Je, kuna watu wanaoweza kusoma mawazo ya wengine? 🧠

Asante kwa maoni mkuu🙏🙏

1. Hao wanaosomea wanafunzwa kuisoma akili ya mtu direct au wanafundishwa kusoma body language ya mtu hata kama yupo kwenye utulivu mkubwa

2. Kuna uwezekano mtu akazaliwa na huu uwezo ?
Kwahiyo hiki ni kipaji?

3. Niambie hapo kuhusu manabii

4 nitapitia nyuzi za mzee Pascal Mayalla kadri nitakavyopata muda asante
 
kudai kujua moja kwa moja kilicho kwenye akili ya mtu: “Ananichukia,” “anaficha kitu,” au “anafikiria X.?

Hii hakuna anayeweza kufanya

Claim Vs Evidence
 
Nonverbal cues,

Naona mnamix gestures with mind reading

Hivyo ni vitu vitano tofauti
Ukiona nime mix
Wewe kuligundua hilo ni kwa sababu unajua zaidi kwa maana hiyo

Karibu utueleze tofauti na namna ya kutofautisha hivyo vitu vi 5
Nasubiri mkuu 📝
 
So uligundua ana wivu kupitia ishara?
Mi nataka kujua je mtu anaweza kusoma mawazo ya mwingine

Au ni ishara ndio zinatafsiri kile mtu anachokiwaza ?
Yule mshikaji ana wivu sana na nilikuwa namjua vyema. Kukusaidia zaidi tafuta hiki kitabu , nilishawahi kuwa nacho mwaka 2014 sijui kilipotelea wapi lakini pale Efatha kwa Mwingira nadhani kipo na kipo na cha kiswahili


Huyu mwandishi Iyke alikuwa ni Makamu wa rais wa Wachawi Africa, halafu huwa tunabishana sana kuhusu uchawi lakini ukikisoma hiki kitabu utajifunza na kufahamu mengi. Huyu Mwandishi alishaokokà na kuwa Pastor mkubwa sana na siri nyingi za uchawi amezianika wazi
 
Ukiona nime mix
Wewe kuligundua hilo ni kwa sababu unajua zaidi kwa maana hiyo

Karibu utueleze tofauti na namna ya kutofautisha hivyo vitu vi 5
Nadibiri mkuu 📝
Ukiona ni “mix,” basi tayari kuna distinction muhimu umeiona. 🙂 Tatizo ni kwamba mara nyingi watu wanachanganya kile kinachoonekana, signal yenyewe, na interpretation ya signal hiyo.
Kwa mfano, gesture ni movement fulani; nonverbal cue ni taarifa inayoweza kutolewa bila maneno; body language ni broader pattern ya posture/movement/expression; inference ni tafsiri tunayofanya kutokana na cues; na mind reading ni kudhani unajua moja kwa moja kilicho kwenye akili ya mtu.
Kwa hiyo si kila gesture ni ujumbe maalum, na si kila cue inatupa access ya moja kwa moja kwenye thoughts za mtu. Hapo ndipo tofauti kati ya observation, interpretation, na mind reading ilipo.
 
1. inaweza ikawa ni direct au in-direct ili uweze kumsoma mtu ni lazima mjongeo wa mwili na sauti uwepo japo hata maiti inaweza kuzungumza ukitaka kuisoma
2. ndio inawezekana kabisa intelligency wengi wamezaliwa na huo ujuzi...ila ukisoma sana unaweza ukajiongezea maarifa ya kukuwezesha kuwajua watu na binaadam...
3. manabii wengi wamesoma au wamezaliwa na kipawa cha utambuzi...hivyo akikuona tu anaweza kukuelewa na kucheza na akili yako akakuvuruga ukamuamini...ila ni kitu kidogo tu watu wanadanganyika kwa kuambiwa mambo yao ambayo wanadhani wanayafahamu wenyewe....!
 
Duh makamu wa rais wa wachawi? vipi online kinapatikana mkuu
 
Kusoma mawazo ya mtu ni rahisi sana kama ukivuta ganja kiasi kwa mtu unaemfahamu

kwa mtu usiemfahamu vuta pia kiasi na uwe msikilizaji sana
Ni hayo tu!
 
Kwanza finale wanawake wamepata mtu wa kuwatoa unyonge,maana siku za nyuma ilikuwa inasemwa mbona wanawake hawachapishi nyuzi?

Sasa walau wamepata mwakilishi wao,tena haandiki tu nyuzi kama nyuzi ili mradi awe ameandika ila ni nyuzi ambazo hata ukisoma hujutii kutumia muda wako kuzisoma

Hongera sana mto mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…