Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu mleta mada, nimeangalia andiko na michango kibao sijasoma kwa undani ila nimekerwa na nukuu ya Bonus reference:Great Businesses Don't Start With a Plan - Anthony Tjan - Harvard Business Review!
Nitakuja nichangie kisawasawa maana haya mambo ya kuona baadhi ya watu walishawahi kufanikisha mambo yao kwa kubahatisha then ndiyo tunaifanya inakuwa ni principle siyo sahihi.
Nitasoma na nitachangia lakini awali ya yote plan ni jambo la lazima siyo kwenye biashara tu ni katika fani zote, architects, surgeons, engeneers, hata waalimu wanatengeneza lesson plans! Business plan siyo kitu cha pekee sana, plan is a plan hata kama ni ujenzi wa nyumba. Kujiendea endea tu ndiyo matokeo haya Dar es Salaam yote ni skwata!! Hakuna hata pa kupitisha barabara!!
Mnaoshabikia doing things without planning mnaturudisha gizani, ni kufundishana uchawi na wengine hatuko tayari! Nitarudi !!! (Sijaisoma hoja yote mnisamehe kama nimepotoka nitajisahihisha nikiisoma yote).
Nikauliza:;kwamba,IKIWA MTU ANASHINDWA KU-INTEGRATE MCHANGANUO NA BIASHARA HALISI,BASI MCHANGANUO SI MUHIMU SANA,ILA KUNA KITU MUHIMU KINAKOSEKANA.Kumbe ili mjadala ili uwe na manufaa,tunatakiwa kutegua hicho kitu muhimu kilichojificha.
Yawezekana nikaonekana kama nahamisha mada na kuielekeza kwingine,inawezakana kwa mtazamo wa haraka..ila kwa undani wake,lazima tukubali kwamba,ikiwa mchanganuo una umuhimu huo tunaoona,then kwanini watu wengi washindwe kuutafsiri ktk biashara halisi? Tena kibaya zaidi watalamu na wasomi wenye uwezo wa hali ya juu kabisa ktk kuandaa michanganuo hii kitalamu,ndio wanaofeli zaidi zoezi hi!!
........ Lakini pia tulishawahi kujiuliza ni kwa nini matajiri wengi elimu zao ni za kawaida sana?Jibu lipo wazi kwamba,hawa ni watu wa kujilipua! Ni watu wasioogopa risk! Hawa ni watu wenye spirit ya ujasiriamali! ...................
Plan ni lazima, ingawa sishabikii kuufuata ushauri wa kila mtaalamu, lakini kwa kila lengo ni lazima uwe na plan jinsi gani utalifikia. Hapa ndio unakutana na mikopo nk. Mifano ya wajasiriamali hao wawili ni kuwa tayari waliishafanya utafiti na kufikia malengo yao. Mengi alihitaji extra capital na mwingine hakuhitaji lakini tunaona washauri au watalaamu wetu waliwakatisha tama hivyo kuamua kuendelea na malengo yao. Bila plan huwezi fanya kitu ila simaanishi complicated plans ambazo unaomba kutengenezewa hata wewe mwenyewe huelewi inamaanisha nini. Ndo maana watu wanachukua mikopo mikubwa kwa plan hizi za kutengenezewa na ma cashflow yasiyo real kwani hawajafanya utafiti wowote matokeo yake biashara zinaanguka wanashindwa kurudisha hii mikopo. Plan uwe nayo mwenyewe na hapo utajua ni means gani za kufikia malengo yako sio kuchukua ya mtu au kuandukiwa bila kuielewa vizuri.
KUBOTA najua unanizungumzia mimi, ok niko mbali na sitaweza kuandika vyema kwa kutumia simu ila by kesho au kesho kutwa nitajibu
Mchanganuo Wa Biashara si kwa ajili ya Kupeleka Benk pekee, Mchanganuo una kazi nyingi sana katika Biashara.
1. Kwanza hutakiwi kupelekea watu wakuandalie Mchanganganuo wako, Mchanganauo unatakiwa utokane na kile unacho amini wewe
2. Vision na Mision ni muhimu sana katika Biashara yako unapelekea watu wa edit na kuweka wanavyo taka ni mbaya sana
3. Kilichopo kwenyeVision ni lazima kifikiwe.
4. Wafanyakazi wako wanatakiwa wausome mchanganuo wa Biashara yako kabla ya Kuanza kazi, wengi hatufanyi hivyo matokeo yake wafanyakazi wanafanya kazi bora liende na hawajui kampuni ina malengo gani au imejiwekea malengo gani.
5. Mchanganuo ndo time table yako, manake ndo time frame ya kila kitu.
6. Kwa wale wanaotafuta joint venture ni lazima uwe na mchangauo wako.
7. Mambo yanapoenda vibaya kwenye business sehemu ya kufanya mlinganisho ni kweye mchanganuo wako.