Je, kurudia au kubadili rangi gari ni vibaya?

Je, kurudia au kubadili rangi gari ni vibaya?

Andres

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2013
Posts
502
Reaction score
815
Wakuu habari za muda huu,

Kuna suala naomba nipate ufahamu zaidi.

Imekuwa ni kawaida kwa watu kuuliza kama gari limerudiwa rangi au kubadilishwa rangi pale anapotaka kulinunua mkononi kwa mtu.

Na mara zote imeonekana kama kupaka rangi gari ni kama inaishusha thamani. Inapelekea wengine kuficha hili.

Sasa swali langu, kwani haya magari huko kiwandani si mwanzo ni material yanayopakwa rangi tu?

Au ukishapaka rangi gari, itapauka au kuchubuka ukilinganisha na rangi inayotoka nayo kiwandani?

Kiufupi kwanini inachukuliwa kama kitu cha kushusha thamani gari ? Kwani hamna mafundi wenye weledi wa rangi kiasi hicho Tanzania.
 
1. Upate fundi wa kueleweka
2. Ubora wa rangi, kuna rangi og na fake maamuzi ni yako hata fundi atakwambia hilo
3. Aina ya rangi kuna rangi ni gharama na kuna baadhi ya gari lazma upake rangi 2 hapo cost lazma iwe juu.
4. Aina ya gari
5. Fundi akipuliza rangi lazma apige na polish japo wengi huwa hawafanyi hvo
 
Wanapaka nenda hta kwa Ttr sema andaa 2m ukitaka uhakika wa rangi ila ukitaka bora rangi nenda kwa fundi juma hta 150k unakula rangi yako safu
Rangi za kuchanganya na vijiti vya mpera hizo ndio za 150k unapakiwa gari zima😂😂😂 ila ukitaka rangi halisi kopo tu la litre 1 na additives zake lazma walambe M na inapakwa kwa ratios!
 
Rangi za kuchanganya na vijiti vya mpera hizo ndio za 150k unapakiwa gari zima[emoji23][emoji23][emoji23] ila ukitaka rangi halisi kopo tu la litre 1 na additives zake lazma walambe M na inapakwa kwa ratios!

Jamaa angu kapuliza bampa ya mbele crown ametoa 200k ila huwezi jua kama alipuliza rangi kuna watu ni mafundi sana
 
Jamaa angu kapuliza bampa ya mbele crown ametoa 200k ila huwezi jua kama alipuliza rangi kuna watu ni mafundi sana
Yeah kuna watu wako makini! Ila gari za kupuliziwa rangi bana iwe nyeupe walau ikiwa silver unakuta rangi ina mawingu mawingu flani yani kuna sehem kama haijashika vizuri hivi basi dah😂😂😂
 
Yeah kuna watu wako makini! Ila gari za kupuliziwa rangi bana iwe nyeupe walau ikiwa silver unakuta rangi ina mawingu mawingu flani yani kuna sehem kama haijashika vizuri hivi basi dah[emoji23][emoji23][emoji23]

Na pearl hizi rangi hata zikioshwa zinang’aa sana[emoji119]
 
Back
Top Bottom