Je, kurudia au kubadili rangi gari ni vibaya?

Je, kurudia au kubadili rangi gari ni vibaya?

Wakuu habari za muda huu,

Kuna suala naomba nipate ufahamu zaidi.

Imekuwa ni kawaida kwa watu kuuliza kama gari limerudiwa rangi au kubadilishwa rangi pale anapotaka kulinunua mkononi kwa mtu.

Na mara zote imeonekana kama kupaka rangi gari ni kama inaishusha thamani. Inapelekea wengine kuficha hili.

Sasa swali langu, kwani haya magari huko kiwandani si mwanzo ni material yanayopakwa rangi tu?

Au ukishapaka rangi gari, itapauka au kuchubuka ukilinganisha na rangi inayotoka nayo kiwandani?

Kiufupi kwanini inachukuliwa kama kitu cha kushusha thamani gari ? Kwani hamna mafundi wenye weledi wa rangi kiasi hicho Tanzania.
Kupaka Rangi kuna hasara mbili,
Inaweza kuleta picha kua gari ilipata ajali ikanyooshwa na kupakwa Rangi.

Pili Rangi ya kurudia sio bora kama rangi iliyokuja na gari.
 
Anhaa lakini sio kwamba rangi kubadilishwa au kurudiwa ni kitu kibaya kwa gari kama halijapata shida yoyote? Mfano mi nna crown ya silver nataka iwe nyeusi, nikibadili rangi sijaishusha thamani
Kama ulikuwa upate 8m utapata 5milion au 4.5
 
Anhaa lakini sio kwamba rangi kubadilishwa au kurudiwa ni kitu kibaya kwa gari kama halijapata shida yoyote? Mfano mi nna crown ya silver nataka iwe nyeusi, nikibadili rangi sijaishusha thamani
Kuna utaratibu wa kufuata unapotaka kubadili rangi. Kama ni nyeupe maana yake hata TRA imesajiliwa kwa rangi hiyo.
 
Back
Top Bottom