtu

sasa katika hizi nne mbili zinaweza kubadilika kwa sababu ni external yaani zile za malezi na jamii iliyomzunguka lakini za kurithi na namna mtu alivyo mara nyingi sio rahisi kabisa kubadilika labda Mungu aingilie kati kama ulivyosema hapo juu,

sasa mkuu kutokana na mifano kadhaa mabyo mimi nimejione mtu kushindwa kubadilika na kuacha tabia kama vile ulevi,umalaya,uchonganishi n.k,tusema tabia hizi kulingana na ufafanuzi wako zinafall kwenye hulka au tabia?

plus bila kusahau wewe binafsi kutupa experience yako ya hii kitu mkuu,kama ulishawahi kukabiliana na changamoto ya kumbadilisha mtu au mtu kutaka kukubadilisha au ulichokishuhudia kwa jirani Rafiki au ndugu
MIMI nina mtazamo tofautu kidogo naamini hakuna tabia za kurithi bari kile mtoto anachojifunza tangu anazaliwa
mfn mtoto tangu akiwa tumboni katika wiki ya 32 anaanza kusikia km nyimbo zinazoimbwa radion mnavyoongea inamaana hadi siku anazaliwa tayari kuna sauti anakuwa amezizoea baada ya sauti sasa unafatia harufu 7bu bado hajaanza ona ndo mana mtoto ukimshika wew analia lkn akipewa mamaake akisikia ile harufu ya ziwa anapoa akishaaza kuona anaanza mazoea sasa kwa wazazi na watu wa karibu kisha mazingira ya nyumbani baadae kabisa akiweza toka mwenyewe kwenda nyumba ya jirani anaanza kujifunza ya dunia sasa
hvyo binadamu kadili anavyokua anayojifunza na kukumbana nayo ndo yanambadilsha katika kila lika analopitia na jinsi mnavyomchukulia au jamii inavyomchukulia ndivyo huakisi tabia yake
mfn mtoto inafika hatua ananijua kabisa sisi kwetu hoehae au mm yatima sina wazazi naishi kwa mjomba hvyo mara nyingi tabia huendana na mazingira
ndo mana unaweza kuta tabia ya mtoto fulani nzuri sana mkalimu nk 7bu anajijua yeye yatima na km unavyojua YATIMA HADEKI
akapitia manyanyaso yakambadilisha
lkn utakuta toto wale kina JUNIOR hovyo kabisa kutokana na linavyolelewa

hvyo athari za kitabia au hizo hulka zinatokana hatua za ukuaji anazopitia mtoto sio kusema kurithi au yeye alivyo bali ni vile tu maisha anayokumbana nayo
mfn mama malaya abaushi na mtoto wa kike na kila siku mauncle wapya hata yeye akikua anaona kawaida kubadili wanaume
au baba mlevi anapiga mama mtoto anaona naye akikua nae anaona kawaida
lkn baba mlevi anapiga mama lkn mtoto anaishi kwa bibi na babu ambao watu wa dini maadili mema sasa ataanzaje kuwa mlevi eti amrithi babayake na hakuna mazingira ya ushawushi hivyo
wakurya ni majasili kutokana na makuzi yao lkn mtoto mkurya akazaliwa nzanzibar akajulia nzanzibar lazima atakuwa na tabia za wanzanzibari hata lafudhi itabadilika pia

mm bwana kulikuwa na rafiki ingawa si wa karibu tulisoma wote msingi kwa kweli alikuwa mpole mkarimu na alikuwa yuko vizuri kichwani kupita viwango kiasi hadi walimu walikuwa wanampenda tulipoteana miaka mingi siku nakuja kutana nae mkoani ni deleva malori aisee kwa mademu sijapata ona na anapenda kubet kinoma yaan hvyo ni mambo tu ambayo maisha yanaambadilisha mtu
hvyo hakuna kinachoshindikana ikiwa huyo mtu mwenyewe mpo katika mazingira gani kwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tabia ya kuzaliwa nayo(inborn) sio rahisi kumbadilisha mtu ila tabia ambayo mtu anakuwa nayo kutokana na mazingira(acquired) unaweza kumbadilisha mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu sawima asante kwa jibu lako,lakini unaongeleaje kuhusu wale ambao wameshindwa kubadilishwa tabia kama vile ulevi?tuseme ulevi unaweza ukawa ni inborn character?
 
asante mkuu lakini itakuwaje ikiwa mtu huyu atapata hitaji lake unadhani ataendelea na tabia ile uliyombadilisha nayo,say alitaka watoto kawapata,say alitaka aondoe gundu just kwa kulivaa shela,kalivaa unadhani ataendelea kuwa aliyebadilika?
ha ha ha mkuu maisha umbadilisha mtu

katika NDOA ukiupita mwaka wa kwaza wa matatizo na vikwazo mkaushinda mwaka wa tatu wakuchokana na kuzoeana mkapiga mwaka wa tano mnavumilia 7bu mnalea tu watoto bila hvyo mngeachana
mkishaingia mwaka wa 7 basi hapo mnakuwa mwili mmoja ata mkigombana hauishi mwenzi mnarudiana na hata mkiachana kabisa hakuna atakatepata mbadala wa mwenzie mtatafutana tu au mawazo juu ya mwezie hataushi kichwani
hvyo mkuu ndoa sio FURAHA km wengi wanavyoamini ukioa au kuolewa wewe ni kuserebuka tuu
NDOA ni maisha km unavyoishi wewe huvi hapo sasa hvi hizo changamoto unazokumbana nazo katika maisha yako na unapigana nazo ndio NDOA ipo hivyo mkuu hvyo mengne inabidi ufumbe macho upambane nayo ukubaliane nayo
7bu huyo mwenye tabia unazotaka hakuvutii hata na humpendi
lkn huyo mwenye tabia za hovyo ndo yupo moyoni mwako na unampenda hasa
katika VITABU VITAKATIFU vinasema OENI katika mnaowapenda
na mm nakazia OA mkuu unayempenda 7bu utamvumilia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nmewahi kubadilishwa, Nikawa navaa nikabu mpaka tulipoachana , imenifanya watu wengi wadhani mimi ni muslim,maana sometimes navaa sana majuba
Ila wanaume hawabadilikagi kirahisi na sijawahi kutaka kumbadilisha mtoto wa mtu.. Let asshole be asshole you will sleep better.
hukubadilishwa bali ulibadilika wewe mwenyewe bcz u were in love, and u wanted to make him happy, women do a lot of stupid things when they r in love tofauti na wanaume
 
mkuu sawima asante kwa jibu lako,lakini unaongeleaje kuhusu wale ambao wameshindwa kubadilishwa tabia kama vile ulevi?tuseme ulevi unaweza ukawa ni inborn character?
Kubadilisha addiction ni kazi ngumu sana mtu akishakuwa addicted kumtoa huko kunahitaji nguvu za ziada au aamue mwenyewe baada ya kumkuta ya kumkuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dah mamie najaribu kufikiria kilichombadilisha hapo nakosa majibu mujarabu,ni mapenzi yake kwako au aliona tu mabadiliko ambayo wewe unayataka yanamletea na yeye manufaa au ni nini?
Alinipenda sana ndo sababu nahisi
 
Back
Top Bottom