Je, Kuna Umuhimu wa Kuandika Mchangamanuo/Mpango wa Biashara?

Je, Kuna Umuhimu wa Kuandika Mchangamanuo/Mpango wa Biashara?

Mkuu Hapa kuna Vitu Viwili vinachanganywa

1. Spirit

2. Mchanganuo/Mpango kazi wako

-Mkuu Spirit ya Ujasirimali haina uhusiano na Mchanganuo, na Spirit ni kuwa na hamu sana na biashara na inakusaidia kuto kata tamaa kabisa, na ndo Driving Force katika maisha ya Ujasrimali,

- Unaweza ukawa na hiyo Spirit na usiwe na mafanikio katika biashara yako, na si kweli kambwa kila mwenye hiyo Spirit ni lazima afanikiwe, no Spirit inahitaji force nyingine ya kukupeleka mbele zaidi

- Ndo maana huwa nasema Entreprenership haifundiswi Chuoni, na hakuna Chuo hapa Duniani cha Kufundisha Ujasiriamali, WHY? Kwa sababu Spirt ya Ujasirimali haifundishwi kamwe, ile hutoka moyoni mwako ni like Mapenzi huwezi fundisha mtu Kumpenda mtu fulani, kama hampendi ni hampendi

- So Nini Kinafundishwa Vyuoni?
Kule wanafundisha mambo kama vile, Masoko, Jinsi ya Kuandaa mchanganuo ya biashara, mambo ya Financial plan, customer care, sales skills, Pricing na kazalika, haya hayaitaji Spirit ni lazima either uyasome ili kukusaidia katika biashara zako

-SO KWA NINI WATU WENGI WANA SHINDWA BASI PAMOJA NA KUWA NA MICHANGANUO?
-Jibu ni kwamba hata ukiwa na mchanganu bora kuwahi kutokea, bila utekelezaji mzuri ni hakuna kitu, ni lazima uwe na hiyo Spirit ili usonge mbele na biashara yako

-NA KWA NINI KUNA WATU WAKO KATIKA BIASHARA MIAKA 3O LAKINI HAWAJAPIGA HATUA?
Utakubaliana na mimi kwamba kuna baashi ya watu Mfano, MAMA LISHE, MAFUNDI WA KUTENGENEZA/KUCHONGA MAJIKO NA KAZALIKA, WA MAMA WANAO PIKA VITUMBUA.MANDAZI

Hawa wako kwenye game miaka mingi sana, na wengi wako pale pale n unawaona kweli wako na juhudi sana za kazi zao, mara nyingi hawa ndo wana kosa elimu ya Ujasirimali/Biashara ambayo inaweza wasaidia kujua sasa wana move vipi kutoka hapo walipo, wana kosa kuchanganua mambo

MWISHO, KUNA WATU WENGI SANA WALIKUWA WAFANYA BIASHARA WAZURI/WAJASIRIMLI WAZURI LAKINI LEO HII HAWAPO, WALSHA FILISIKAU KUFA, NA WALIKUWA WANAMILIKI BIASHRA MBALIMBALI

Hawa walikuwa Wajasirimali but walikosa elimu y kuwapeleka mbele, walikuwa hawajui wana panga vipi bei zao, walikuwa hawaui wnatakiwa kwa wapi miaka 30 ijayo, walikwa hawajui wanadill vipi a ushindani, so that is why leo hii hawapo tena,

NA SI KWEI KWAMBA UKIWA NA SPRIT NDO HUWEZI FILISIKA AU KUPOTEA KABISA KWENYE GAME,NA MCHANGAUO UNAWEZA ANDAA WEWE MWENYEWE,

INGAWA KUNA WATU WANA UN WRITEN BUSINESS PLANING, YAANI WAMEANDIKA TU VICHWANI MWAO

Mkuu tuko pamoja naafikiana na wewe kwa mambo mengi ila twende taratibu wengine tuko wazito kuelewa baadhi ya maelekezo. Ninakubaliana kweli kwamba suala la spirit lipo kwa kiasi kikubwa. Sasa kuifanya story iwe fupi ni kwamba hao wenye spirit wapo ni wengi na wengi wamelala, hawajijui tu kuwa wanapotential ya kuwa matajiri! Hao wanahitaji kuhamasishwa kuamsha spirit zao, ni watu wako gereza la kifikra kwa kujiona kuwa wamefungwa na mambo fulani na visingizio kibao kama vile ambavyo wewe Mkuu umekuwa ukifundisha hapa! Spirits huamshwa, ndiyo mafunzo hayo! Kuna watu wanajua kuhamasisha mtu hadi anafunguka! Kuna mbinu zipo za kuamsha spirit na kumfundisha mtu jambo lolote akaweza kulifanya! Haya yanafanyika kila siku watu wanaingia kwenye gemu. Kudhani kwamba ujasiria mali haufundishiki na hakuna chuo cha ujasiria mali duniani hayo ni maneno mazito kuyasemea tu humu JF ambamo kila mtu anasema chochote!!

Hapo kwenye red Mkuu unahitaji kuweka wazi unamaanisha kitu gani iwapo hicho ndicho hicho hicho unakikataa siku zote! Hapo unasisitiza na unakubaliana na ukweli kuwa ujasiria mali unafundishwa. Tujikite kwa hao hao wenye spirit, hao hao wenye courage na hao hao wenye burning desire to be rich, hao hao wachache wenye enthusiasm, suala la kufundisha ujasiria mali lipo pale pale, maneno kuwa ujasiria mali haufundishiki hizo ni lugha za vijiweni tu.
 
Mkuu KUBOTA (na wengine wengi) shukran kwa maoni yako, lakini ningependa kuwajua hao wataalam ni wapi ? ? ? je ni yule aliyejufunza field/mtaani na kufanikisha kama vile Bakheressa au Mengi ? ? ? au ni yule aliyekaririshwa ndani ya vyumba vya madarasa tu na yeye hana hata mfano hai ? ? Nahisi wewe utakuwa aidha Mhasibu / Finance Manager/ economist by professional na kama nimepatia kwa akili yako kubwa inavyoonekana na kwa kujiamini nakushauri uongezee kusoma program yeyote ya ENTRPRENEURSHIP nadhani utakamilika haswa,,,,,,, sisi tunasema DARASA LA UHAKIKA NI VITENDO,,,,

Who is a Professional Entrepreneur ? ? juma mwenye degree tatu za biashara au Bakheressa na Mengi ? ?
Kimsingi utaalam maana yake ni kuwa na maarifa mengi ya kufanikisha mradi au jambo fulani,, Je unadhani huyo Bakheressa hana hayo maarifa ? kwa uhakika hao wafanyabiashara wana madegree zaidi ya tatu tatu hasa ukifanya assessment ya kitaalam utakuta yale yote yalioko madarasani wanayajua yote.

Vile vile kusoma kwa maana ya elimu ili kupata maarifa sio lazima uingie darasani ? mfano mzuri wa elimu ya field/mitaani ni Raisi wa S.A. Jacob Zuma ambaye wanadhani hata hiyo primary education hana...
mfano wa pili ni huyo Bakheressa na wengine wengi tu....

Sasa basi kuhitimisha mimi nasema kama ni mtaalam wa uhakika kama ulivyoshauri ni hao ma mentor kama Mengi, Bakheressa, na wengine wengi uwaulize plan zao wanaziandikaje, n.k. sababu lazima wanazo na ni muhimu...

Chasha , Mrimi, Malila, Ericua Kimasha naomba maoni yenu kwa hili shukrani

Mkuu Consult kwanza nakupongeza sana kwa kunishauri nijifunze elimu ya ujasiria mali jambo ambalo nasisitiza linatekelezeka. Nitaendelea kujifunza maana ni mchakato usiokuwa na mwisho. Pili mimi hizo fani zote unazokisia siyo zangu. Mimi mtu wa kawaida tu ambae ninajibidiisha sana kutafuta maarifa kwa vitendo. Watu wote wanapaswa na wana haki kujua mambo ya utafutaji wa pesa maana ndiyo injini ya maisha yetu. Si wahasibu, wachumi au wataalamu wa masuala ya fedha pekee ndiyo wanahaki kuyajua haya, hii ni elimu ya kawaida kwa watu wote! Hapa hatuongelei kutengeneza rocketi tunasema mchanganuo wa biashara ni jambo la muhimu. Kupata ushauri wa kitaalamu ni muhimu, kujishughurisha ili kujifunza maarifa ya kuboresha shughuri zetu ni muhimu na hii haihitaji kuwa na elimu kubwa ili kuelezea hili.

Kuhusu wataalamu, hao ni wale watu wanolijua fika jambo ambalo unataka usaidiwe au ufundishwe. Hawa wataalamu wapo na ukiwatafuta utawapata tu. Hii inajumuisha pia watu wote waliofanikiwa kufanya jambo unalotaka kulijua au kulifanya hata kama ni watu wa mitaani tu, hatuongelei watu wenye vyeti pekee anaweza kuwa hata jirani yako aliefanikiwa sana kufanya jambo unalokusudia kulifanya. Hata wale wataalamu waliokaririshwa madarasani wanafaa kutumika iwapo hao ndiyo pekee wanaoweza kupatikana kwa wakati huo. Elewa kuwa unapokuwa huna options utachukua kile ambacho kinachopatikana kwa wakati huo. Hivi iwapo huyo mtu aliekaririshwa darasani akikuambia kwamba ukitaka kuongeza mapato ya biashara yako punguza matumizi au ongeza uzalishaji! Utakuwa hujaupata ujumbe? Huyo mtu akikueleza kuwa mbinu rahisi ya kukusanya mtaji ni kuweka akiba 10% ya kila income utakayo pata! Utampuuza tu kwa vile hanabiashara kama Bakhresa? Ndiyo maana niliandika huko nyuma kwamba hivi kama ukiikuta makala ya ujasiria mali gazetini hutaisoma ukaelimika? Ukikuta kitabu kinachoelekeza namna ya kuchanganua mpango wa biashara utadharau kwa vile hakijaandikwa na Mengi? Kama hawaandiki tukae tu?

Mkuu Consult ukisoma post yangu hapo nyuma ni kwamba ninawaheshimu sana wajasiliamali waliofika juu kwa kuhangaika wenyewe! Hao kama ni kupewa tuzo wangekuwa na mzigo wa ma Ph D, ninachokisema hapa ni kwamba mbinu wanazozitumia hao matajiri ndiyo hizo zilileteleza watu kuzifanyia utafiti, kuzitambua na kuanza kufundisha na wengine. Utaalamu ni kutoka kwa yeyote yule aliefika pale ambapo ungependa ufike, kama hawapo wa namna hiyo basi ingia kichwa kichwa kama kina Mengi na Bakhresa piga trial and error hadi utatoboza!!
 
Mkuu CHASHA mara nyingi na kwenye maandiko yako umekuwa ukikazana sana kusema ujasiriamali haufundishwi, na unakataa kata kata kwamba haijawahi kutokea na wala haitakuja kutokea. labda utusaidie ni utafiti gani uliofanya kuweza kuleta hiyo sheria.
Yanaweza kuwa ni maoni yako mkuu kutokana na uzoefu wako ila haiwezi kufanya kuwa ni sheria. kila kitu kinafundishwa ni swala la muda tu na matakwa ya mtu. hata upendo hufundishwa, kuna watu wamepata malezi mabovu na kujikuta hawana upendo ila kwa kurekebishwa wanajikuta wanajifunza kuishi vizuri na wenzao kwa upendo. unapochanganya mambo ni pale unapfananisha ujasiriamali na mahusiano ya kimapenzi, ni vitu viwili ambavyo havina ufanan wowote.
sote tunajua maamuzi mengi yanayofanyika kwenye mahusiano ya kimapenzi ni emotional ni mara chache sana yanakuwa rational. ila kwenye ujasiriamali na biahsara huwezi kwenda kwa emotional decisions.
 
kwa wote,
mada hii imeibua michango mingi na mizuri sana kwa wajasiriamali na wafanya biashara kwa ujumla. naomba niulize swali moja,
kama mtu ana utaalamu wa biashara alisomea ama aliojifunza na akaamua kuutumia huo utaalamu kama ndio biashara yake na akawasaidia watu wakanufaika na yeye akanufaika mpaka kufikia kuwa mshauri mkubwa, bado tunahitaji naye awe na biashara? huko kutoa ushauri wa kitaalamu si ndio biashara yake ambayo ametumia ujuzi wake kuikuza?
kama mtu ni mshauri wa masoko mpaka anakufikia wewe ama unamfikia yeye ina maana tayari alishatengeneza soko ama ameshaliona soko, sasa inabidi tena huyu mtu awe na banda la nyanya ili akushauri njia bora ya kuuza nyanya zako?
mimi nafikiri washauri wapimwe kwa uwezo wao wa kudeliver, kama mtu anakushauri kitu na kinafanya kazi hakuna haja ya kuhoji kwa nini yeye hakifanyi. huenda kupitia utaalamu huo ndio biashara anayopenda kuifanya kulingana na mazingira ama mpango wake wa maisha.
 
Mkuu @KUBOTA (na wengine wengi) shukran kwa maoni yako, lakini ningependa kuwajua hao wataalam ni wapi ? ? ? je ni yule aliyejufunza field/mtaani na kufanikisha kama vile Bakheressa au Mengi ? ? ? au ni yule aliyekaririshwa ndani ya vyumba vya madarasa tu na yeye hana hata mfano hai ? ?

Who is a Professional Entrepreneur ? ? juma mwenye degree tatu za biashara au Bakheressa na Mengi ? ?
Kimsingi utaalam maana yake ni kuwa na maarifa mengi ya kufanikisha mradi au jambo fulani,, Je unadhani huyo Bakheressa hana hayo maarifa ? kwa uhakika hao wafanyabiashara wana madegree zaidi ya tatu tatu hasa ukifanya assessment ya kitaalam utakuta yale yote yalioko madarasani wanayajua yote.

Vile vile kusoma kwa maana ya elimu ili kupata maarifa sio lazima uingie darasani ? mfano mzuri wa elimu ya field/mitaani ni Raisi wa S.A. Jacob Zuma ambaye wanadhani hata hiyo primary education hana...
mfano wa pili ni huyo Bakheressa na wengine wengi tu....

Chasha, Mrimi, Malila, @Ericus Kimasha naomba maoni yenu kwa hili shukrani

CONSULT
,
Binafsi sina jibu ila nimeweka mifano ambayo inatoa mtazamo wa jibu langu.

Watu wengi hufanya makosa kwa kudhani kuwa kwa mtu kutokwenda vidato au kufika chuo basi hajaelimika. Wengi tulio na fikra hizi tunatoa maana fupi mno ya "kuelimika" au kwa Kiingereza "to be educated." Hili neno "educated" linatokana na neno la kilatini "educo," maana yake "educe" (kamua, toa nje, pata, lete mbele). Mtu aliyeelimika siyo lazima awe yule aliye na shehena ya elimu ya jumla au elimu maalumu/mahsusi kupitia mfumo rasmi. Mtu aliyeelimika ni yule aliyetengeneza milango yake ya fahamu na anayeweza kuishughulisha kumpa chochote anachohitaji bila kuathiri haki na matakwa ya wengine.

Naomba kutumia mfano wa Henry Ford, mtu amabye ugunduzi wake umetembeza magari mengi zaidi juu ya ardhi kuliko mwingine yeyote.

Kuna watu wengi sana walikuwa wanasema Henry Ford hakusoma kwa sababu hakufika High-School kwa viwango vya nchi yake. Wakati wa vita ya kwanza ya dunia, gazeti la Chicago likachapisha tahariri ambayo miongoni mwa maelezo yake yalimshtumu, Henry Ford kwa kumuita "mtu asiye na elimu" Ford akapinga kwa nguvu zote kauli hii na akaenda mbali zaidi kufungua kesi dhidi ya gazeti hili kwa kumdhalilisha. Kesi ilipoletwa mahakamani, Mawakili wa gazeti wakaomba kuithibitishia mahakama na jopo la majaji kwa kumtaka Henry Ford aingie kizimbani. Mawakili wakamuuliza Ford maswali mbalimbali yote hayo yakilenga kuithibitishia mahakama kupitia majibu ya mlalamikaji mwenyewe kwamba kweli ni "Mbumbumbu"

Mahojiano ilikuwa kama ifuatavyo:
"Benedict Arnold alikuwa nani?" na "ni wanajeshi wangapi wa Jeshi la Uingereza walipelekwa Amerika kuzima mapigano mwaka 1776?" Katika kujibu swali la mwisho, Ford akasema "Sijui namba halisi ya Wanajeshi wa Uingereza waliopelekwa lakini nimesikia ilikuwa ni idadi kubwa kuliko wale wote waliorudi"

Baada ya mlolongo wa maswali, mwisho Ford akakinai na katika kujibu maswali yenye kuudhi, akamsonta mmoja wa Mawakili aliyeuliza swali huku akionyesha kukerwa, akamwambia; Kama kweli nikitaka kujibu maswali ya kipuuzi uliyouliza au maswali mengine uliyokuwa unauliza, ebu kwanza nikukumbushe jambo moja, nina mpangilio wa vitufe vya kubonyeza vya kielektroniki kwenye dawati la ofisi yangu, na kwa kubonyeza kitufe cha huduma ninayohitaji ninaweza kumuita msaidizi wangu anayeweza kujibu swali lolote ninalotaka kupata jibu lake kuhusiana na shughuli ambayo nimewekeza nguvu zangu zote (automobiles). Sasa nataka unijibu, kwa nini kichwani mwangu nijitwike maarifa ya jumla jumla (general knowledge) kwa minajiri ya kuwa na Uwezo wa kujibu maswali kama haya ilihali nimezungukwa na watu wanaoweza kunikamilisha kwa kunipatia maarifa ninayohitaji?

Mimi sijui tunapimaje kusoma na kuelimika. Lakini ningedhani kipimo kizuri ni jinsi elimu au maarifa uliyonayo yalivyokukomboa na kukuwezesha kuyamudu vema mazingira na maisha yako kwa ujumla. Kama kijana asiyejua "what is HTML nor Balance sheet" anamtengenezea ajira Programmer ambaye ni senior IT graduate na kisha anamuajiri B.Com (Accounting), CPA/ACCA amtunzie mahesabu. Na hawa waajiriwa wawili kutwa wanalia njaa na kutembeza vyeti, basi huyo mwenye Uwezo wa kuyatumia maarifa na elimu za wengine akayamudu maisha ndiye aliyeelimika. Wengine walisoma tu.
 
Mkuu Ericus Kimasha nakupongeza kwa post yako nzuri, kwa maoni yangu, nikichangia paragraph ya mwisho ya post yako iliyotangulia, mimi naona huyo mwenye uwezo wa kuyatumia maarifa na elimu za wengine akayamudu maisha ndiye aliyeelimika lakini pia na hao ambao huyo mwenye uwezo aliwatumia wakamtatulia matatizo yake kwa kutumia elimu zao wameelimika pia. Duniani tunaishi kwa kutegemeana na asitokee mtu upande mmoja akajiona yeye mjanja zaidi ajipe yeye uerevu kuliko wanaomfanikishia mambo asiyoyaweza yeye. Wasomi ambao hawajaelimika ni hao wanaoshinda njaa na vyeti mkononi mwisho wasiku wao haviwasaidii na jamii haifaidiki na elimu yao.
 
Mkuu CHASHA mara nyingi na kwenye maandiko yako umekuwa ukikazana sana kusema ujasiriamali haufundishwi, na unakataa kata kata kwamba haijawahi kutokea na wala haitakuja kutokea. labda utusaidie ni utafiti gani uliofanya kuweza kuleta hiyo sheria.
Yanaweza kuwa ni maoni yako mkuu kutokana na uzoefu wako ila haiwezi kufanya kuwa ni sheria. kila kitu kinafundishwa ni swala la muda tu na matakwa ya mtu. hata upendo hufundishwa, kuna watu wamepata malezi mabovu na kujikuta hawana upendo ila kwa kurekebishwa wanajikuta wanajifunza kuishi vizuri na wenzao kwa upendo. unapochanganya mambo ni pale unapfananisha ujasiriamali na mahusiano ya kimapenzi, ni vitu viwili ambavyo havina ufanan wowote.
sote tunajua maamuzi mengi yanayofanyika kwenye mahusiano ya kimapenzi ni emotional ni mara chache sana yanakuwa rational. ila kwenye ujasiriamali na biahsara huwezi kwenda kwa emotional decisions.

Mkuu hongera sana kwa maswali yako, watu wengi humu tunanufaika na ushauri na wengi wetu tunachanganya na za kwetu kichwani pia nadhani huo mjadala kuwa ujasiriamali haufundikishi na debate kubwa sana sshv nadhani hata chasha ameitoa kwenye mtandao nimekuwekea baadhi tu za address hapa na wewe uzipitie nadhani utapata uwelewa zaidi kama kawaida penye debate jibu ni mtazamo wako tu yawezekana wewe ni wale wanaosema kuwa "ujasiriamali unafundishika"

Why Entrepreneurship Can't (and Shouldn't) Be Taught in School | Inc.com
Can You Learn to be an Entrepreneur? [ANSWERS] - Teach A CEO
Founder Institute
Entrepreneurship can't be taught in schools, but some education helps | SmartPlanet
 
kwa wote,
mada hii imeibua michango mingi na mizuri sana kwa wajasiriamali na wafanya biashara kwa ujumla. naomba niulize swali moja,
kama mtu ana utaalamu wa biashara alisomea ama aliojifunza na akaamua kuutumia huo utaalamu kama ndio biashara yake na akawasaidia watu wakanufaika na yeye akanufaika mpaka kufikia kuwa mshauri mkubwa, bado tunahitaji naye awe na biashara? huko kutoa ushauri wa kitaalamu si ndio biashara yake ambayo ametumia ujuzi wake kuikuza?
kama mtu ni mshauri wa masoko mpaka anakufikia wewe ama unamfikia yeye ina maana tayari alishatengeneza soko ama ameshaliona soko, sasa inabidi tena huyu mtu awe na banda la nyanya ili akushauri njia bora ya kuuza nyanya zako?
mimi nafikiri washauri wapimwe kwa uwezo wao wa kudeliver, kama mtu anakushauri kitu na kinafanya kazi hakuna haja ya kuhoji kwa nini yeye hakifanyi. huenda kupitia utaalamu huo ndio biashara anayopenda kuifanya kulingana na mazingira ama mpango wake wa maisha.

Mkuu Kinacho Fundishwa ni Busiess Skills, Na tofautisha kati y hivyo vitu viwili, Business slls ndo inayo fundishwa na si Ujasirimali, Huwezi fundisha mtu Ujasirimali mkuu hata siku Moja,

So naomba kwanza utofautise kati ya Business Skills na Entrprenership,

WAKUU KWA YOYOTE ATAKAYE NI JIBU HAYA, NI WAPI, CHUO KIPI, SEMINA IPI, KONGAMANO IPI, MASHAURI WA BIASHARA YUPU ULISHA KUTA VIFUTAVYO VINAFUNDISHWA

- Maswala ya how to take Risk
- How to caliculate hiyo Risk
-Ishu za Comitement
-Confidence

Commitment ndo Driving force ya Mjasirimali,wakuu, a huwezi fundishwa Commtment, ni commitement nd in ku driive kweny haya
1. Kuto kata tamaa kabisa hata kama umefeli mara ngapi,
2. Kufanya kazi kwa muda mrefu ana hata 24 hours
3. Kuwa na ubunifu
4. Kutelekeza mambo mengine yote na kudill n moja tu,

SO HAYA HAYAFUNDISHWI MKUU, TUACHEKUCHANGANYA MADESA,

VYUO VYOTE NA HATA MIMI CHUO NILICHO SOMA TULIFUNDISWA HAYA
1- Business planing
2. Financila planing
3. Maswala ya marketing
4. ishu zote za pricing, promotion na kazalika
5. ishu z cost

Kama kuna mtu anajua popote pale iwe Tanzania au hata nje Chuo kinacho fundishaishu za Commitement, onfidance, Sprit kwa ujumala wake, na mengine aniambie nitaenda kusoma

KAMA ULISHA SIKIA WATU WAKO BISE KUFUNDISHA WATU SIJUI UJASIRIMALI LKINI HAWANA HATA KIBDANDA CH KUCHJIA SIMU, AU KAMA ULISHA SIKIA MTU ANA MASTERS YA ENTREPRENERSHI ILA YUKO ANATAFUTA KAZI, KAMA ULISA SIKIA KUN MTU NI phd holder wa Entreprenership ila anaogopa biashara kama ukoma ni kwa sababu ya haya hapa chini
- Maswala ya how to take Risk

- How to caliculate hiyo Risk
-Ishu za Comitement
-Confidence

MWISHO TUACHE KABISA KUCHANGANYA KATI YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI HAPO NDO TUNAPO KOSEA NA KUKUZA SANA HUU MJADALA

Hapo kwenye Red,Mkuu wakati mimi nasoma haya yanayo itwa masomo ya Ujasirimali, tuliwahi kumuuliza mwalimu mbonaunatufudisha lakini huna hata Kibanda? Jibu alituambia Ujasirimali si ishu ya KITOTO.

Na mimi ninacho taka Kama wewe ni Mshauri wa biashar basi uwe na SHAMBA DARASA LAKO, ila kama nilivyo sema wakuu THEORY NA PRACTICAL MARA ZOTE HAZIOANI

Na Tutambue kwamba Elimu inayo tolewa nawashari wa Biashara ni elimu ya Biashar na si Elmu ya UJASIRIAMALI, Tatizo tunapotoshwa na wana siasa na sisi tunachukulia yale wanayo tamka wao

Mkuu hongera sana kwa maswali yako, watu wengi humu tunanufaika na ushauri na wengi wetu tunachanganya na za kwetu kichwani pia nadhani huo mjadala kuwa ujasiriamali haufundikishi na debate kubwa sana sshv nadhani hata chasha ameitoa kwenye mtandao nimekuwekea baadhi tu za address hapa na wewe uzipitie nadhani utapata uwelewa zaidi kama kawaida penye debate jibu ni mtazamo wako tu yawezekana wewe ni wale wanaosema kuwa "ujasiriamali unafundishika"

Why Entrepreneurship Can't (and Shouldn't) Be Taught in School | Inc.com
Can You Learn to be an Entrepreneur? [ANSWERS] - Teach A CEO
Founder Institute
Entrepreneurship can't be taught in schools, but some education helps | SmartPlanet

Mkuu hata Huko kwli nisha pita na ukuta Mijadala mikubwa sana, Ila niseme ukweli kuna Time tulikuwa tunatoa semina zakufa mtu za Ujasirimali, nilikuwa na shrika fulani, Tulikuwa tunafundisha kiulkweli, lLA CHA AJABU KILA KIPINDI CH EVELUTION KIKIFIKA, KUNA KUW HAKUNA CHANGES ZOZOTE ZILE, na hapo nilianza na mimi kuamni kwamba huwezi fundisha mtu Ujasirimali, ila unaweza mpatia elimu ya biashara,

WATU WANACHANGANY MAMBO MAWILI HAPA, ELMU YA BIASHARA NA UJASIRIMALI, Hivi ni vitu viwii tofauti kabisa, sasa wengi wetu tunaichanganya pamoja that is why ubishi unakuwa mwingi sana

Katika kila jambo ambalo binadamu amewahi kulifanya likang'ara wamewahi kutokea binadamu wakatengenza kitu kingine kukinzana na kilichopo. Kukiwa na positive watatengeneza negative, always lazima wawepo watu wa kunegate lolote utakaloibua, ndiyo maana kuna virus kwenye computor! Watu waligundua kutengeneza computor wengine wakatengenza virus kuhujumu computor na programme zake. Wapo watu daima ni kwenda kinyume na ukweli! Usipokuwa na msimamo na kuiamini akili yako ni rahisi sana kuwa corrupted! Kuna watu unaweza kudhani ni waelewa na waerevu wa mambo kumbe ni watu wenye kuchanganya mambo na kunywesha sumu watu wengine! Mwenye akili timamu tumia akili yako kujua ukweli wa jambo, asitokee mtu kukupandikizia kichwani kwako kwamba yeye kasoma sana, sijui kafanya kazi hii wala ile, kwamba ni yeye tu anajua ukweli wengine hawajui! Watanzania mtakaosoma hapa kazaneni kutafuta maarifa, watu wengi wanafanikiwa kwa kujifunza, kila jambo linafundishika, kama wewe umevutiw kufanyaujasilia mali jifunze wanayofanya waliofanikiwa. Hizi hadithi zingine ni kupimana ujuaji usiokuwa na tija kusaidia watu.
 
Miaka ya hivi karibuni, katika jitihada za kuhamisha ujasiriamali, uanzishaji wa Biashara na utengenezaji wa ajira kwenye sekta binafsi kumekuwa na msisitizo wa wajasiriamali kuandika michangamanuo/mipango ya Biashara. Kuna wakati wajasiriamali na wajasiriamali-watarajiwa hufikiri kuwa michangamanuo hii ndiyo suluhisho la vikwazo vyao vyote na ufunguo wa mafanikio katika biashara. Leo nataka kutumia mifano miwili kuleta mada ili tujadili kama kweli mchangamanuo/mpango wa Biashara ndiyo kigezo cha mafanikio katika Biashara.

Nitatumia hadithi za wafanyabiashara wawili. Kwa bahati nzuri wote ni wazawa wa Tanzania na hivyo wanafahamika vema na wengi wetu. Nitamtumia Mzee Reginard Mengi mmiliki wa vyombo vya habari vya habari na Mwanahisa Mkuu wa Bonite Bottlers; vyote vikiwa chini ya Kampuni Tanzu ya IPP. Katika mfano wetu nitatumia maji ya Kilimanjaro yaliyo chini ya Bonite Bottlers Ltd. Na katika mfano wa pili, nitamhusisha Mzee Salim Bakheresa. Naamini sihitaji kumsemea sana huyu kwa kuwa, kwa nadra sana mtu aliye Tanzania atapitisha siku bila kutumia bidhaa ya Azam. Asipokula bidhaa ya Azam kama kitafunwa, atailamba kama ice cream na asipoilamba atainywa kama maji au soda. Lakini katika mada hii nitatumia uanzishwaji wa Kiwanda cha vinywaji vya soda za Azam Cola.

Hadithi zinadai kuwa Mzee Mengi baada ya kuona fursa ya kuuza maji safi ya kunywa kwenye chupa, aliamuua kutengeneza mchangamanuo ili umsaidie kuzishawishi taasisi za fedha katika kupata mkopo. Lakini kila alipojaribu kuutembeza mchangamanuo huu, alikwama na mara alipoaga ofisi za hizi Taasisi, Mameneja waliitana, wakamcheka na kumdhihaki kwa kusema “huyu Bwana amechanganyikiwa. Maji atamuuzia nani?”. Inasemekana hata baada ya kupata mbadala wa mtaji na kuanzisha kiwanda, Mzee Mengi alipomualika Mwalimu Nyerere katika uzinduzi wa maji ya Kilimanjaro alisema “Wewe Mengi ubepari unakupeleka pabaya. Unataka kuwauzia ndugu zako maji?”

Hadithi ya pili inamuhusu Mzee Bakheresa na uanzishwaji wa Kiwanda chake kilichopo Mbagala Maji-Matitu. Kiwanda hiki ndicho kinachozalisha Azam Cola. Inasemekana kabla ya kuanzisha kiwanda hiki, wataalamu walipewa kazi ya kufanya upembuzi yakinifu na kuandaa mchangamanuo. Baada ya kutimiza kazi yao waliiwakilisha kwa mteja na kumtaarifu kuwa hiyo Biashara ingehitaji mtaji mkubwa, matishio (risks) yake yangekuwa makubwa wakati marejesho yalikuwa hasi (negative returns). Baada ya taarifa hii inasemekana Mzee bakheresa aliomba kitabu cha Hundi na kusaini hundi yenye thamani ya shillingi bilioni tano na kuwaamrisha wataalamu pamoja na timu yake ya uongozi kuanzisha hicho kiwanda haraka sana.

Katika mfano wa kwanza tumeona jinsi Mzee Mengi alivyokuwa na mchangamanuo wa Biashara mzuri lakini hukakosa ladha mbele ya taasisi za kifedha na mwisho ukakataliwa. Lakini pamoja na kukataliwa Mzee Mengi akaweza kuanzisha kiwanda cha maji ya Kilimanjaro yawezekana kwa kutumia mtaji wake mwenyewe. Matokeo ya mchangamanuo wa biashara iliyokataliwa ni bidhaa ya maji ya Kilimjanjaro, maji ambayo sasa yamenunuliwa na nembo ya kimataifa (Coca Cola) na kuzishinda kwa mbali bidhaa nyingine za kimataifa kama DASANI. Vile vile katika mfano wa pili tumeona Wataalamu wakihitimisha kazi ya upembuzi na uandaaji wa mchangamanuo wa Biashara kwa kumshauri Mzee Bakheresa kutoanzisha kiwanda cha vinywaji baridi. Lakini kinyume chake Mzee Bakheresa akakaidi ushauri na kuanzisha vinywaji vya Azam Cola ambayo leo hii ni mshindani mkuu wa vinywaji vya Coca Cola.

Baada ya maelezo haya na mifano hii ningependa tujadili swali moja kuu:

Je, kuna umuhimu wa kuandika Mchangamanuo/Mpango wa Biashara?

Bonus reference:Great Businesses Don't Start With a Plan - Anthony Tjan - Harvard Business Review

[-]<>[-]
[-]<>[-][-]<>[-] [-]<>[-] [-]<>[-][-]<>[-]

Uchochezi wa Mada:
Mkuu DASANI hiyo hiyo si inatengenezwa na coca cola ?...ni kama umefananisha fanta passion na fanta orange mkuu..ladba useme kiu maarufu kilimanjaro ni maarufu tanzania..ila mbele(Western world) ni DASANI...au ulikua unamaanisha nin hapo mkuu..!!
 
Umeshindwa kujibu hoja umeingia kwingine, wewe ndo unatafuta sifa hapa, mim nitafute sifa ili iwe vipi? Jibu hoja na watu wako hapa kujifuna, ishu za sijui kasoma zinaingia vipi hapa?

Ninaodika ni nacho amini mimi, siko hapa kumharibia mtu, na kama ni hii kazi hata mimi naifanya sana hadi leo na kesho ila kuifanya hakubadili ukweli

Na kama huwezi jibu hoja kaa kimya make naona mjadala umebadilika kuwa ni Hasira

AU MLETA MAADA ONGEA NA MOD WAFUNGE,

Make umeanza kuwa wa Majungu

Katika kila jambo ambalo binadamu amewahi kulifanya likang'ara wamewahi kutokea binadamu wakatengenza kitu kingine kukinzana na kilichopo. Kukiwa na positive watatengeneza negative, always lazima wawepo watu wa kunegate lolote utakaloibua, ndiyo maana kuna virus kwenye computor! Watu waligundua kutengeneza computor wengine wakatengenza virus kuhujumu computor na programme zake. Wapo watu daima ni kwenda kinyume na ukweli! Usipokuwa na msimamo na kuiamini akili yako ni rahisi sana kuwa corrupted! Kuna watu unaweza kudhani ni waelewa na waerevu wa mambo kumbe ni watu wenye kuchanganya mambo na kunywesha sumu watu wengine! Mwenye akili timamu tumia akili yako kujua ukweli wa jambo, asitokee mtu kukupandikizia kichwani kwako kwamba yeye kasoma sana, sijui kafanya kazi hii wala ile, kwamba ni yeye tu anajua ukweli wengine hawajui! Watanzania mtakaosoma hapa kazaneni kutafuta maarifa, watu wengi wanafanikiwa kwa kujifunza, kila jambo linafundishika, kama wewe umevutiw kufanyaujasilia mali jifunze wanayofanya waliofanikiwa. Hizi hadithi zingine ni kupimana ujuaji usiokuwa na tija kusaidia watu.
 
Na kuna watu wanaingia kichwa kichwa kuchangia ili muradi.

Hapa hatuzungumzii elimu ya biashara na wal hatuzungumzii elimu ya kwenda either kufundishwa kufuga kuku au bata,

Hapa tunazungumzia Ujasiriamali na tunazani ukiwa my be mfuga kuku basi wewe ni mjasiriamali, mimi nafuga kuku na ishu zingine ila sina sifa ya kuitwa mjasiriamali.

TUJADILO KWA HOJA NA SIO HASIRA
 
Mkuu DASANI hiyo hiyo si inatengenezwa na coca cola ?...ni kama umefananisha fanta passion na fanta orange mkuu..ladba useme kiu maarufu kilimanjaro ni maarufu tanzania..ila mbele(Western world) ni DASANI...au ulikua unamaanisha nin hapo mkuu..!!
Kilimanjaro-drinking-water.png

Lyamber,
Hauko mbali na taarifa japo ukweli ni kwamba Maji ya Kilimanjaro awali hayakuwa chini ya Registered Trade Mark ya Coca Cola bali yalinunuliwa (acquired) miaka ya 2003 baada ya DASANI kushindwa kabisa kupata market entry kwenye soko la Tanzania. Kwanza kulikuwa na tatizo la kiufundi ambalo maji ya DASANI yalipoingizwa sokoni yalikuwa na Chlorine nyingi hilo likawa kosa la kwanza na kubwa lililochangia kushindwa kukubalika. Kuna kipindi iliwagharimu kufanya "recall from the market" kuondoa mzigo wa DASANI na hii ikachangia kuharibu sura na kuaminika kwa maji haya. Na kama ilivyo kawaida ya hizi "Multinational Businesses" If they can't beat you, they acquire you kupunguza gharama za kushindana na wewe ili waendelee kufaidikia na wigo fulani wa uhuru katika ushindani wa masoko. Na ndiyo janja ile ile Coca Cola wamefanya kwa Azam Cola. Kama utakumbuka Coca Cola wamehaha sana kumfunika Azam Cola, wametumia mpaka mbinu za Kimahaka kumshitaki Azam kwa kutumia neno "cola" kwenye vinywaji vyake lakini mwisho wa yote, baada ya kushindwa kote huko ndo wakamua kuingiza sokoni kwa nguvu zote Coca Cola take-away product lines.

Fuatilia vyanzo hivi vitakupa mwanga: Azam cola, Ni kweli Azam Cola imepigwa marufuku

Ni kweli nje ya Tanzania na hasa nje ya Africa DASANI ni chapa inayokubalika na inauza. Lakini leo hii hata ukipewa dau uitafute DASANI jijini Dar es Salaam hutoipata. High end markets zote zimeshikwa na Kilimanjaro ambayo kwa sasa ni product ya Coca Cola na hivyo kuakisi mfano wako wa kufananisha Fanta Orange na Fanta Passion!
 
Last edited by a moderator:

Daaaj mkuu nafurahi sana kuona mtanzania mwenzangu uko well informed kiasi hiki aisee big up kaka..kwa kweli maji ya dasani yalivyoingiaga yalikuaga na ladha tofauti kidogo..nimesema hivyoo maana kuna siku miaka ya nyuma sana nilichekigi show inaitwa MTV Cribs niishangaa sana kuona jamaa anafungua fridge halafu amejaza DASANi kibao nikajua tu kwamba hiyo ni label ya mbele..ngoja nisome hizo habari za coca cola na azam maana nilizitafutaga lakini sikuzipata..over..!!
 
Mkuu Kinacho Fundishwa ni Busiess Skills, Na tofautisha kati y hivyo vitu viwili, Business slls ndo inayo fundishwa na si Ujasirimali, Huwezi fundisha mtu Ujasirimali mkuu hata siku Moja,

So naomba kwanza utofautise kati ya Business Skills na Entrprenership,

WAKUU KWA YOYOTE ATAKAYE NI JIBU HAYA, NI WAPI, CHUO KIPI, SEMINA IPI, KONGAMANO IPI, MASHAURI WA BIASHARA YUPU ULISHA KUTA VIFUTAVYO VINAFUNDISHWA

- Maswala ya how to take Risk
- How to caliculate hiyo Risk
-Ishu za Comitement
-Confidence

Commitment ndo Driving force ya Mjasirimali,wakuu, a huwezi fundishwa Commtment, ni commitement nd in ku driive kweny haya
1. Kuto kata tamaa kabisa hata kama umefeli mara ngapi,
2. Kufanya kazi kwa muda mrefu ana hata 24 hours
3. Kuwa na ubunifu
4. Kutelekeza mambo mengine yote na kudill n moja tu,

SO HAYA HAYAFUNDISHWI MKUU, TUACHEKUCHANGANYA MADESA,

VYUO VYOTE NA HATA MIMI CHUO NILICHO SOMA TULIFUNDISWA HAYA
1- Business planing
2. Financila planing
3. Maswala ya marketing
4. ishu zote za pricing, promotion na kazalika
5. ishu z cost

Kama kuna mtu anajua popote pale iwe Tanzania au hata nje Chuo kinacho fundishaishu za Commitement, onfidance, Sprit kwa ujumala wake, na mengine aniambie nitaenda kusoma

KAMA ULISHA SIKIA WATU WAKO BISE KUFUNDISHA WATU SIJUI UJASIRIMALI LKINI HAWANA HATA KIBDANDA CH KUCHJIA SIMU, AU KAMA ULISHA SIKIA MTU ANA MASTERS YA ENTREPRENERSHI ILA YUKO ANATAFUTA KAZI, KAMA ULISA SIKIA KUN MTU NI phd holder wa Entreprenership ila anaogopa biashara kama ukoma ni kwa sababu ya haya hapa chini
- Maswala ya how to take Risk

- How to caliculate hiyo Risk
-Ishu za Comitement
-Confidence

MWISHO TUACHE KABISA KUCHANGANYA KATI YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI HAPO NDO TUNAPO KOSEA NA KUKUZA SANA HUU MJADALA

mkuu CHASHA, asante sana kwa ufafanuzi ulioutoa, na pia naomba pamoja na wachangiaji wote tusiweke ubishi tu hapa kama mashindano bali tutoe hoja ili kila mtu ajifunze.
sasa mkuu chasha naomba turudi ground zero, naposema kila kitu kinafundishika kwanza naomba tuelewane simaanishi kufundishwa darasani tu. kunamwalimu mzuri sana ambae hakuna anayeweza kumkwepa ambaye ni EXPERIENCE mambo yote uliyzungumzia ya risk taking na mengineyo wengi wamejifunza through experience tena the hard way. hakuna mtu aliezaliwa akijua kutake risk, hakuna DNA ya ujasiriamali kwenye mwili wa binadamu. Mazingira tuliyokulia ama tunayoishi yana mchango mkubwa sana kwa jinsi maisha yetu yalivyo. Ndio maana nasema kila kitu kinafundishika ni utayari wa mtu kutaka sana kukifanya hicho kitu na kukubali ku learn through the hard way.
unapokataa ujasiriamali haufundishiki kata kata ni ku-undermine human mind capacity. watu wana uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo makubwa sana. tofauti ni uzoefu na mazingira.
kama umefundisha watu na hawakufundishika sio kosa lao ila ni njia unayofundishia ndio imeshindwa kutoa majibu mazuri. kama unatoa kozi hizo hebu kaa chini utafute mbinu nyingine ya kufundishia ambayo itakuwa shirikishi zaidi na kutambua uwezo wa unaowafundiaha kama hutoshangazwa na majibu mazuri utakayoyapata. Tatizo linakuja pale mtu anapotaka kujifunza ujasiriamali ndani ya wiki moja ama mwezi mmoja.
na unapozungumzia degree za ujasiriamali zinazotolewa vyuo vikuu hizo ndio hopeless kabisa sote tunajua mfumo wa vyuo vikuu vyetu, hata anaesomea uinjinia anaandaliwa kwenda kuwa masimamizi, hivyo hatuwezi kupata majibu mazuri kwenye kozi za ujasiriamali kwa kupitia mfumo mbovu na ulioshindwa.

Yes,
1.description of the business
2.budgeting
3.SWOT ANALYSIS,(STRENGTH,WEAKNESSES,OPPORTUNITIES,,THREAT)
4.finances seeking

Hivi hapo juu NI baadhi ya vitu muhimu kibiashara ambavyo utavikuta katika michanganuo ya biashara.
Maelezo juu ya biahshara husika hutoa taswira ya biashara sokoni,huonyesha wateja walengwa na washindaNi sokoni, hii pekee ni nyenzo katika kuendesha biashara kwa faida.
Budget huainisha kiasi cha fedha kinachohitajika kuanzisha biashara pamoja na makadilio ya mapato ambayo huhitaji utafitti.
SWOT analyses huonyesha nafasi ya biashara yako sokoni(Market share)
 
Mkuu ni kweli ila bado niko pale pale. Kuna vitu vinafundishika unaweza soma jinsi ya kutafuta masoko, kuuza, kutangaza, kukirimu wateja, kupunguza gharama za uzalishaji na kazalika, mkuu kujifunza haya sio sehemu ya ujasiriamali,
BADO NASISITIZA TUNACHANGANYA VITU VIWILI HAPA,KUFANYA BIASHARA NA UJASIRIAMALI

mkuu CHASHA, asante sana kwa ufafanuzi ulioutoa, na pia naomba pamoja na wachangiaji wote tusiweke ubishi tu hapa kama mashindano bali tutoe hoja ili kila mtu ajifunze.
sasa mkuu chasha naomba turudi ground zero, naposema kila kitu kinafundishika kwanza naomba tuelewane simaanishi kufundishwa darasani tu. kunamwalimu mzuri sana ambae hakuna anayeweza kumkwepa ambaye ni EXPERIENCE mambo yote uliyzungumzia ya risk taking na mengineyo wengi wamejifunza through experience tena the hard way. hakuna mtu aliezaliwa akijua kutake risk, hakuna DNA ya ujasiriamali kwenye mwili wa binadamu. Mazingira tuliyokulia ama tunayoishi yana mchango mkubwa sana kwa jinsi maisha yetu yalivyo. Ndio maana nasema kila kitu kinafundishika ni utayari wa mtu kutaka sana kukifanya hicho kitu na kukubali ku learn through the hard way.
unapokataa ujasiriamali haufundishiki kata kata ni ku-undermine human mind capacity. watu wana uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo makubwa sana. tofauti ni uzoefu na mazingira.
kama umefundisha watu na hawakufundishika sio kosa lao ila ni njia unayofundishia ndio imeshindwa kutoa majibu mazuri. kama unatoa kozi hizo hebu kaa chini utafute mbinu nyingine ya kufundishia ambayo itakuwa shirikishi zaidi na kutambua uwezo wa unaowafundiaha kama hutoshangazwa na majibu mazuri utakayoyapata. Tatizo linakuja pale mtu anapotaka kujifunza ujasiriamali ndani ya wiki moja ama mwezi mmoja.
na unapozungumzia degree za ujasiriamali zinazotolewa vyuo vikuu hizo ndio hopeless kabisa sote tunajua mfumo wa vyuo vikuu vyetu, hata anaesomea uinjinia anaandaliwa kwenda kuwa masimamizi, hivyo hatuwezi kupata majibu mazuri kwenye kozi za ujasiriamali kwa kupitia mfumo mbovu na ulioshindwa.

mkuu CHASHA, asante sana kwa ufafanuzi ulioutoa, na pia naomba pamoja na wachangiaji wote tusiweke ubishi tu hapa kama mashindano bali tutoe hoja ili kila mtu ajifunze.
sasa mkuu chasha naomba turudi ground zero, naposema kila kitu kinafundishika kwanza naomba tuelewane simaanishi kufundishwa darasani tu. kunamwalimu mzuri sana ambae hakuna anayeweza kumkwepa ambaye ni EXPERIENCE mambo yote uliyzungumzia ya risk taking na mengineyo wengi wamejifunza through experience tena the hard way. hakuna mtu aliezaliwa akijua kutake risk, hakuna DNA ya ujasiriamali kwenye mwili wa binadamu. Mazingira tuliyokulia ama tunayoishi yana mchango mkubwa sana kwa jinsi maisha yetu yalivyo. Ndio maana nasema kila kitu kinafundishika ni utayari wa mtu kutaka sana kukifanya hicho kitu na kukubali ku learn through the hard way.
unapokataa ujasiriamali haufundishiki kata kata ni ku-undermine human mind capacity. watu wana uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo makubwa sana. tofauti ni uzoefu na mazingira.
kama umefundisha watu na hawakufundishika sio kosa lao ila ni njia unayofundishia ndio imeshindwa kutoa majibu mazuri. kama unatoa kozi hizo hebu kaa chini utafute mbinu nyingine ya kufundishia ambayo itakuwa shirikishi zaidi na kutambua uwezo wa unaowafundiaha kama hutoshangazwa na majibu mazuri utakayoyapata. Tatizo linakuja pale mtu anapotaka kujifunza ujasiriamali ndani ya wiki moja ama mwezi mmoja.
na unapozungumzia degree za ujasiriamali zinazotolewa vyuo vikuu hizo ndio hopeless kabisa sote tunajua mfumo wa vyuo vikuu vyetu, hata anaesomea uinjinia anaandaliwa kwenda kuwa masimamizi, hivyo hatuwezi kupata majibu mazuri kwenye kozi za ujasiriamali kwa kupitia mfumo mbovu na ulioshindwa.

Mkuu Malikita Amani asante sana michango yako bombaaaa !
 
Back
Top Bottom