MIMI nina mtazamo tofautu kidogo naamini hakuna tabia za kurithi bari kile mtoto anachojifunza tangu anazaliwa
mfn mtoto tangu akiwa tumboni katika wiki ya 32 anaanza kusikia km nyimbo zinazoimbwa radion mnavyoongea inamaana hadi siku anazaliwa tayari kuna sauti anakuwa amezizoea baada ya sauti sasa unafatia harufu 7bu bado hajaanza ona ndo mana mtoto ukimshika wew analia lkn akipewa mamaake akisikia ile harufu ya ziwa anapoa akishaaza kuona anaanza mazoea sasa kwa wazazi na watu wa karibu kisha mazingira ya nyumbani baadae kabisa akiweza toka mwenyewe kwenda nyumba ya jirani anaanza kujifunza ya dunia sasa
hvyo binadamu kadili anavyokua anayojifunza na kukumbana nayo ndo yanambadilsha katika kila lika analopitia na jinsi mnavyomchukulia au jamii inavyomchukulia ndivyo huakisi tabia yake
mfn mtoto inafika hatua ananijua kabisa sisi kwetu hoehae au mm yatima sina wazazi naishi kwa mjomba hvyo mara nyingi tabia huendana na mazingira
ndo mana unaweza kuta tabia ya mtoto fulani nzuri sana mkalimu nk 7bu anajijua yeye yatima na km unavyojua YATIMA HADEKI
akapitia manyanyaso yakambadilisha
lkn utakuta toto wale kina JUNIOR hovyo kabisa kutokana na linavyolelewa
hvyo athari za kitabia au hizo hulka zinatokana hatua za ukuaji anazopitia mtoto sio kusema kurithi au yeye alivyo bali ni vile tu maisha anayokumbana nayo
mfn mama malaya abaushi na mtoto wa kike na kila siku mauncle wapya hata yeye akikua anaona kawaida kubadili wanaume
au baba mlevi anapiga mama mtoto anaona naye akikua nae anaona kawaida
lkn baba mlevi anapiga mama lkn mtoto anaishi kwa bibi na babu ambao watu wa dini maadili mema sasa ataanzaje kuwa mlevi eti amrithi babayake na hakuna mazingira ya ushawushi hivyo
wakurya ni majasili kutokana na makuzi yao lkn mtoto mkurya akazaliwa nzanzibar akajulia nzanzibar lazima atakuwa na tabia za wanzanzibari hata lafudhi itabadilika pia
mm bwana kulikuwa na rafiki ingawa si wa karibu tulisoma wote msingi kwa kweli alikuwa mpole mkarimu na alikuwa yuko vizuri kichwani kupita viwango kiasi hadi walimu walikuwa wanampenda tulipoteana miaka mingi siku nakuja kutana nae mkoani ni deleva malori aisee kwa mademu sijapata ona na anapenda kubet kinoma yaan hvyo ni mambo tu ambayo maisha yanaambadilisha mtu
hvyo hakuna kinachoshindikana ikiwa huyo mtu mwenyewe mpo katika mazingira gani kwa sasa
Sent using
Jamii Forums mobile app