Je, kusahau ndoto uliyoota muda mfupi kabda ya kuamka huwa ni kawaida?

Je, kusahau ndoto uliyoota muda mfupi kabda ya kuamka huwa ni kawaida?

Niliwahi kulitolea maelezo hili siku za nyuma. Mleta mada, embu tafuta desa hilo litakusaidia.
 
Nakumbuka hyo moja nilimuota mtu tulisoma nae kitambo and after few days nilikutana naye kituoni Mwenge na mazingira ni yale yale ya kwenye ndoto yalijirudia. Niliogopa! Ila badae nikapotezea nikasahau
Haijawah nitokea tena nadhani.

Sipendi sana kufatilia mambo ya ndoto maana ndoto zingine hua sio nzuri zinaweza fanya uishi kwa hofu
Na mimi nilikua najiuliza, hivi kuota ndoto na kisha mambo uliyoyaota yakawa yanajirudia kwenye ulimwengu halisi tunaweza kua
Niliwahi kulitolea maelezo hili siku za nyuma. Mleta mada, embu tafuta desa hilo litakusaidia.
Sawa Mkuu, ngoja nipekue
 
Naamini ndoto ziko kiimani zaidi,Mambo mengi niyafanyayo bila ndoto huwa Sina uhakika wa kufaulu kwa Mambo hayo!!!

Ndoto hutuletea taarifa ya mambo yajayo na hivyo kutupa onyo ama tahadhari,na Kama mtu anaota ndoto baadae anazisahau au Haiti kabisa huyo ni sawa na marehemu yampasa kujichunguza mienendo yake,kuna siku nililala na kuota mke wangu anachati na mtu ambaye alikuwa hawala yake wa zamani,na Hadi namba ya simu ya bwana yake nilioneshwa,nilipoamka asubuhi nilimwambia mke wangu akakataa,baada ya siku mbili nilimfuma na namba ilikuwa Ni Ile Ile niliyoota.

Nilipokuwa shule nikiota nakimbia mbio ,na katika mbio hizo tuko watatu na nikawa eidha wa kwanza au wa pili na hata wa tatu Basi lazima nishike namba hizo katika matokeo ya mitihani yangu.

My brother mwaka 2010 aliniambia kuwa ameota kuwa Tanzania Kuna siku moja itatawaliwa na mwanamke ,nilimkatalia na nilimwambia labda miaka 100 ijayo ,Leo hii tuko katika utawala wa mwanamke.

Juzi kaniambia kuwa kaota makamu wa rais Dr. mpango amechukua madaraka,lakini ni katika namna ambayo si nzuri ,

Ndoto Mimi huziamini Sana,kikubwa ukilala na kuota ndoto ambayo Ni mbaya,pale pale amka na uikemee ili kuzui Mambo hayo kutokea.
Dawa ni kuliewa tu,ukilewa hunting chochote cha zaidi ni kushtuka asubuhi...huelewi chochote.
 
Back
Top Bottom