Je, kuna uwezekano wa vita kuu ya dunia ya 3 kutokea? Na JE, tujiandaaje??

Tsyamatsy

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2023
Posts
265
Reaction score
421
Wahenga walinena, 'lisemwalo lipo na kama halipo liko njiani linakuja!'

Katika hii vita Kati ya Urusi na Ukraine, Urusi ilishataadharisha mapema kuwa iwapo Mataifa ya NATO yatairuhusu Ukraine kutumia Silaha za masafa marefu kushambulia ndani ya Urusi, basi Urusi itahesabu kuwa NATO imeingilia vita hivyo.

Hii ina maana Urusi itahesabu kuwa inapigana na NATO.
Sasa pamoja na Ukraine kuruhusiwa kutumia Silaha hizo na nyongeza sasa imeruhusiwa kutumia mabomu ya kutegwa ardhini yaliyopigwa marufuku.

Urusi nae ana-test na kuweka Sawa mitambo yake ya nyuklia. Sasa Hatima yake NI nini??

Mwaka 1978 wakati Tanzania inapambana na Uganda, Mwalimu Nyerere aliagiza WaTanzania kuchimba maandaki ili kuwa tayari na sehemu za kujificha iwapo mambo yangeenda mrama.

Na wito huo uliitikiwa ipasavyo na wananchi.

Je, Kwa hili la Urusi na NATO linaloendelea Kwa sasa, Viongozi wetu wanajiandaa vipi iwapo kitawaka huko??

Wanatishana tuu kwa hapa tulipofikia ni ngumu sana kuwa na aina hiyo ya vita
 
Sisi tupo tayari kutoa mchango wetu, kuna Timu urusi na timu marekani zinaandaa keyboard kwa mapambano
1000012697.jpg
 
Wanatishana tuu kwa hapa tulipofikia ni ngumu sana kuwa na aina hiyo ya vita
Kabla Mrusi hajaivamia Ukraine alianza Kwa kuonya hivi hivi, na Akina Marekani wakampuuza, na hatimae akafanya kweli na Hadi Leo vita inaendelea. Na Biden amedhamiria kutuachia msala katika siku hizi zake za utawala wake, na akifahamu fika kuwa Mrusi hatabiriki. Ogopa kupambana na mtu ambae ameamua Bora afe kuliko kutawaliwa!
 
Vita kuu ya dunia ya 3 vs Vita kuu ya 3 ya dunia! Hizo ni phrases mbili zenye maana tofauti kabisa.

Kukujibu ulichouliza; hakuna uwezekano wa vita kuu ya dunia ya 3 kwa maana halisi ya vita kutokea. Hivyo, hakuna sababu ya kujiandaa kwa kitu ambacho hakitarajiwi.
 
Kama ni vita ya Congo au Sudan Sawa, lakini hii ya miale na mionzi mmh!
Wamepigana Russia na Ukrain, huku wewe unauuziwa chapati moja 2000, na mchele ulikuwa mpaka 4000 kwa kilo , sukari ilipotea, mahindi yalifika bei ambayo haijawahi tokea tupate uhuru,
Haya changanya na za kwako, hiyo miale haitakufikia wewe mmatumbi hauna mashiko katika siasa za dunia.....
Utabanwa na mahitaji yako tu.........
 
Vita kuu ya dunia ya 3 vs Vita kuu ya 3 ya dunia! Hizo ni phrases mbili zenye maana tofauti kabisa.

Kukujibu ulichouliza; hakuna uwezekano wa vita kuu ya dunia ya 3 kwa maana halisi ya vita kutokea. Hivyo, hakuna sababu ya kujiandaa kwa kitu ambacho hakitarajiwi.
Iwapo Urusi wanawatengenezea raia wake vifaa vya kujikinga na mionzi ya nyuklia na kuamuru jeshi lake kujibu shambulizi lolote toka Magharibi, NI Kwa nini serikali yetu wasilione hili na kujiandaa. Kujiandaa Kwa madhara yanayoweza kutokea Kama vita ya Ukraine ilipoanza kulitokea uhaba WA chakula, mafuta kupanda bei n.k. Waingereza wanasema 'Once beaten twice shy!' au tuseme ' kufanya kosa sio kosa bali kurudia kosa ni kosa' Serikali waliangalia hili!
 
Wahenga walinena, 'lisemwalo lipo na kama halipo liko njiani linakuja!'

Katika hii vita Kati ya Urusi na Ukraine, Urusi ilishataadharisha mapema kuwa iwapo Mataifa ya NATO yatairuhusu Ukraine kutumia Silaha za masafa marefu kushambulia ndani ya Urusi, basi Urusi itahesabu kuwa NATO imeingilia vita hivyo.

Hii ina maana Urusi itahesabu kuwa inapigana na NATO.
Sasa pamoja na Ukraine kuruhusiwa kutumia Silaha hizo na nyongeza sasa imeruhusiwa kutumia mabomu ya kutegwa ardhini yaliyopigwa marufuku.

Urusi nae ana-test na kuweka Sawa mitambo yake ya nyuklia. Sasa Hatima yake NI nini??

Mwaka 1978 wakati Tanzania inapambana na Uganda, Mwalimu Nyerere aliagiza WaTanzania kuchimba maandaki ili kuwa tayari na sehemu za kujificha iwapo mambo yangeenda mrama.

Na wito huo uliitikiwa ipasavyo na wananchi.

Je, Kwa hili la Urusi na NATO linaloendelea Kwa sasa, Viongozi wetu wanajiandaa vipi iwapo kitawaka huko??

System ya western baada ya kugundua trump atakuja kumaliza huu msala wameamua kutengeneza mazingira yawe magumu kwa Trump kufikia hilo. Na ndan ya miez hii miwili ijayo dunia ipo kwenye hatar kubwa zaid kuliko miaka hii mitatu ya vita iliyopita.
 
Back
Top Bottom