Je, kuna umuhimu kama taifa kufanya usaili kwa kada ya Afya na Ualimu ndo Uajiri?

Waajirwa wa afya Kuna bodi zetu husika Kama pharmacy council, Kila mwanataaluma ana leseni yake ya kazi, Kila mwaka anailipia na pia hufanya CME/CPD Ili kushikilia leseni yake. Hivyo yoyote mwenye leseni hai ni mwanataaluma mwenye ujuzi na Yuko vizuri.

Kifanya mtihani ni upotevu wa muda na pesa ya taifa
Wahasibu wana bodi pia,na wanasajiliwa,Enginers wana bodi na wanasajiliwa pia..lakini interview za kazi wanafanya..wewe ni nani usifanye?
 
Hawa waalimu na watu wa afya wana matatizo ya akili aisee, cjui wanajiona wao n akina nani mpaka wasifanye usaili 😂
Hata ukizaliwa lazima upigwe kofi la makalio ili ulie kama interview.Sembuse kwenda kufundisha na kutoa tiba?Hiki kizazi cha ekibindankoi na milegezo ni chafya ya kimpumu.🤣🙏🤣
 
Mtake msitake, lazima mfanye usaili 😂
Hata wapige mayowe kwa kiwango kipi,usaili ni lazima sana.
-kuwatambua vema wahitajika wa kweli.
-kuepusha udanganyifu na kufanyiana majaribio ya usaili.Atakuja muhusika.
-muda mzuri wa kuvichunguza vyeti.
-kupata maelezo na uwezo binafsi ana kwa ana toka kwa msailiwa.
-kuwajengea kujiamini wasailiwa.
-kuepusha lawama za rushwa kwa kufanya zoezi kwa uwazi.
-kuanza kuwazoesha wasailiwa kuona maana halisi ya ofisi tegemewa.
-kupima uaminifu,uadilifu,usikivu,utimizaji vigezo hitajika na kujali muda.
-kuwasili,kuitika eneo rasmi la usaili na kufanya usaili ni moja ya usaili.
NB:Kizazi hiki kimekua cha viumbe janjajanja sana.Ni vema kuwakusanya pamoja na kukagua vyeti ghushi na watu wasiohusika kupitia wataalamu na vifaa maalumu.Na muda utakaotumika ni mfupi kuliko kuajiri hobelahobela halafu baadaye kuanza kuwafuatilia sehemu za kazi na kutumia malifedha nyingi zaidi na muda mrefu.Wavumilie.
 
Umeua mkuu.

Tena mm nilitamani sana wafanye usaili tatu yn written, practical na Oral ili iwe unyama zaidi 😂
 
Interview yenyewe simpo tuu lkn kelele kibao 😂
Wawe watulivu.Ni usaili wa kawaida tu.Wao wanadhani wakiingia chumba cha usaili watakutana na lidubwana kuuubwaaa linaitwa MR.USAILI.Au wanadhani usaili unafanana na vikwazo walivyowekewa Iran kwamba wataambiwa waviruke kama vikwazo jeshini au kamba.
 
Hawa watu inabidi tuwe nao karibu ili kuwaweka sawa kiakili mana hapo walipo wameshakata tamaa 😂
 
Zamani wahitimu walikua ni wachache, sahizi ni wengi. Ili kuleta fairness katika selection usahili ni muhimu
 
Wahasibu wana bodi pia,na wanasajiliwa,Enginers wana bodi na wanasajiliwa pia..lakini interview za kazi wanafanya..wewe ni nani usifanye?
Leseni zao zinakuja hai Kwa muda Gani?

Unahitaji kuelewa kua Kila mwaka Kuna CPD (Continuous medical/Pharmaceutical education na CME zinafanywa) na wanataaluma hupimwa ujuzi wao na kama wako below wanafutiwa leseni zao.

Kama wako assessed Kila mwaka na bodi husika ya Nini USAILI. Mwajiri anahitaji kujua Nini kwenye interview wakati mamlaka/bodi husika inatambua wanataaluma wao wenye sifa ya kuajiriwa?
 
Waajirwa wa afya Kuna bodi zetu husika Kama pharmacy council, Kila mwanataaluma ana leseni yake ya kazi, Kila mwaka anailipia na pia hufanya CME/CPD Ili kushikilia leseni yake. Hivyo yoyote mwenye leseni hai ni mwanataaluma mwenye ujuzi na Yuko vizuri.

Kifanya mtihani ni upotevu wa muda na pesa ya taifa
Ikiwa kila mtu ana sifa kama unavyosema na nafasi za kazi ni chache huku idadi ya wenye sifa ikiendelea kuongezeka kila mwaka, unadhani njia gani inaweza kutumika ili kuleta usawa kati ya wale watakaopewa kazi na wale watakaokosa kazi?"
 
Leseni zao zinakuja hai Kwa muda Gani?

Unahitaji kuelewa kua Kila mwaka Kuna CPD (Continuous medical/Pharmaceutical education na CME zinafanywa) na wanataaluma hupimwa ujuzi wao na kama wako below wanafutiwa leseni zao.

Kama wako assessed Kila mwaka na bodi husika ya Nini USAILI. Mwajiri anahitaji kujua Nini kwenye interview wakati mamlaka/bodi husika inatambua wanataaluma wao wenye sifa ya kuajiriwa?
Kama hutaki kazi achana na interview. Sawa? Who are you mpaka uipangie serikali cha kufanya?
 
Back
Top Bottom