Je, kuna watu ambao wako systematically prone kwa tabu na mateso na ni vigumu mikosi yao kuondolewa kirahisi kama wengine?

Je, kuna watu ambao wako systematically prone kwa tabu na mateso na ni vigumu mikosi yao kuondolewa kirahisi kama wengine?

Mi nadhani kuna watu tu wana bahati nzuri na wengine wana bahati mbaya haijalishi ni wema au wabaya kiasi gani. Sasa hiyo bahati nzuri au mbaya unaipataje ndio sijui.
Ingekuwa ni uchapa kazi basi wabeba zege wangekuwa na maisha mazuri sana maana ni wachapa kazi haswaa. Sio kwamba watu ni wavivu, wana bidii sana ila hawana bahati, chochote wanachojaribu hakiendi. Wameshachanganya maombi mpaka ya kufunga kavu lakini hola. Kuna watu wanalima maheka kibao kuvuna gunia moja. Wakati wengine wanatokea hapo hapo. Bado naendelea kuamini kuwa ni issue ya BAHATI, NYOTA, NEEMA.
Inafikirisha sana

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mwanadamu asie kuwa na changamoto. Asilimia kubwa ya watu duniani tunapitia matatizo makubwa mbali mbali ila kuna wale watu ambao utafikiri furaha hata robo sio ridhiki kwao.

Unaweza mkuta mmama, mwenye hurka ya kuishi vyema na watu lakini anapitia mateso kutoka kwa mme wake, wifi zake kumchukia, ana magonjwa ya muda mrefu, watoto nao karibia wote wameharibika na bado mengine kuongezeka.

Unakuta mama huyu awali amepita kwa waganga wote wenye sifa lukuki ila hakuna msaada.

Then akaamua kuokoka na kujiweka katika utumishi ila unaweza ana miaka zaidi 15 katika utumishi wa kweli ila bado ni mtu wa tabu juu ya majanga.

Najua mna mifano mingi huko mitaani kwenu.

Sasa unajiuliza amekuwa mhanga wa laana za mababu zake ambazo ni unforgiven?

Je, amekingia mgongo na the higherpower yani hata afanye nini ni mateso ndio njia yake hadi kaburini?

Ni mtu wa kuzungukwa na strong negative energy zinazo mtesa??
Ninamwamini Mungu kwa 100% ila nasema matatizo yote yanapaswa kutatuliwa kwa wakati wake, wakati ukishapita unaweza kufikiri hakuna Mungu! Ila kunakuwepo na msaada au neema ya tumaini na ustahimilivu ambapo hata kama hutapata exactly uombacho lakini unapewa neema ya ustahimilivu.
 
Back
Top Bottom