Je kuna watu wako hai mpaka sasa Kama walivyoahidiwa na Bwana Yesu?

Je kuna watu wako hai mpaka sasa Kama walivyoahidiwa na Bwana Yesu?

Down To Earth

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
21,940
Reaction score
16,643
Reference:
Marko 9:1
Luka 9:27
Mathayo 16:28

Mistari yote hio ina ujumbe unaofanana, ya kwamba
Screenshot_20241202-120321.jpg

Maneno hayo yalitamkwa na Bwana Yesu mwenyewe akiwa katika mwili wa damu na Nyama akiwaambia kuna watu watauona ufalme wa Mungu kabla ya kufa..

Kumbuka ishapita miaka elfu 2 mpaka sasa

Je, hao watu wako wapi???
 
Reference:
Marko 9:1
Luka 9:27
Mathayo 16:28

Mistari yote hio ina ujumbe unaofanana, ya kwamba
View attachment 3167298

KITAB AL MUKADAS Hakisomwi Kwa kukariri kama Quran ust!😆😆😆
👇👇
2 Corinthians 3:6
[6]Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.
 
Reference:
Marko 9:1
Luka 9:27
Mathayo 16:28

Mistari yote hio ina ujumbe unaofanana, ya kwamba
View attachment 3167298

Maneno hayo yalitamkwa na Bwana Yesu mwenyewe akiwa katika mwili wa damu na Nyama akiwaambia kuna watu watauona ufalme wa Mungu kabla ya kufa..

Kumbuka ishapita miaka elfu 2 mpaka sasa

Je, hao watu wako wapi???
Kutokana na nukuu ulizoonyesha ni wazi kuwa wewe ni msomaji mzuri wa maandiko yaani Biblia. Utakumbuka pia halijaonekana kaburi la Musa, kwa maana hiyo hakuna aliyemzika, kadhalika Eliya alitwaliwa mzima mzima. Sasa nikukumbushe, mara kadhaa Maria mama yake Yesu alikuwa akimfuata kule alikokuwa akienda pamoja na wanawake wengine kadhaa. Bikira Maria aliyeandaliwa kutwaa mimba ya Yesu, Masihi wa Mungu, je anaweza kuachwa mwili wake uharibike wakati huyo mwanae Yesu aliweza kufufua watu wengine? Bikira Maria alichukuliwa akapaa mbinguni. Kuna watu watauliza, imeandikwa wapi? Naomba wasome Yohana 21:25
"Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa".
 
Ufalme wa Mungu mbona ulishakuja kitambo sana, kabla hata Yesu hajaondoka.
Soma Luka 11:20 (Lakini, ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia).

Na ufalme huo hata mimi ninao,
Luka 6:20 (Akainua macho yake akawatazama wanafunzi wake, akasema, Heri ninyi mlio maskini, kwa sababu ufalme wa Mungu ni wenu.)
 
Back
Top Bottom