Je, Kuna Umuhimu wa Kuandika Mchangamanuo/Mpango wa Biashara?

Entareyehirungu

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2006
Posts
488
Reaction score
471
Miaka ya hivi karibuni, katika jitihada za kuhamisha ujasiriamali, uanzishaji wa Biashara na utengenezaji wa ajira kwenye sekta binafsi kumekuwa na msisitizo wa wajasiriamali kuandika michangamanuo/mipango ya Biashara. Kuna wakati wajasiriamali na wajasiriamali-watarajiwa hufikiri kuwa michangamanuo hii ndiyo suluhisho la vikwazo vyao vyote na ufunguo wa mafanikio katika biashara. Leo nataka kutumia mifano miwili kuleta mada ili tujadili kama kweli mchangamanuo/mpango wa Biashara ndiyo kigezo cha mafanikio katika Biashara.

Nitatumia hadithi za wafanyabiashara wawili. Kwa bahati nzuri wote ni wazawa wa Tanzania na hivyo wanafahamika vema na wengi wetu. Nitamtumia Mzee Reginard Mengi mmiliki wa vyombo vya habari vya habari na Mwanahisa Mkuu wa Bonite Bottlers; vyote vikiwa chini ya Kampuni Tanzu ya IPP. Katika mfano wetu nitatumia maji ya Kilimanjaro yaliyo chini ya Bonite Bottlers Ltd. Na katika mfano wa pili, nitamhusisha Mzee Salim Bakheresa. Naamini sihitaji kumsemea sana huyu kwa kuwa, kwa nadra sana mtu aliye Tanzania atapitisha siku bila kutumia bidhaa ya Azam. Asipokula bidhaa ya Azam kama kitafunwa, atailamba kama ice cream na asipoilamba atainywa kama maji au soda. Lakini katika mada hii nitatumia uanzishwaji wa Kiwanda cha vinywaji vya soda za Azam Cola.

Hadithi zinadai kuwa Mzee Mengi baada ya kuona fursa ya kuuza maji safi ya kunywa kwenye chupa, aliamuua kutengeneza mchangamanuo ili umsaidie kuzishawishi taasisi za fedha katika kupata mkopo. Lakini kila alipojaribu kuutembeza mchangamanuo huu, alikwama na mara alipoaga ofisi za hizi Taasisi, Mameneja waliitana, wakamcheka na kumdhihaki kwa kusema "huyu Bwana amechanganyikiwa. Maji atamuuzia nani?". Inasemekana hata baada ya kupata mbadala wa mtaji na kuanzisha kiwanda, Mzee Mengi alipomualika Mwalimu Nyerere katika uzinduzi wa maji ya Kilimanjaro alisema "Wewe Mengi ubepari unakupeleka pabaya. Unataka kuwauzia ndugu zako maji?"

Hadithi ya pili inamuhusu Mzee Bakheresa na uanzishwaji wa Kiwanda chake kilichopo Mbagala Maji-Matitu. Kiwanda hiki ndicho kinachozalisha Azam Cola. Inasemekana kabla ya kuanzisha kiwanda hiki, wataalamu walipewa kazi ya kufanya upembuzi yakinifu na kuandaa mchangamanuo. Baada ya kutimiza kazi yao waliiwakilisha kwa mteja na kumtaarifu kuwa hiyo Biashara ingehitaji mtaji mkubwa, matishio (risks) yake yangekuwa makubwa wakati marejesho yalikuwa hasi (negative returns). Baada ya taarifa hii inasemekana Mzee bakheresa aliomba kitabu cha Hundi na kusaini hundi yenye thamani ya shillingi bilioni tano na kuwaamrisha wataalamu pamoja na timu yake ya uongozi kuanzisha hicho kiwanda haraka sana.

Katika mfano wa kwanza tumeona jinsi Mzee Mengi alivyokuwa na mchangamanuo wa Biashara mzuri lakini hukakosa ladha mbele ya taasisi za kifedha na mwisho ukakataliwa. Lakini pamoja na kukataliwa Mzee Mengi akaweza kuanzisha kiwanda cha maji ya Kilimanjaro yawezekana kwa kutumia mtaji wake mwenyewe. Matokeo ya mchangamanuo wa biashara iliyokataliwa ni bidhaa ya maji ya Kilimjanjaro, maji ambayo sasa yamenunuliwa na nembo ya kimataifa (Coca Cola) na kuzishinda kwa mbali bidhaa nyingine za kimataifa kama DASANI. Vile vile katika mfano wa pili tumeona Wataalamu wakihitimisha kazi ya upembuzi na uandaaji wa mchangamanuo wa Biashara kwa kumshauri Mzee Bakheresa kutoanzisha kiwanda cha vinywaji baridi. Lakini kinyume chake Mzee Bakheresa akakaidi ushauri na kuanzisha vinywaji vya Azam Cola ambayo leo hii ni mshindani mkuu wa vinywaji vya Coca Cola.

Baada ya maelezo haya na mifano hii ningependa tujadili swali moja kuu:

Je, kuna umuhimu wa kuandika Mchangamanuo/Mpango wa Biashara?

Bonus reference:Great Businesses Don't Start With a Plan - Anthony Tjan - Harvard Business Review


[-]<>[-]
[-]<>[-][-]<>[-] [-]<>[-] [-]<>[-][-]<>[-]

Uchochezi wa Mada:

 
[QUOT

Baada ya maelezo haya na mifano hii ningependa tujadili swali moja kuu:

Je, kuna umuhimu wa kuandika Mchangamanuo/Mpango wa Biashara?

Bonus reference:Great Businesses Don't Start With a Plan - Anthony Tjan - Harvard Business Review[/QUOTE]

Sina uhakika kama wote wanaohitaji mchanganuo wanakuwa wanahitaji mkopo, nadhani mchanganuo ni kama mwongozo au kioo cha jambo/biashara/investment unayotaka kuifanya hata kama una mtaji wako.

Mfano; dereva anapokwenda njia mpya, huwa anauliza umbali na hali ya barabara hata kama ni dereva wa siku nyingi na mmbobezi wa kazi hiyo.
 
Business plan ama mchanganuo wa biashara una malengo kadhaa. Mojawapo ni estimation of the cost, during project implementation.

Pia mtazamo mwingine ni kuonyesha faida na hasara za mradi, je outcome za mradi zitarudisha fund zilizotumika katika project implementation?

Pia business plan inatumika katika swala zima la kutafuta funds for financing the project, ingawa most of successful candidates ni wale wenye viable profit generating projects.

Sasa swali langu ni kama Bwana Mengi alikuwa anataka kuanza from the scratch? Au it was already viable project?
As for Bakhressa it was explicit that he was loaded with cash to fund his own project. ..I don't know if am correct, I stand to be corrected.
 
Kaka Malila nimependa sana hoja na mfano uliotumia lakini kwa kuwa mie ni mchokoza mada sitachangia.

...Bwana Mengi alikuwa anataka kuanza from the scratch? Au it was already viable project?..
Historia ya maji safi ya chupa ya kununua kwa Tanzania iliandikwa na Mzee Mengi. Kabla yake, maji safi ya kunywa yalikuwa katika orodha za bidhaa zipatikanazo bure (free goods). Hakukuwa na kiwanda cha maji, kiroba cha maji wala chupa. Ni Mzee Mengi ndiye aliyevumbua latent demand na kuifanyia kazi. Lakini kwa sababu tunaona mambo kwa mtazamo tofauti, Taasisi za kifedha zikachukulia hii kuwa biashara ambayo haiwezi kufanikiwa.
...As for Barkhressa it was explicit that he was loaded with cash to fund his own project. ..I don't know if am correct, I stand to be corrected.
Perhaps you are correct but irrespective of how much he had at disposal, the fact that the Return on Investment (RoI) was found to be negative could have discouraged a normal businessman to move forward and inject that huge sum.
 
That's where the principles of business applies. Take big risks for big investments, though they encourage to take moderate and calculated risks. You win some you lose some, but only winners take risks.
 
Mtazamo wangu ni tofauti kidogo. Hivi tulishawahi kujiuliza ni kwa nini watu wengi waliofanikiwa kibiashara si wanauchumi?Mimi nadhani kuna tofauti kubwa kati ya wazo la biashara na mchanganuo wa biashara.Kwanza lazima uwe na wazo,baada ya kupata wazo,hatua inayofuata ni jinsi ya kuimplement hilo wazo. Mara nyingi kwenye wazo ndipo penye kazi kubwa,na kwa uzoefu,wazo la kuana biashara linategemea zaidi spirit ya ujasiriamali zaidi kuliko elimu ya vyeti! Nitafafanua. Ingekuwa roho ya mafanikio kibiashara ni elimu,hapa namaanisha idea na mchanganuo wa kitalamu/kisomi,basi shughuli nyingi za kiuchumi kwa maana ya biashara ingekuwa inamilikiwa na watamu na wasomi wa mambo hayo.Lkn hii ni tofauti kabisa. Lakini pia tulishawahi kujiuliza ni kwa nini matajiri wengi elimu zao ni za kawaida sana?Jibu lipo wazi kwamba,hawa ni watu wa kujilipua! Ni watu wasioogopa risk! Hawa ni watu wenye spirit ya ujasiriamali! Hiki ni kitu ambacho hutafudishwa shule yoyote.Wakati wasomi wanakaa mezani na michanganuo yao,wajasiriamali wako juani wanatafuta alternatives! Wakati msomi anacalculate faida na risks,mjasiriamali anaminimize risk kutokana na uzoefu aliopata juzi alipopata hasara.Wakati msomi anahesabu hela kwenye makaratasi,mjasiriamali anahesabu hela kwenye pochi au kwenye mradi wake! nk..nk..nk..nk.. Hivi pia tulishajiuliza ni kwa nini watalamu wengi wenye mawazo mazuri ya biasha hatuoni biashara zao wenyewe? Kwani wameshindwa nini kukaa mezani na kuchanganua hiyo michanganuo yao wakapeleka benki wakapewa mikopo wakaanzisha biashara zao? Lakini pia ni wangapi tumewaona wameanza na biashara za kutembeza juani ila baada ya muda tunawaona wanamiliki biashara zao tena nzuri tu;je nani kawachanganulia biashara zao?
 
wapi Chasha, Kubota, Asigwa and the likes?
 
Natambua hapa tutaongea sana,ila kamwe haitabadili ukweli kwamba, mafanikio huja kutokana na spirit ya kuthubutu,kujituma na kutokata tamaa-mimi huo ndio naona mchanganuo wa biashara.

Mtachanganua sana biashara kweye makaratasi,lakini mwisho wa siku biashara ni wazo zuri la biashara,mazingira mazuri,mtaji,wateja na juhudi binafsi.. Ni mara chache sana mtu akaanzia mbali na kamtaji kadogo,baadaye mataji ukakua na kupata mafanikio halafu akakwama eti kwa sababu hakua na mchanganuo wa biashara.

Ila ni mara nyingi sana mtu akawa na mchanganua mzuri wa biashiara na mtaji wa kutosha lkn akaja akafeli ikiwa hana spirit ya ujasiriamali.. Halafu mimi naamini spirit ya ujasiriamali mtu anazaliwa nayo au anajifunza kutoka akiwa mdogo kabisa..
 

Hujajibu swali la msingi ambalo ni; je mchanganuo wa biashara ni muhimu au la? Nadhani mtoa maada analenga huko. Sasa kufanikiwa au kutofanikiwa sio hoja mama.
 
Mchanganuo Wa Biashara si kwa ajili ya Kupeleka Benk pekee, Mchanganuo una kazi nyingi sana katika Biashara.

1. Kwanza hutakiwi kupelekea watu wakuandalie Mchanganganuo wako, Mchanganauo unatakiwa utokane na kile unacho amini wewe

2. Vision na Mision ni muhimu sana katika Biashara yako unapelekea watu wa edit na kuweka wanavyo taka ni mbaya sana

3. Kilichopo kwenyeVision ni lazima kifikiwe.

4. Wafanyakazi wako wanatakiwa wausome mchanganuo wa Biashara yako kabla ya Kuanza kazi, wengi hatufanyi hivyo matokeo yake wafanyakazi wanafanya kazi bora liende na hawajui kampuni ina malengo gani au imejiwekea malengo gani.

5. Mchanganuo ndo time table yako, manake ndo time frame ya kila kitu.

6. Kwa wale wanaotafuta joint venture ni lazima uwe na mchangauo wako.

7. Mambo yanapoenda vibaya kwenye business sehemu ya kufanya mlinganisho ni kweye mchanganuo wako.
 
Hujajibu swali la msingi ambalo ni; je mchanganuo wa biashara ni muhimu au la? Nadhani mtoa maada analenga huko. Sasa kufanikiwa au kutofanikiwa sio hoja mama.
Obvious hakuna mtu atakayesema hakuna maana ya kuwa na mpango katika biashara yake;maana maana hata wakati wa butter trade kulikuwa na wafanya biashara wengi ambao walikuwa hawajui kusoma na kuandika ila walikuwa na mipango yao ya kuendesha biashara..Ninachosimamia mimi ni kitendo cha kusubiri au kuwatafuta watalam wanaojitangaza(hata humu wamo)kutoa ushauri wa kibiashara ikiwa ni pamoja na kuandika hiyo michanganuo ya kisomi,ili mtu aanze mradi wake.

Na hapa ndipo watu wengi wanapofeli..siamini unaweza vipi kusimamia mawazo ya mtu mwingine au nadharia uliyopata sehemu fulani ikiwa huna spirit au ile self motivation ambayo aidha umezaliwa nayo,au umejifunza tangu upo mtoto.. Je,tulishawahi kujiuliza ni kwa nini matajiri wengi wameanza kufanikiwa ktk umri mdogo?? Jibu lipo wazi..wamezaliwa na spirit ya ujasiriamali au wamejifunza wangali wadogo na kutumia vizuri fursa walizopata..

Sasa sisi tunaosubiri tusomee biashara au tuandikiwe michanganuo ndio wengi wetu tunaohangaika na makaratasi na kulialia na serikali iongeze mishahara ili tupate mitaji mikubwa ya kuanzisha biashara biashara ya maana..kwanini? Kwa sababu ktk mchanganuo lazima uoneshe wapi utapata capital,na biashara gani nzuri yenye faida na heshima mtaani kwetu!!

Kwa kuwa umesema mada ni kuhusu michanganuo na si mafanikio,basi pengine ungetusaidia ikiwa tunafanya mchanganuo huo ili iweje? Na kwa hakika wengi wetu tutasema mchanganuo mzuri ndio unaoleta mafanikio,na wengi watasema,mchananuo wa msomi utakuwa bora kuliko wa mtu asiye msomi!
 
Mrimi

Nakubaliana na ww kwa mengi sana ktk hoja yako.

Kioo kikikuonyesha kuwa hujavaa vizuri hakiwezi kukuzuia kwenda matembezini, pia kikikuonyesha kuwa umependeza bado haina maana kuwa hutapata matope njiani, lakini kioo kinabaki pale pale kuwa kimekuonyesha ulivyo. Mchanganuo hata uwe mzuri vipi haujitekelezi, mtekelezaji ni wewe, mchanganuo uko pale kama kioo cha kazi unayotaka kufanya tu.

Hawa unaowasema ni risk takers na ndio maana wanaishia kupata high returns. Hata mimi nilishakutana nayo hayo sana lakini siachi kuchanganua ninachofanya na kuweka pamba masikioni ktk utekelezaji ili nivuke.
 
Last edited by a moderator:
Ninachokiona hapa kuna mgongano wa vitu viwili, kimoja ni bussiness idea na kingine ni mchanganuo wake

  • Mengi na Bakhresa walikua na bussiness idea na hawakuwa wazuri sana katika kuandaa mchanganuo.Na hapa ndipo ilipolala siri ya ujasiriamali.Wao wana uwezo wa kuona opportunities na wakazitambua lakini hawawezi kuziainisha
  • Mchanganuo wa kibiashara hufanywa na wataalamu waliosomea mambo hayo japo si lazima wawe na entrepreneurship spirit. Kitu MENGI/BAKRESA walichoshindwa kuelewana hawa jamaa wa michanganuo ni either hawakuelewa nini jamaa walichokiona au professional zao zimekaa kimadesa sana hawaelewi nini kiko katika actual field

Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuwa na mchanganuo wa kibiashara hasa kutoka kwa mtaalamu aliyebobea japo inaweza ikawa ni kikwazo kwa mjasiriamali ambaye ana bussiness idea yake na akashindwa kupata mtu ambaye ana bussiness spirit kama yake.

Mara nyingi kigezo kinachofanya kuonekana kuwa IDEA fulani haifai ni NEGATIVE RETURNS na mara zote ni kutokana na RISKS katika biashara. Lakini mjasiriamali yeyote anatakiwa kuona mambo kwa mtazamo chanya sana kwani RISKS zipo na faida kubwa katika biashara hupatikana katika sehemu yenye RISKS kubwa
 

Nadhani hili suala tusilione kama ni unique kwa Tanzania tu. Hali hii huwakuta wajasilia mali wengi sehemu mbali mbali duniani. Hebu ona hii:

 


Mkuu Mimi huwa niko Against na kuandikiwa Mchanganuoa na watalamu, Tatizo kubwa sana ni kwamba watalamu wako kibiashara na kitu kingine, na mkuu Mchangnoa hata siku moja hauweziandaliwa mtu akiw amekaa Ofisini, hapo ndo watu huwa wana kosea, na waandishi waMichanganuoa wanacho fanya ni Ku edit michananuomingine, usidhani kamba huwa wanaandika mwanzo mwisho

Mchanganuoa, ni mawazo yako na jinsi unavyo fikilia biashara yako iwe, namchanganuoa si lazimaufuate zile hatua zote za Michanganuo, No unaweza andika kadri unavyo ona ina faa nabado ikakuongoza,

Nakumbuka kuna sehemu nilisoma Kulikuwa na Mashindano ya Kuandaa michangauo ya Biashara, sasa watu walicho fanya ni kuafuta waandaaji na wakawaandalia michanganuo si kabisa, Ila alitokea mtu ambaye yeye aliandika mwenyewe na aliandika page tatu tu,na wahusika walivyo pitia kwa kweli ilibidi jamaa ashinde kwa sababu mchanganuo pamoja na kwamba haukufuata hatua lakini jamaa alijitahidi sana na kulikuwa na point

Na tatizo kubw sana linalotusua nin kuamini kwamba unaweza mpigia simu mtu na akakuandalia mchanganuo bora, ni Ok kwa taasisi za Kifedha za Bongo unaweza pata mke nao wao wako kimagumashi sana,

Ila ikija kwamba mchanganuo ukusaidie katika biashara yako, ni lazima uwe umeweka kile unacho taka,
Vitu kama Mision na Vision si vitu vya kujiandikia tu ilimuradi
 

Mkuu Hapa kuna Vitu Viwili vinachanganywa

1. Spirit

2. Mchanganuo/Mpango kazi wako

-Mkuu Spirit ya Ujasirimali haina uhusiano na Mchanganuo, na Spirit ni kuwa na hamu sana na biashara na inakusaidia kuto kata tamaa kabisa, na ndo Driving Force katika maisha ya Ujasrimali,

- Unaweza ukawa na hiyo Spirit na usiwe na mafanikio katika biashara yako, na si kweli kambwa kila mwenye hiyo Spirit ni lazima afanikiwe, no Spirit inahitaji force nyingine ya kukupeleka mbele zaidi

- Ndo maana huwa nasema Entreprenership haifundiswi Chuoni, na hakuna Chuo hapa Duniani cha Kufundisha Ujasiriamali, WHY? Kwa sababu Spirt ya Ujasirimali haifundishwi kamwe, ile hutoka moyoni mwako ni like Mapenzi huwezi fundisha mtu Kumpenda mtu fulani, kama hampendi ni hampendi

- So Nini Kinafundishwa Vyuoni?
Kule wanafundisha mambo kama vile, Masoko, Jinsi ya Kuandaa mchanganuo ya biashara, mambo ya Financial plan, customer care, sales skills, Pricing na kazalika, haya hayaitaji Spirit ni lazima either uyasome ili kukusaidia katika biashara zako

-SO KWA NINI WATU WENGI WANA SHINDWA BASI PAMOJA NA KUWA NA MICHANGANUO?
-Jibu ni kwamba hata ukiwa na mchanganu bora kuwahi kutokea, bila utekelezaji mzuri ni hakuna kitu, ni lazima uwe na hiyo Spirit ili usonge mbele na biashara yako

-NA KWA NINI KUNA WATU WAKO KATIKA BIASHARA MIAKA 3O LAKINI HAWAJAPIGA HATUA?
Utakubaliana na mimi kwamba kuna baashi ya watu Mfano, MAMA LISHE, MAFUNDI WA KUTENGENEZA/KUCHONGA MAJIKO NA KAZALIKA, WA MAMA WANAO PIKA VITUMBUA.MANDAZI

Hawa wako kwenye game miaka mingi sana, na wengi wako pale pale n unawaona kweli wako na juhudi sana za kazi zao, mara nyingi hawa ndo wana kosa elimu ya Ujasirimali/Biashara ambayo inaweza wasaidia kujua sasa wana move vipi kutoka hapo walipo, wana kosa kuchanganua mambo

MWISHO, KUNA WATU WENGI SANA WALIKUWA WAFANYA BIASHARA WAZURI/WAJASIRIMLI WAZURI LAKINI LEO HII HAWAPO, WALSHA FILISIKAU KUFA, NA WALIKUWA WANAMILIKI BIASHRA MBALIMBALI

Hawa walikuwa Wajasirimali but walikosa elimu y kuwapeleka mbele, walikuwa hawajui wana panga vipi bei zao, walikuwa hawaui wnatakiwa kwa wapi miaka 30 ijayo, walikwa hawajui wanadill vipi a ushindani, so that is why leo hii hawapo tena,

NA SI KWEI KWAMBA UKIWA NA SPRIT NDO HUWEZI FILISIKA AU KUPOTEA KABISA KWENYE GAME,NA MCHANGAUO UNAWEZA ANDAA WEWE MWENYEWE,

INGAWA KUNA WATU WANA UN WRITEN BUSINESS PLANING, YAANI WAMEANDIKA TU VICHWANI MWAO
 
Nawashukuru wachangiaji na wasomaji wa mada hii. Michango yote inayotolewa inalo la maana kwa mjasiriamali makini. Naamini ipo siku hadithi na michango ya mada hii itatumika kwenye mafunzo ya Ujasiriamali. Hivyo kwa hakika tunajadili mada yenye tija kwa Taifa na vizazi vyake.

Michango mingi inaona umuhimu wa mjasiriamali kuwa na Mpango wa Biashara. Franky ametuhamasisha kuchukua uthubutu uliokadiriwa vema, Mrimi katuhoji ni kwa nini watalamu wengi wenye mawazo mazuri ya biashara hatuoni biashara zao wenyewe na pia yeye anaona ujasiriamali ni hali mtu anazaliwa nayo. mito umefanya kazi nzuri kutuletea Chasha na asigwa. Wametupa michango murua inayotokana na uzoefu halisi kutoka uwanja wa Biashara. Namshukuru pia ndugu yetu Nyenyere kwa kutukumbusha kuwa fursa ya Biashara inapokuja, huja na muonekano tofauti na katika muelekeo tofauti. Na mara nyingi ina tabia ya kujificha katika bahati mbaya au vikwazo vya muda mfupi. Ujio wa namna hii ndiyo hutuhadaa wengi kukata tamaa na kuikimbi fursa njema.

Asante Kaka Malila kwa kutudhibiti ili tubaki kwenye hoja ya msingi. Lakini haitakuwa vibaya kama katika kuichambua mada na kuitafakari mifano iliyotumika tukitanua wigo kwa kuangalia ni vitu gani vya ziada vinavyoukamilisha Mpango wa Biashara kuwa nyenzo ya muhimu kwa mafanikio ya mjasiriamali? Yawezekana ni tabia! Tabia gani? Nasaba; nasaba zipi? Elimu! Kwa namna gani? Na mengine mengi.

Naendelea kuufuatilia huu mjadala kwa karibu. Nitaongea na Kaka Maxence Melo tujadili jinsi tunavyoweza kuufikisha mjadala kwenye hitimisho lenye maazimio endelevu na kisha nitawashirikisha wachangiaji wote. Wachangiaji mnaweza kupendekeza mada hii ifunge rasmi lini au iachwe huru?
 
Mleta mada,

Nimependa mifano uliyotumia kusupport mada lakini nafikiri ni ya upande mmoja tu, labda tungepata na mifano inayoonyesha waliofanikiwa kibiashara kwa kuandikiwa / kuandika michanganuo ya biashara zao ili kuleta uzito sawa kwenye mada.

Swali kwako, Je unafikiri Mzee Bakheresa angekua katika nafasi nzuri ya kuandika hundi ya "Tshs bilioni tano" kwa ajili ya biashara yake mpya ya Azam Cola bila kuona "gharama halisi" za utekelezaji katika mchanganuo wa biashara?

Umuhimu wa mpango biashara hutegemea mambo kadha wa kadha ,mfano: Lengo la mpango biashara - kukopa / kukuza mtaji au mwongozo, mipango ya mbele ya biashara, nyenzo ya kujitathmini kibiashara - kujua kama biashara inafikia malengo au la n.k. Katika mazingira ya sasa ya biashara na kasi ya mabadiliko ya uendeshaji biashara nafikiri faida za kutumia mpango biashara zinazidi hasara. Hivyo, nathubutu sema kwamba kuna umuhimu wa kuandika mpango biashara kwa ajili ya ustawi chanya wa biashara.
 
Mchanganuo wa biahara ni muhimu kwa ukuaji wa biashara. tatizo wengi wanafikiri kwamba utaandaa mchanganuo pale tu utapohitaji kukopa mtaji kutoka taasisi mbalimbali. mchanganuo wa biahsara ndio muelekeo wa biashara yako, malengo yake na hatua za ukuaji. kutkuwa na mchanganuo ndiko kunafanya biashara nyingi hazikui miaka yote zipo vile vile tu.

Kama alivyosema CHASA kuandikiwa mchanganuo wa biashara na mtu ndio sababu kubwa ya biashara nyingi kushindwa. ila kama mtu atasaidiwa kuandika mchanganuo na mtaalamu kwa kutumia mawazo yake ya biashara inaweza kumsaidia sana kwa sababu kuna vitu labda hakuviweka maanani wakati anafikiria utekelezaji wa wazo lake.

Mwisho tusilinganishe biashara za wakati huu na za zamani(hata miaka 5 iliypita), teknolojia imekuwa kwa kasi sana miaka ya hivi karibuni hivyo bila ya kuwa na mpango madhubuti ni dhahiri njia itakuwa ngumu.
 
Nimependa mifano uliyotumia kusupport mada lakini nafikiri ni ya upande mmoja tu, labda tungepata na mifano inayoonyesha waliofanikiwa kibiashara kwa kuandikiwa / kuandika michanganuo ya biashara zao ili kuleta uzito sawa kwenye mada..
Asante lakini samahani sijakupata vema.
  1. Maji ya Kilimanjaro ni bidhaa ya Mzee Mengi yenye mafanikio na zao la Mpango wa Biashara uliokataliwa na Taasisi za Kifedha
  2. Vinywaji vya Azam Cola ni mali ya Azam Group of Companies mali ya Mzee Salim Bakheresa navyo pia vinafanya vema lakini ni zao la Mpango wa Biashara ulioonyesha matishio makubwa kwenye marejesho ya uwekezaji
Hivyo katika mifano yote Michangamanuo ya Kibiashara iliandikwa na biashara zote zilianzishwa na zinaendelea kwa mafanikio makubwa
Swali kwako, Je unafikiri Mzee Bakheresa angekua katika nafasi nzuri ya kuandika hundi ya "Tshs bilioni tano" kwa ajili ya biashara yake mpya ya Azam Cola bila kuona "gharama halisi" za utekelezaji katika mchanganuo wa biashara?.
Jibu lako ni HAPANA. Na nyongeza ya hapo hizo siyo gharama halisi bali makadirio ya kiasi kinachohitajika kwa uwekezaji kamilifu. Gharama halisi zinapatikana baada ya uwekezaji kuwa umekamilika.
Asante kwa mchango wako mzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…