Je, kutosheka katika sex ni dhana na wajibu binafsi, tegemezi au shirikishi? Na mwenye vigezo na ufahamu ni nani?

Je, kutosheka katika sex ni dhana na wajibu binafsi, tegemezi au shirikishi? Na mwenye vigezo na ufahamu ni nani?

Mwanamwaiche

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2022
Posts
665
Reaction score
968
Salaam wanajukwaa

Naomba ufikirie, ujitazame, ujipime na usome hadi mwisho penye mapungufu jazia, penye kosa kosoa, na maoni au mtazamo wako ni muhimu.

Hili neno kuridhika katika sex ni jukumu la kila mshiriki? na ili mtu aridhike ni dhana tegemezi au shirikishi? Mwenye kipimo Cha mridhiko ni nani na hicho kipimo kinafahamikai kiasi gani? Na mtambuka Kwa ufahamu na mahitaji ya jinsia zote?

Mathalani kama mnufaika wa jambo dhana na vigezo ninakuwa navyo mimi, je mtoa huduma ama mshiriki mwenza yeye wajibu wake ni na anajuaje vigezo vyangu, paso kuuliza, kumwambia, ama kuweka bayana juu ya huduma na mridhisho wake?

Je ni dhana jumuishi, shirikishi, binafsi? maandalizi kihisia, imwili na kiakili ni jukumu la nani?

Je, kuna muafaka wowote katika muktadha wa jinsia na maazimio yoyote kiujumla kati ya walimwengu kuwa:

1. Kuridhika kwa mwanamke ni hivi, ikawa bayana.

2 Kuridhika Kwa mwanaume ni hivi, ikawa bayana pia.

3. Huu mtihani uitwao sex na mrejesho wa kuridhika, notes na walimu wenye upamoja katika ufahamu wako wapi?

Ipi nene, ipi ndefu, ipi fupi, ipi pana, ipi maji, ipi kavu, ipi joto, ipi, baridi, ipi telezi, ipi legezo, ipi ya kubana?

Matarajio katika sex huwa ni shirikishi kwa jinsia zote, katika yapi, kwanini na ili iweje? Kuridhika ni hitaji la kila mshiriki Kwa wakati huo au kila liwapo tendo na ni kwa jinsia zote?

Changamoto binafsi za washiriki mfano lishe duni, stress, ugonjwa, matamanio, style pendwa, maandalizi pendwa, na je, hii dhana maandalizi na mizuka yake ni kwa kila mechi na timu yoyote yenye ushiriki au inategemea na timu shiriki, referee ni nani na maainisho ya mchezo fair na furahishi kwa washiriki wote ni yapi, kadi ya njano na nyekundu itokeje, wakati gani na kwa kosa lipi. Je, hao wanakuwa na mafundisho aina hizo za makosa?

Kutamani, kupenda, kudumu na Kwa muda katika mapenzi ni kupi na kunapimwaje?

Nahitimisha kwa mtazamo chekeshi, fikirishi na chokozi. Kuridhika iwavyo iweje ni jukumu na maandalizi binafsi kwa asilimia kubwa, kazi ya mshirika ni kushirikishwa katika hayo matarajio yako sio wote wenye macho ya rohoni, macho ya vitumbua na macho ya matango.

Tozo sahihi na stahiki huwa na vigezo na huwa ni shirikishi na halalii. Tujipime dharau za mdomo tukumbuke kunguru na njiwa wapo.

Nawaslisha
 
Nadhani Kila Mtu ashinde mechi zake mwenyewe! Haya mambo yakutaka kumridhisha Mtu ni aina fulani ya ushetani!
 
Yaani kama uko na majukumu ya ada, Kodi ya nyumba, chakula, mavazi, Wazazi nyumbani, pressure ya Kazini, Majirani, Siasa, TOZO, traffic Police stress, wezi, vibaka na bado unataka kumridhisha Mtu "mentally" ambaye mnalala kitanda kimoja siku 365¼ huo ni uwendawazimu...
 
Ukiwa busy na maisha utajikuta unaridhika tu, kama huna kazi za kuweka busy LAZIMA kichwa Cha juu kiende Likizo then the other part itakua "active". Ridhiko kubwa kwenye family (sizungumzii Singles and gold diggers) ni uwezo wa Baba kumudu mahitaji ya family kimatibabu, kiafya, kiulinzi, chakula, malazi, Elimu, usafiri na Zaidi KIROHO! Mengine ni ushetani mtupu
 
Kuridhishana kimapenzi hucreate win- win situation, yaani kila mtu atakuwa amefaidika,ila kinyume na hivyo huleta loose- win situation ambapo mmoja pekee ndo atakuwa amefaidika na tendo.

Tofauti na suala la ngono yapo Mambo mengine mengi ambayo hulets mutual satisfaction kwenye nyumba.Mfano baba kupmpenda mkewe na kumhudumia ipasavyo,mke naye kumheshimu mmewe na kumhudumia ipasavyo.
 
Kuridhika ni kufika kileleni. Kama unayeshiriki naye ni mtu wako ni wajibu wako kuhakikisha kuwa wote mnamaliza mwendo usimuache mwenzako njiani. Kama ni wa kununua wewe piga kivyako vyako ya kwake atajiju si umempa chake?

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom