Je, kuna utofauti wa kufikiri kati ya Mwafrika na watu weupe?

Mnaotupia picha zinazoonesha hao wazungu Wa JF mnataka tuelewe nini??

Jee hiyo picha ingekuwa na wazungu wengi na waafrika watatu mngeileta kwenye mada hii!!?
 
Huenda tuko sawa ila jamaa waliwahi kujipata aisee.

Wamehustle toka miaka hiyo sisi na kina chifu mangungu hata hatujui kama dunia ina watu zaidi yetu.

Wao wakatugundua sisi 😂😂 ajabu hii.. wakagundua milima, maziwa na mabonde yetu ajabu tena hii...

Jamaa waliwahi kujipata, wale walioenda nao sawa vyedi ndo wametoboa nao kama wajapani, waliojitwist na kuhustle kivyao na wakatoboa pia ni kama wachina.

Ila sisi walituganda kishenzi mpaka kesho, hatujitambui, tuna tamaa, tunatamani kila kitu chao.
 
Upumbavu mzigo mzito sasa umejibu nn
 

Afrika tunafikiri kimaskini, hatuna teknolojia bora na mifumo zetu za elimu pia ni mibovu hivyo zinatudidimiza zaidi ila Wazungu/waasia wana wanafikiria kitajiri, wana teknolojia na elimu bora.
 
Hata South Africa bila watu weupe leo hii SA ingekua kama Burundi, ukitaka kuamini hilo angalia crime rate ya SA, kesi za rushwa kwa viongozi n.k..
 
Mfano mzuri kwenye mpira,timu za Africa zikipata nafasi tano za kufunga wanafunga moja,wengine wakipata nafasi tano goli ni tatu au nne.
 
Kubwa! Mtu mweupe hawezi kukaa na mafuriko hadi ikulu kwa miaka 60 wala kuishi bila umeme nusu karne bila kupata solution
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…