Kama kuna busara ya kisiasa tunakatakiwa kuwa nayo wapinzani ni hiki kipindi ambacho wapinzani wanapayuka hovyo kumchafua hayati JPM. JPM is gone na kila mtanzania anafahamu juu ya utawala wake. Kama alifanya mema basi atahukiwa na Mungu na wananchi wanayo nafasi ya kujua mabaya na mazuri yake.
Sasa sisi kama wapinzani tunatakiwa kupambana na hayati JPM au Ccm hii ya mama Samia.
Je tukikomaa kumchafua hayati JPM ndio tutafanikiwa kisiasa?
Nawakilisha mimi Kama
Yaani watu wote wakiwa na akili duni za kufikiri na kisha kuamua kama zako, maisha yasingekuwa na maana kabisa...
Yes, he's dead but he's in the history books....
Na katika maisha haya, historia ni mwalimu wa wakati uliopo na tunatumia historia ku - predict future...
Mfano, ni mtu mjinga pekee (kama wewe) na asiye na maarifa anayeweza kutoihusianisha hali ya maisha ya sasa ya watanzania kisiasa, kiuchumi na kijamiii na tawala zilizokuwa chini ya Nyerere J.K, Mwinyi A.H, Mkapa B.M, Kikwete J.K na Magufuli J. P wote hawa chini ya CCM...
Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu, atazitumia tawala hizi zote kama baseline ya kujifunza kwa kuonya na kutahadharisha ili utawala uliopo na ule ujao kuepuka makosa ya hawa watangulizi wao...
John P. Magufuli atasemwa na ataendelea kutumiwa kama reference point ya footprints ya UTAWALA MBAYA na MUOVU ZAIDI kuwahi kutokea Tanzania tangu uhuru...
Na hii si kwa sababu wewe hutaki asemwe kwa ujinga wako, bali ni kwa ajili ya manufaa ya wananchi na utawala huu uliopo sasa chini ya Rais Samia na ule unaokuja aidha baadae mwaka huu, ama mwaka kesho au 2025 katika kufanya maamuzi sahihi ya kiutawala...
Sasa tukimchafua hayati ndio na sisi tutapaa kisiasa?
Hili nalo ni la kujibu?
Anyway, ngoja ujibiwe. "Kumchafua hayati" kwa tafsiri yako maana yake nini eti?
Na by the way, unawezaje kukichafua au kukisaficha kitu kisicho na uhai, kilichokufa...?
Unatumia dimension gani kufikiri na kuuliza swali kama hili...?
Katika mazingira haya wewe
Kamanda Asiyechoka, hapa hasemwi wala hajadiliwi Magufuli as a person tena maiti. Tunajadili footprints za utawala wa Rais Hayati John P. Magufuli...!!