Je, kuna umuhimu kama taifa kufanya usaili kwa kada ya Afya na Ualimu ndo Uajiri?

Je, kuna umuhimu kama taifa kufanya usaili kwa kada ya Afya na Ualimu ndo Uajiri?

Gwamanga

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2021
Posts
223
Reaction score
434
Leta hoja yako, ijikite kwenye
1.Kwanini miaka mingi kada hizi hazikuwa na usaili isipokuwa sasa.
2. changamoto kiujumla za Mchakato wa usaili kwa kada hizi
3. Faida ya kufanya na kutofanya usaili
4.Bajeti za wizara kutekeleza usaili.
5.Hitimisho.
Usaili ni mchakato au utaratibu wa kuuliza na kujibu maswali ili kupata taarifa au kuchunguza sifa, ujuzi, au uwezo wa mtu fulani. Usaili hutumika mara nyingi katika ajira, ambapo mwajiri anawahoji waombaji wa kazi ili kubaini kama wanafaa kwa nafasi fulani. Pia, usaili unaweza kufanywa kwa madhumuni mengine kama vile utafiti au kutafuta habari.

Zama zimebadilika muajiri anahitaji efficient individuals , si cheti au ufaulu mkubwa maana hivyo haviendi kufanya kazi, but efficiency ya mtu
 
Usaili wa siku moja unatosha kumpima mtu kuliko vyeti yake vya kitaaluma? kumbuka katoka form4, six, cheti au diploma, degree, je dk 30 za usahili zinatosha kweli kumpima mtu huyo??
 
Kwa sasa waombaji ni wengi mno sasa kwenye ushindani kama huo kila mtu anataka hizo ajira usaili ndio namna pekee ya kuweka usawa wa kupata nafasi kutokana na majibu ya usaili wenye score nzuri za usaili watapata ajia ila kama nafasi za ajira ni 50 na waombaji ni 10 hapo hakuna maana yeyote ya usaili.
 
Leta hoja yako, ijikite kwenye

1. Kwanini miaka mingi kada hizi hazikuwa na usaili isipokuwa sasa.
2. changamoto kiujumla za Mchakato wa usaili kwa kada hizi
3. Faida ya kufanya na kutofanya usaili
4. Bajeti za wizara kutekeleza usaili.
5. Hitimisho.

Soma Pia: Kada ya Ualimu na Afya wafanyiwe usaili wakati kaujiriwa kama ilivyo kada zingine
Ahsante Sana Kwa mjadala huu mzuri.

Kwa serikali muajiri mara nyingi haonekani, ambae wengi humchukulia ni Mh Raisi au waziri husika wakati huo. Kufanyiwa USAILI na kuajiriwa serikalini hakuna maana kabisa maana baada ya ajira hakuna anaekuja au kutambua uwezo wako huko utakapo pangiwa kazi.
 
Leta hoja yako, ijikite kwenye

1. Kwanini miaka mingi kada hizi hazikuwa na usaili isipokuwa sasa.
2. changamoto kiujumla za Mchakato wa usaili kwa kada hizi
3. Faida ya kufanya na kutofanya usaili
4. Bajeti za wizara kutekeleza usaili.
5. Hitimisho.

Soma Pia: Kada ya Ualimu na Afya wafanyiwe usaili wakati kaujiriwa kama ilivyo kada zingine
Waajirwa wa afya Kuna bodi zetu husika Kama pharmacy council, Kila mwanataaluma ana leseni yake ya kazi, Kila mwaka anailipia na pia hufanya CME/CPD Ili kushikilia leseni yake. Hivyo yoyote mwenye leseni hai ni mwanataaluma mwenye ujuzi na Yuko vizuri.

Kifanya mtihani ni upotevu wa muda na pesa ya taifa
 
Usaili wa siku moja unatosha kumpima mtu kuliko vyeti yake vya kitaaluma? kumbuka katoka form4, six, cheti au diploma, degree, je dk 30 za usahili zinatosha kweli kumpima mtu huyo??
Vyeti vya kitaaluma its easy kupata, but utendaji is rare, is why saili zinaouwa kwneye hatua ratu au zaidi.
Sioni haja kwanini saili ziondolewe
 
Ni upumbavu tu na usumbufu

Mtu amehitimu anavyeti, mmempima mkampa na leseni tena usahili wa nn kama mnahisi hana sifa leseni ya nini mlimpa?

Ujinga ni mzigo nchi hii
Yale yale yampka uwe wakili upite SHOOL OF LAW hii nchi ujuaji mwingi ili tu kuwakwamisha wasio na misuli.
 
Kila waziri na sera zake, kuna haja kma Taifa kuwa na Ramani 1 inayotuongoza, cheki issue ya michepuo waliyoyafanya. hopeless zero preparations.
 
Utumishi shikilieni hapo hapo, hakuna kada kuajiriwa bila usaili.

Kwan kada ya ualimu na afya wana u-special upi mpaka wasifanye usaili wakati kada zingine zinafanya usaili?

Utumishi shikilieni hapo hapo, msiachie hata kidogo.
 
Mbaya zaid ety n watu wa afya na waalimu 😂 sasa hawa wataweza kuhudumia jamii kama wanaogopa usaili 😂
Sasa,kama wanaogopa na kuichukia interview ya dakika kumi,vipi interview ya kila siku tuifanyayo maishani hadi kufa wataiweza kweli?
 
Back
Top Bottom