Kupitia Account Number haiwezekani kabda awe na CVV pamoja na Exp date, hapo mtandaoni ataagiza mziko kwa kutosha tu[emoji16], ikiwezekana hadi kuhamisha mzigo wote kabsa
Kuna kitu watu wanachanganya kidogo linapokuja swala la malipo/ utoaji wa fedha kwa njia ya mtandao.
Unapozungumzia fedha kutoka kwenye akaunti ya mteja endapo mdukuaji/mwizi amepata CVV na Expiry date ya kadi ya benki, kitu kingine kinachohitajika ni kadi namba na sio akaunti namba.
Kwa kusema hili, kama nitatoa akaunti namba tu, bila taarifa zangu za kadi kujulikana na mtu mwingine na kama kadi yangu imewezeshwa kufanya manunuzi ya mtandao, basi hapatakuwa na hatari ya mtu kutoa fedha kwa njia ya mtandao.
Kinyume chake ni kwamba tunapswa hifadhi kadi zetu za benki katika hali ya usalama ili kuficha taarifa za kadi ikiwa ni pamoja na kadi namba, expire date na CVV. Pia haishauriwi kumpigia mtu picha ya kadi yako na kumtumia kwa njia ya mitandao, maana unatoa taarifa muhimu za kadi yako. Hata tunapotuma taarifa za kadi zetu mfano namba za kadi basi kuna utaratibu wa kuficha zile namba kwa kutoziandika zote, bali kureplace baadhi ya namba kwa ***.
Utaratibu ni kuandika namba sita za mwanzo, kisha unaficha sita zinazofuata na kuandika nne za mwisho. Na hii hufanyika kama unashare kwenye mitandao au email na mtu.
Ila endapo utapaswa fanya manunuzi basi zinapohitajika hizi namba basi utalazimika kuzituma kama zilivyo pamoja na taarifa nyingine zitakazo hitajika.
Jambo la kujifunza ni kuwa usitumie kadi yako kufanya manunuzi ya kimtandao yanayo hitaji utoaji wa taarifa za kadi yako kwenye mitandao isiyokuwa secured. Pia inashauriwa kutumia njia zingine kama Paypal ambao hawa kimsingi utawapa taarifa ya kadi yako, na pindi utakapofanya malipo basi itahitajika wewe ukubali kwanza kabla fedha haijakata kwenye akaunti. Wao wanafanya kazi kama mtu kati baina ya mnunuzi na muuzaji.
Mwisho kabisa, unaweza fanya manunuzi kwa njia ya kadi kwa kadi ambazo hazina hata akaunti namba zaidi ya namba ya kadi na taarifa zingine kama CVV na expiry date.