Entareyehirungu
JF-Expert Member
- Oct 27, 2006
- 488
- 471
Miaka ya hivi karibuni, katika jitihada za kuhamisha ujasiriamali, uanzishaji wa Biashara na utengenezaji wa ajira kwenye sekta binafsi kumekuwa na msisitizo wa wajasiriamali kuandika michangamanuo/mipango ya Biashara. Kuna wakati wajasiriamali na wajasiriamali-watarajiwa hufikiri kuwa michangamanuo hii ndiyo suluhisho la vikwazo vyao vyote na ufunguo wa mafanikio katika biashara. Leo nataka kutumia mifano miwili kuleta mada ili tujadili kama kweli mchangamanuo/mpango wa Biashara ndiyo kigezo cha mafanikio katika Biashara.
Nitatumia hadithi za wafanyabiashara wawili. Kwa bahati nzuri wote ni wazawa wa Tanzania na hivyo wanafahamika vema na wengi wetu. Nitamtumia Mzee Reginard Mengi mmiliki wa vyombo vya habari vya habari na Mwanahisa Mkuu wa Bonite Bottlers; vyote vikiwa chini ya Kampuni Tanzu ya IPP. Katika mfano wetu nitatumia maji ya Kilimanjaro yaliyo chini ya Bonite Bottlers Ltd. Na katika mfano wa pili, nitamhusisha Mzee Salim Bakheresa. Naamini sihitaji kumsemea sana huyu kwa kuwa, kwa nadra sana mtu aliye Tanzania atapitisha siku bila kutumia bidhaa ya Azam. Asipokula bidhaa ya Azam kama kitafunwa, atailamba kama ice cream na asipoilamba atainywa kama maji au soda. Lakini katika mada hii nitatumia uanzishwaji wa Kiwanda cha vinywaji vya soda za Azam Cola.
Hadithi zinadai kuwa Mzee Mengi baada ya kuona fursa ya kuuza maji safi ya kunywa kwenye chupa, aliamuua kutengeneza mchangamanuo ili umsaidie kuzishawishi taasisi za fedha katika kupata mkopo. Lakini kila alipojaribu kuutembeza mchangamanuo huu, alikwama na mara alipoaga ofisi za hizi Taasisi, Mameneja waliitana, wakamcheka na kumdhihaki kwa kusema "huyu Bwana amechanganyikiwa. Maji atamuuzia nani?". Inasemekana hata baada ya kupata mbadala wa mtaji na kuanzisha kiwanda, Mzee Mengi alipomualika Mwalimu Nyerere katika uzinduzi wa maji ya Kilimanjaro alisema "Wewe Mengi ubepari unakupeleka pabaya. Unataka kuwauzia ndugu zako maji?"
Hadithi ya pili inamuhusu Mzee Bakheresa na uanzishwaji wa Kiwanda chake kilichopo Mbagala Maji-Matitu. Kiwanda hiki ndicho kinachozalisha Azam Cola. Inasemekana kabla ya kuanzisha kiwanda hiki, wataalamu walipewa kazi ya kufanya upembuzi yakinifu na kuandaa mchangamanuo. Baada ya kutimiza kazi yao waliiwakilisha kwa mteja na kumtaarifu kuwa hiyo Biashara ingehitaji mtaji mkubwa, matishio (risks) yake yangekuwa makubwa wakati marejesho yalikuwa hasi (negative returns). Baada ya taarifa hii inasemekana Mzee bakheresa aliomba kitabu cha Hundi na kusaini hundi yenye thamani ya shillingi bilioni tano na kuwaamrisha wataalamu pamoja na timu yake ya uongozi kuanzisha hicho kiwanda haraka sana.
Katika mfano wa kwanza tumeona jinsi Mzee Mengi alivyokuwa na mchangamanuo wa Biashara mzuri lakini hukakosa ladha mbele ya taasisi za kifedha na mwisho ukakataliwa. Lakini pamoja na kukataliwa Mzee Mengi akaweza kuanzisha kiwanda cha maji ya Kilimanjaro yawezekana kwa kutumia mtaji wake mwenyewe. Matokeo ya mchangamanuo wa biashara iliyokataliwa ni bidhaa ya maji ya Kilimjanjaro, maji ambayo sasa yamenunuliwa na nembo ya kimataifa (Coca Cola) na kuzishinda kwa mbali bidhaa nyingine za kimataifa kama DASANI. Vile vile katika mfano wa pili tumeona Wataalamu wakihitimisha kazi ya upembuzi na uandaaji wa mchangamanuo wa Biashara kwa kumshauri Mzee Bakheresa kutoanzisha kiwanda cha vinywaji baridi. Lakini kinyume chake Mzee Bakheresa akakaidi ushauri na kuanzisha vinywaji vya Azam Cola ambayo leo hii ni mshindani mkuu wa vinywaji vya Coca Cola.
Baada ya maelezo haya na mifano hii ningependa tujadili swali moja kuu:
Je, kuna umuhimu wa kuandika Mchangamanuo/Mpango wa Biashara?
Bonus reference:Great Businesses Don't Start With a Plan - Anthony Tjan - Harvard Business Review
[-]<>[-] [-]<>[-][-]<>[-] [-]<>[-] [-]<>[-][-]<>[-]
Uchochezi wa Mada:

Nawashukuru wachangiaji na wasomaji wa mada hii. Michango yote inayotolewa inalo la maana kwa mjasiriamali makini. Naamini ipo siku hadithi na michango ya mada hii itatumika kwenye mafunzo ya Ujasiriamali. Hivyo kwa hakika tunajadili mada yenye tija kwa Taifa na vizazi vyake.
Michango mingi inaona umuhimu wa mjasiriamali kuwa na Mpango wa Biashara. Franky ametuhamasisha kuchukua uthubutu uliokadiriwa vema, Mrimi katuhoji ni kwa nini watalamu wengi wenye mawazo mazuri ya biashara hatuoni biashara zao wenyewe na pia yeye anaona ujasiriamali ni hali mtu anazaliwa nayo. mito umefanya kazi nzuri kutuletea Chasha na asigwa. Wametupa michango murua inayotokana na uzoefu halisi kutoka uwanja wa Biashara. Namshukuru pia ndugu yetu Nyenyere kwa kutukumbusha kuwa fursa ya Biashara inapokuja, huja na muonekano tofauti na katika muelekeo tofauti. Na mara nyingi ina tabia ya kujificha katika bahati mbaya au vikwazo vya muda mfupi. Ujio wa namna hii ndiyo hutuhadaa wengi kukata tamaa na kuikimbi fursa njema.
Asante Kaka Malila kwa kutudhibiti ili tubaki kwenye hoja ya msingi. Lakini haitakuwa vibaya kama katika kuichambua mada na kuitafakari mifano iliyotumika tukitanua wigo kwa kuangalia ni vitu gani vya ziada vinavyoukamilisha Mpango wa Biashara kuwa nyenzo ya muhimu kwa mafanikio ya mjasiriamali? Yawezekana ni tabia! Tabia gani? Nasaba; nasaba zipi? Elimu! Kwa namna gani? Na mengine mengi.
Naendelea kuufuatilia huu mjadala kwa karibu. Nitaongea na Kaka Maxence Melo tujadili jinsi tunavyoweza kuufikisha mjadala kwenye hitimisho lenye maazimio endelevu na kisha nitawashirikisha wachangiaji wote. Wachangiaji mnaweza kupendekeza mada hii ifungwe rasmi lini au iachwe huru?