Je, Kuna ulazima mwanamke abadili jina baada ya kuolewa?



Kasome/soma Isaya 4:1 na kuendelea utapata huo utabiri.
 
Kasome/soma Isaya 4:1 na kuendelea utapata huo utabiri.
asante sana bwana Malila, ni kweli isaya 4:1 inasomeka hivi
"Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema,Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, LAKINI TUITWE TU KWA JINA LAKO; utuondolee aibu yetu"
nadhani sasa ndio tupo kwenye hiyo stage kwa maana wanawake wengi wana uwezo wao wa kujikimu na kujitunza , tatizo kubwa walilonalo ni mambo ya ndo kuitwa MRS
 

Usione mdada/mmama kapiga buku na mihela juu halafu anakwenda kuegesha kwa mtu mwenye mke na familia yake,tayari ilisha andikwa hiyo. Mtu kung`ang`ania surname ya mtu saa nyingine humpa heshima fulani mbele ya jamii kwamba yeye sio NUNGAYEMBE fulani hivi,ila yuko single kwa ajali ya ndoa/mapenzi and alike.
 
Mimi ninaona kutumia surname ya mwanaume ni aina ya unyonge ambayo wanawake wanayo, inabidi wanawake wajitoe kwenye unyonge huo.
Haiwezekani mwanaharakati wa masuala ya akina mama aliyesimama kidete kupinga mfumo dume ilhali yeye mwenyewe anaitwa Mrs. Juma, wanawake watajikomboa kweli?
 

mwanamke aliumbwa kwa sababu ya mwanaume na si mwanaume kwa sababu ya mwanamke na hiyo hata kama hautafata misingi ya kidini ni hiko hivyo tu, hata ukienda kwenye maeneo ambayo hakuna dini kabisa wanafata system hiyohiyo ambayo ni nature
 
mwanamke aliumbwa kwa sababu ya mwanaume na si mwanaume kwa sababu ya mwanamke na hiyo hata kama hautafata misingi ya kidini ni hiko hivyo tu, hata ukienda kwenye maeneo ambayo hakuna dini kabisa wanafata system hiyohiyo ambayo ni nature


Hey wake-up sasa hivi ni asubuhi mbona wewe bado umelala? Au kausingizi bado ni katamu na ndoto zako hazijakwisha?
 
uIslam raha sana, hakuna kutumia jina la mume. Mke na lake na mume na lake. waIslam wanaotumia majina ya waUme zao wanapo-olewa waelimishwe kuwa hayo si maadili ya kiIslam, waachane nayo kabisa, ni kujidhalilisha.
 
...Ni lazima mke akishaolewa kutumia jina ukoo la mumewe? ...vipi huyo mke akiendelea kutumia jina hilo hata baada ya kuachika? ...mume ana mamlaka ya kumnyang'anya mtaliki wake "hatimiliki" ya kuendelea kutumia jina la ukoo (wa mume)?

Mbu,

very interesting topic umeleta.

Kwanza kabisa sio lazima abadili jina to my name.
Lakini if she did na tukichana, inabidi unirudishie
jina langu usije ukaniharibia 'CV' huko mbele.

regards.
 
Huu mjadala umekuwa mrefu ila ni mzuri ningependa kuchangia......

inawezekana ni mtazamo wangu ila nilikuwa naamini kuwa kwa mwanamke kubadili jina akishaolewa ni ishara kuwa anakupenda na amekukubali wewe uwe kiongozi wa familia yake (kama ambavyo alikubali baba yake mzazi kuwa kiongozi wake kabla hajaolewa). ingawaje ni kitu cha kurithi lakini maana yake huwa inabadilika kizazi kwa kizazi.

Hivyo basi mwanamke wa leo akibadili jina na kumfuata mumewe kwangu mie nalichukulia kama ishara ya upendo na kamwe si utumwa au kujidhalilisha kama tu ilivyo kwa mke kumfulia mume underwear (si kwa kuwa ni kazi yake kama mke bali anaweza amua kufua au kuacha isipokuwa kama anampenda sana mumewe na hapendi kumwona akiteseka kufua)

Nawakilisha
 
Anaesema ni ishara ya utumwa muongo kwani hata sheria zote zinatambua hivyo au unataka niambia kuna Mr Opra hapa? maana hata internationally mie nikitumia passport yenye jina la maiden then certificate au vyeti vingine ni Mrs inakubalika kabisa. Pili kama kuna huo usawa vipi watoto waitwe jina la nani??? Kuna kinamama ambao wanawaita watoto majina yao ila sifahamu kwenye birth certificate wameandikwa nini?
Kwako Mwanajamii1 kufua underwear, ni sawa tu kwani mie nae niona wezi wamekuja nina amani kabisa najua hiyo ni role ya Mr: ni mgawanyo tu wamajukumu nikiwa pregnant hata yeye anaweza kufua. Kikubwa ni upendo, maadili na utii ndani ya nyumba=amani
 
...Hivyo basi mwanamke wa leo akibadili jina na kumfuata mumewe kwangu mie nalichukulia kama ishara ya upendo na kamwe si utumwa...

....Sasa iweje Mwanamke akiachika au hata akishaolewa na Mume mwingine bado anang'ang'ania kutumia Surname ya ex -wake?

Na mifano ya karibu, lakini katika ku protect anonymity ya 'mbu' katika uenezi wa malaria, sitotaja majina πŸ˜€

...kwa celebrities, kuna kina Tina Turner, Graca Machel, Winnie Madikizela -Mandela...
 

. Ni kweli inashangaza lakini nafikiri pia suala la usumbufu na mazoea linaweza kuchangia. Kunakuwa na previledges ambazo mtu alikuwa akizipata wakati ule na asingependa kuzikosa so anabakia na jina ila kuna wale wengine ambao kusema kweli huwa hawajali wala hawajui kama ina athari.

Sipati picha ningekuwa mie lol siku ya kurudisha makabrasha yake namrudishia na jina lake labda kama kaniacha wakati bado nampenda............. mbona atakoma!
 
....Sipati picha ningekuwa mie lol siku ya kurudisha makabrasha yake namrudishia na jina lake labda kama kaniacha wakati bado nampenda............. mbona atakoma!

...dah! ...yaani hivyo ulivyoandika tu hapo mimi tayari 'nimeshakoma!' πŸ˜€
 
Hapa tunaongelea patrimonial tu lakini kumbukeni pia matrimonial
 
sio kila wanachofanya wazungu na wamarekani ni sahihi,wakinadada tumieni majina yenu

jamaa mmoja baada ya kuasiana na mkewe alienda kumfanyia fujo ofisini asitumie tena jina lake ,eti anmzibia bahati yake ,wabeijing mpo,
si rahisi babako kukwambia usitumie jinalake ukimuudhi
 
kubadilisha au kutokubadilisha kunategemeana na maslahi

kwa hiyo wanawake wengi siku hizi wanaangalia kama majina ya baba zao yana mafao kuliko ya waume zao....

kama jina la baba yako ni kubwa unakuta wanawake wengi halibadilishi...
lakini kama wewe steved jina lako ni kubwa basi huyo binti atabadilisha tu mwenyewe..
msalimie...
 
Mambo ya kubadili jina sio muhimu tena kama zamani, Kuna nchi zingine , mwanamke hauruhusiwi kubadili jina anapoolewa.
 
Forget about kuchukua jina.

Mwanamke kuolewa kumepitwa na wakati.

Kwa nini aolewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…