Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,101
Habari za Jumatatu wana JF
Kwa ninavyoelewa ndoto zina maelezo tofauti kwa watu tofauti. Kuna fikra kadhaa lakini kubwa ni mbili
Fikra(school of thought) ya kwanza wanasema ndoto ni matokeo ya mawazo yako au mambo unayoyafikiria sana au marudio ya vitu ambavyo ulishawahi kuvifanya zamani
Wanachukulia ubongo wa binadamu ni kama Processing Unit ya computer ambayo hata ikizimwa inaweza kua anajipangia yenyewe ma file yake vizuri bila kua operated na mtu
Fikra ya pili ni wale wanaosema ndoto ni jambo la kiimani(spiritual) na huwa ni ujumbe unaokwambia kuhusu habari zijazo au taarifa ya kitu kilichotokea au kitakachotokea katika ulimwengu wa kiroho kiwe kizuri au kibaya na ambacho kitaweza kutokea au hata kisitokee katika ulimwengu halisi
Mimi sina ujuzi wa lolote katika hayo mawili lakini kuna mambo kadhaa yalishawahi kutokea kwangu kama ndoto na baadae yakatokea kwenye ulimwengu halisi
Mimi ni shabiki lialia wa Simba SC. Mwezi July mwaka huu niliota ndoto na immediate baada ya kuamka nikaisahau na sikuikumbuka mpaka siku mbili kabda ya Simba kucheza na wale Wabotswana ile mechi ya ugenini Lunyasi walioshinda 2-0
Niliota tumepigwa goli tatu na tumetupwa nje ya mashindano. Nilipuuza nikijua ni ndoto za Ali bin Nacha tu. Tena baada ya matokeo ya mechi ya kwanza ndio kabisaa nikapuuza. Kilichokuja kutokea baadae kinajulikana!!!!
Hoja na swali langu ni kwamba? Kwanini mtu unaweza ukaota ndoto ndeeefu kama sinema halafu mara tu ukiamka kutoka usingizini unajikuta umeisahau? Kama kuikumbuka inaweza ikawa siku nyingine kabisa
Nauliza swali hili kwa wale wote wenye fikra tofauti tofauti kuhusu kuota ndoto kwa binadamu. Huu usahaulifu wa ghafla kwa kitu kilichokutokea sekunde chache zilizopita upo kwenye sayansi ipi na nini maelezo yake?