comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 9,019
- 6,825
Nimeona katika mijadala yetu kuhusiana na kupanda kwa bei ya vyakula kumezaa tabaka la wakulima (ambalo halitajwi wala kuonewa huruma) na la wananchi (ambalo linatajwa na kuonewa huruma).
Ningependa kuchangia kwa kusema na kumbusha kuwa, hakuna namna yoyote ya kupata chakula bila kulima kwa hiyo yeyote anayejadili chochote kuhusu chakula asimpomtaja mkulima anajilaani.
Kwa mda mrefu wakulima wamekuwa wakipunjwa sana bei ya mazao yao, sasa hilo limefika mwisho baada ya serikali kupanua soko. Mkulima sasa anapata bei ya haki na sahihi ya kumuwezesha kurudisha gharama za uzalishaji na kubaki na faida. Hii inafuata misingi ya SOKO LA HAKI (FAIRTRADE).