Uchaguzi 2020 Je, kuna uwezekano kutangaza nia kugombea Urais kupitia CHADEMA kwa baadhi, kunatumika kama kichaka cha kujifichia aibu ya kushindwa ubunge?.

Hawezi kuwacha upambe mpaka kaka yake atoke altare maana siku hizi ni yesu wa lumumba
nijibu haya maswali;
1. Kutia nia urais kunawanyima kugombea ubunge?
2. Unasema watapata aibu,je hata duniani walizaliwa kuja kuwa wabunge?hakuna maisha bila ubunge?
Bonus: utaacha lini upambe?
 
Watashindwa kwa kukubaliwa kwa CCM au kwa mabavu mapya ya CCM yakishirikisha dola? Nadhani Rafiki yangu unakengeuka sasa! Yellow isn't blue, I think you certainly know that! Just call a spade, spade not another version of the spoon!!
Huyo jamaa ni mnafiki wa kiwango cha SGR!!
 
Pascal amekumbuka shuka wakati kusha kucha, kayachezea maisha kwenye ujana sasa anataka awe dc
Yaani andiko lote limejaa kudhani kuudhani! Ungesema wametia nia wengi kwakua wameshaona kuwa mgombea wa CCm atakua mwepesi...hili ni mojawapo ya maandiko dhaifu na yenye kujipendekeza kuliko yote
 
Nianze kwa kusema Mkuu Mayala Akili yako ni kubwa sana haistaili kudharilishwa kwa bandiko la kijinga kama hili!... Mosi,,kushindwa UBUNGE sio swala la aibu ni swala la demokarasia ni lazima awepo mashindi na ndo maana watu wanashindana hapo Aibu inatoka wapi unless hujui maana ya aibu kitu ambacho sikiamini.. Pili kutangaza nia ya kuomba Ridhaa ya kugombea Nafasi ya Urais ,,haiwazuii wao kugombea Nafasi ya UBUNGE Iwapo chama hakita wapa Ridhaa ya kugombea Urais,rejea hitimisho la mh Msigwa alipo tangaza nia,, Tatu Upinzani sio Lege Lege kama ungelikua Lege Lege wewe na Mataga wenzio msinge uzingatia na wala usinge leta uzi huu,,( mge waacha wafu wawazike wafu wenzao) Uzi huu ni uthibitisho tosha kua mna hofu na upinzani ambao mmeutia kitanzini kwa Miaka 4,,mmetumia hila kulegeza ,,, ,.R.I.P ALPHONCE MAWAZO.,, BE STRONG Antpas Lissu,,Get WELL SOON MBOWE,,,Uwe na Amani popote ulipo Ben Sanane,, And Justice. for Mdude Nyangali...
 
Hata jiwe analijua hilo na kwa sasa kinacho fanyika ni kutimiza ule msemo wa mwiba unapo ingilia ndiyo hapo hapo unapotokea, yaani yesu alivyo ingia madarakani ndiyo maana kunamfanya kuuogopa sana upinzani
Hawa wapumbavu jeuri yao iko hapa.
Hata hao wanaowanunua wanawaaminisha kuwa mbeleko hii itawabeba hata kama wapiga kura wakiwakataa. Uchaguzi huru na wa haki CCM tunawapiga saa nne asubuhi tu.View attachment 1479892
 
Acha kudhalilisha wenzio hivyo. Kwani lazima wote wawe Wabunge? Mbona Watanzania wengi tu tunaendesha maisha nje Bunge kwa raha zetu bila vipaza sauti? Stop belittling fellow human beings like this!
Wanabodi,

Naomba kuanza na angalizo:
Hili ni bandiko la swali, kuhusu ideas ya watangaza nia wa urais Chadema. Kama una majibu, karibu uchangie. Nimeanza na angalizo hili kwasababu humu jf tumevamiwa na ma simple minds ambao kazi yao ni kujadili watu badala ya kujadili ideas!. Kumezuka mtindo wa watu kutokujadili hoja iliyo mezani na badala yake kumjadili mtoa hoja!. Tujifunze kujadili mada iliyo mezani na sio kumjadili mtoa mada.

Kuelekea uchaguzi wa 2020, imetabiriwa kuwa kwa huku Tanzania Bara, Wabunge wote wa upinzani hata wakigombea tena, wataishia kupigwa chini na CCM, kufuatia kukubalika kwa CCM kwa kazi kubwa na nzuri ya kuwaletea maendeleo Watanzania inayofanywa na rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano. Imetabiriwa CCM itashinda uchaguzi Mkuu ujao kwa ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9%.

Hivyo ili kuepuka kushindwa kwa aibu, jee kunauwezekano, huku kutangaza nia ya kuwania kuteuliwa na vyama kugombea urais kupitia tiketi ya chadema, kwa baadhi ya wagombea, sio kweli kuwa wanataka kugombea urais kwa dhati, bali kunatumika tuu kama kichaka cha kujifichia aibu ya kugombea na kushindwa Ubunge?, hivyo kuutumia huo ugombea urais wa kupitia Chadema as an excuse ya kutogombea ubunge?.

Au ndio wanatangaza nia ya kugombea urais kupitia Chadema ili kuutumia ugombea huo kama ngazi ya kujisuru kipigo cha CCM kwa kuwaonyeshea wapiga kura kuwa wao ni presidential materials, hivyo kama wangeweza kuwa rais wa JMT kupitia Chadema, then ubunge ni nini compared?, hivyo kuwapa mileage zaidi ya kuchaguliwa ubunge?.

Lengo la kuuliza hivi, ni kufuatia watia nia wakizidi kumiminika Chadema licha ya kumjua mgombea wa CCM ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli, ni mtu wa namna gani, na amefanya nini, na wewe unajijua ni mtu wa namna gani, unawezaje kathubutu kuchukua fomu kuomba kuteuliwa Chadema kumkabili Magufuli?.

Nilidhani wana Chadema, baada tuu ya kumsikia Tundu Lissu ametangaza nia, then haikutarajiwa kama kuna mtu mwingine yoyote Chadema angethubutu kuchukua fomu kwa upinzani kufutia upinzani legelege uliopo nchini Tanzania kiasi kwamba kwa maoni yangu, ndani ya kambi nzima ya upinzani, watu pekee ambao wanaweza kumkabili rais Magufuli na aka feel angalau ka joto joto cha uchaguzi, ni Tundu Lissu na Zitto Kabwe pekee, hivyo hawa wagombea wengine wanao omba kuteuliwa Chadema, are they serious kweli au wanagombea tuu ili na wao kuonyeshea ni presidential materiale?!.

NB. Leo ninapozungumza haya, sii wengi wanajua kuwa kuna baadhi ya wabunge wa majimbo wa Chadema, hawatagombea tena uchaguzi wa 2020, hivyo namna nzuri ya kutogombea kwa heshima ni kugombea urais!. Lakini kwa wale ambao hawatapitishwa kwenye urais na kuendelea kugombea ubunge, then bandiko hili haliwahusu!.

Jumatatu Njema.
Paskali
Rejea
Elections 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!.

Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja?

Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!.

Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?!.

Elections 2020 - Kukubalika kwa Rais Magufuli/CCM: Kishindo cha asilimia 99.9% ni mawingu tu ya dalili, mvua ni 2020, ni lele tu, ngoma ni 2020!
 
Naona wanafunzi wa Yesu wa chato mko busy kuandika Nyaraka za kitume kwajili ya agano la pili la utawala wa Yesu wenu.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom