Je, kushikamana na Sunnah ni Itikadi kali au ndio njia iliyonyooka?


“Tatizo ni kwamba umeitafsiri Qur’an kwa akili yako bila kurejea maelezo ya Mtume ﷺ na Maswahaba. Qur’an yenyewe imetuamrisha tumtii Mtume ﷺ kwa kile anachotuamrisha, si Qur’an pekee. Allah amesema:
﴿وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا﴾
‘Na alichokupeni Mtume kichukueni, na alichokukatazeni jiepusheni nacho.’ [Al-Hashr: 7]
Na pia amesema:
﴿مَنْ يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّهَ﴾
‘Anayemtii Mtume basi amemtii Allah.’ [An-Nisaa: 80]
Kama Sunnah si hoja, basi tutajuaje idadi ya rakaa za Swalaah? Namna ya kutoa Zakaah? Taratibu za Hijja? Haya yote yamefafanuliwa na Sunnah.
Ama kuhusu ‘wenye mamlaka’, aya haimaanishi kufuata maimamu kipofu. Wanachuoni wameeleza kuwa tunawatii katika haki kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah, si kutunga dini mpya.
Kusema ‘Qur’an pekee’ ni kosa kubwa, kwa sababu Qur’an yenyewe inatuamrisha turejee kwa Mtume ﷺ na kufuata Sunnah yake.”
 
Wapi Quran imesema tufuate Sunnah ya mtume?.. hakuna pahala Quran imetamka Sunnah ya mtume,kwa mujibu wa mkewe,bi Aisha,mwenendo(Sunnah )wa mtume ni Quran
Ikiwa hutakiwi kuwafuata kiupofu maimam bali ikiwa wanafuata Quran ndivyo vivo hivyo unapaswa kumfuata mtume pale atakapoelekeza kwa misingi ya Quran
Ama kwa upande zakkat ni moja ya tano ya kila upatapo faida baada ya kufanya biashara, yaani 20% ndiyo fungu la Allah sw
Ama kuhusu rakaa,swala ina rakaa mbili tu kwa utimilifu wake,kwa mujibu wa Quran
 
Quran rahisi kueleweka na inajitisheleza
44:58,19:97,39:27,5:15,26:195,15:1,6:114,10:1,6:115,7:52,16:89,54:17

Hijja
22:27,22:36,,2:158,22:37,2:196-198,22:29
Zakkat
8:41
Idadi ya rakaa
4:101-103
 

Unajua makosa makubwa wanayofanya waislam wengi ni kukosa elimu...
na elimu ninayo iandika hapa sio elimu ya Quran, ni Elimu ya kawaida inayo muwezesha Muislam kuielewa Quran. Kama mtu hana Elimu pana kidogo kuna vitu vingi kabisa kwenye Quran hawezi kuvielewa
Na ndio wengine hutoa post za kuleta taharuki huko kwenye mitandao ; kwa kuto kuelewa kilichomaanishwa kwenye Quran.

Kuna watu wengi kutwa kuchwa wanakimbizana na sunna, wakati yale matendo ya lazima (fardhi) hawajakamilisha hata kwa 60%
Mtu anagombana na watu kwenye Sunna huku ni mshirikina, muasharati, sio muadilifu, hawajali masikini na mayatima, hachungi ulimu wake nk nk nk
Sunna ni vile vitu vya ziada baada ya kufanya vile vya msingi (faradhi)
Tatizo ni ELIMU, ELIMU, ELIMU....
 
Kwahiyo wewe una mamlaka ya kumpangia huyo Mungu?

Mungu hawezi akajichanganya, aanzishe dini mpya miaka mia sita inayopingana na kila kitu alichokua ameweka, yaani dini ya porno na mabikira 72 na maupuzi mengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…