Je, kupaka matope utawala wa hayati Magufuli kutatubeba wapinzani kisiasa? Magufuli hayupo nasi kwenye ulingo wa kisiasa, kwanini mnakomaa kumchafua?

Utawala Wa JPM haukuwa rafiki kwa jamii nzima wakiwemo Wafanyabiashara wakubwa. Kwa hiyo si wapinzani tu wanaousema utawala huo, wapo Wafanyabiashara, wafanyakazi Wa umma, CCM asilia n.k n.k
Hakuna alipo kubalika ukiacha wale waliofanya hivyo kwa kujikomba na uzandiki
 
Wewe jamaa umetisha sana kwa kuwa na maktaba ya kutosha.
 
Yaani watu wote wakiwa na akili duni za kufikiri na kisha kuamua kama zako, maisha yasingekuwa na maana kabisa...

Yes, he's dead but he's in the history books....

Na katika maisha haya, historia ni mwalimu wa wakati uliopo na tunatumia historia ku - predict future...

Mfano, ni mtu mjinga pekee (kama wewe) na asiye na maarifa anayeweza kutoihusianisha hali ya maisha ya sasa ya watanzania kisiasa, kiuchumi na kijamiii na tawala zilizokuwa chini ya Nyerere J.K, Mwinyi A.H, Mkapa B.M, Kikwete J.K na Magufuli J. P wote hawa chini ya CCM...

Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu, atazitumia tawala hizi zote kama baseline ya kujifunza kwa kuonya na kutahadharisha ili utawala uliopo na ule ujao kuepuka makosa ya hawa watangulizi wao...

John P. Magufuli atasemwa na ataendelea kutumiwa kama reference point ya footprints ya UTAWALA MBAYA na MUOVU ZAIDI kuwahi kutokea Tanzania tangu uhuru...

Na hii si kwa sababu wewe hutaki asemwe kwa ujinga wako, bali ni kwa ajili ya manufaa ya wananchi na utawala huu uliopo sasa chini ya Rais Samia na ule unaokuja aidha baadae mwaka huu, ama mwaka kesho au 2025 katika kufanya maamuzi sahihi ya kiutawala...


Sasa tukimchafua hayati ndio na sisi tutapaa kisiasa?

Hili nalo ni la kujibu?

Anyway, ngoja ujibiwe. "Kumchafua hayati" kwa tafsiri yako maana yake nini eti?

Na by the way, unawezaje kukichafua au kukisaficha kitu kisicho na uhai, kilichokufa...?

Unatumia dimension gani kufikiri na kuuliza swali kama hili...?

Katika mazingira haya wewe Kamanda Asiyechoka, hapa hasemwi wala hajadiliwi Magufuli as a person tena maiti. Tunajadili footprints za utawala wa Rais Hayati John P. Magufuli...!!
 
Ubongo wako uko wazi angalia vizuri.
Kwa hiyo Magufuli alikuwa ni tajiri au maskini
alikuwa ni mtoto wa aina gani kati ya hao wanaozaliwa na neema au lah!?
Usirudie tena kuniuliza hili swali!! kwakuwa Jiwe yeye alipozaliwa lilikuwa ni giza totorooo!!! utosini!!...alikua mpaka utu uzimani kwa bahati tu !...lkn wazee wa koo zao walijua yanayo jilri alipo kufa hawakulia!...kawaid mie nimetabiriwa kuwa Rais punde tu ntakuwa!

Nikusaidie tu!! ubongo ukibaki wazi nusu sekunde huna maisha! hao walio kufundisha ubongo unakaa wazi walikuingiza chaka stuka!! ndo matokeo ya shule za kata haya na ni dhahiri!!
 
Watu wanatakiwa waujue ukweli uliopita uliopo na ujao.

Kuujua ukweli uliopita kunatupa picha ya tuendapo. Mfano kama aliyepita aliharibu na huku aliyepo hakukemea ina maana aliogopa matokeo vipi sasa hataogopa matokeo ya 2025 kama atakemea?
Kwahyo waache watu waseme hatakama ni mambo ya awamu ya kwanza
mbona awamu ya 5 iliziponda awamu zote za awali hata kutaka kuanzishwa kwa kufundishwa kilazima historia nia haikuwa kuelewa tu historia ya hapa nyumbani nia kuu ilikuwa kumpaisha mwendazake na kuponda awamu nyingne kwa technic kali.
Vitabu vilishaandaliwa na waziri wa elimu ndalichako akakubali. Alipoingia mama vitabu vikachomwa moto na kazi ya unafiki ikafia hapo kwa muda. Maana wanafiki hawajawahi kwisha
 
Amechafuliwaje ? Yaani kutaja mapungufu yake kikazi nd
Mmawia sorry hii reply imeingia sipo hii inajajibu kwa Kamanda Asiyechoka
&____________&&&________


Hakuna anaemchafua ila kuna habari za Magu hupendi kusikia unataka asifiwe tu.

Tunajua hupendi watu waongelee chato Airport, n.k kama yeye alikuwa smart kichwani sukari tu si ingeshuka bei sio kupanda, halafu anasema aliikuta elfu 5 yeye pres. Wa wanyonge ndio kaishusha mpaka 2.5

We unadhani Hitler hakujenga miundo mbinu, au Stalin au Mobutu. Ila katika wote hao sijaona mahali watu wanataja jina la Rais na kulipambanisha na Mungu kama ilivyokuwa kwa Magu.

Dah !!! Magu alipitiliza aisee, au umesahau yule kiongozi aliyesema kwa sauti kubwa tu kwamba Mungu anapaswa kumshukuru Magu kwa utendaji wake !! Na Magu ka kaa kimya tu, mbona Mwinyi alipiga marufuku watu kumwita Mtukufu.

Jamaa yako atasemwa sana tena kwa mabaya ndio maana tunakuwa na historia. Historia yako unaijenga mwenyewe, sasa wewe unataka historia ifutike kivipi sasa, wakati chato airport ipo, wakati ni kweli alituambia anatuma boeing kufuata dawa ya covid na jamaa yetu prof akabwia fasta fasta, lakini boeing iliporudi jiiiiiiii
Anavibweka vingi yule mzee pole sana. Huwezi kupiga stop historia.



Sasa tukimchafua hayati ndio na
 
Jirani yangu ni adusa mtendaji wa kata tena mtu mzima anayekaribia kustaafu. Mzee huyu nimemfahamu kwa miaka zaidi ya 12 hivi, ni mpenzi sana wa kuvaa suti za khaki kama zile gwanda za chadema japo sio mwanachama wala shabiki.

Nguo zake zilimfanya asimamishwe kazi kisa tu anahisiwa kwamba ni mwanachama wa chadema. Alikaa bench almost miaka miwili na amerudishwa kazini baada ya kifo cha Magufuli. Mwendazake hakua rais mpenda haki na usawa na wala haina haja ya kumpaka matope ili kumchafua.
 
Anavuna alichopanda! Mazuri aliiyafanya ulikua ni wajibu wake hatuna haja ya kuyakumbuka, tukumbuka mabaya yake tu.
 
Utawala Wa JPM haukuwa rafiki kwa jamii nzima wakiwemo Wafanyabiashara wakubwa. Kwa hiyo si wapinzani tu wanaousema utawala huo, wapo Wafanyabiashara, wafanyakazi Wa umma, CCM asilia n.k n.k
Utawala wa Magufuli haukuwa rafiki kwa waovu
 
Nadhani ungekuwa unamjua Mmawia vizuri usinge andika haya yoote.

Jaribu kumfuatilia vizuri Mmawia
 
Soma kuanzia mstari wa kwanza mmawia atakuwa ameona hapo.

Hata hii kuongelewa sana iwe kijiweni au jf ni historia inaendelea sasa mwingine anataja ipigwe stop.
Nadhani ungekuwa unamjua Mmawia vizuri usinge andika haya yooten.

Jaribu kumfuatilia vizuri Mmawia
 
Soma kuanzia mstari wa kwanza mmawia atakuwa ameona hapo.

Hata hii kuongelewa sana iwe kijiweni au jf ni historia inaendelea sasa mwingine anataja ipigwe stop.
Nimekusoma kamanda.
 
Apumzike kwa Amani Shujaa
 
Kafie Chato huko na kiherehere chako..

Kama alikufurahisha wewe si ufanye hiyo kazi ya kumsafisha? Kwanini unataka hiyo kazi tuifanye sisi sote?
 
hahaha hat nymba km hamna
 
Mtu muovu anapaswa kusimangwa akiwa hai au amekufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…