Je, kuwa na dini ni miongoni mwa vigezo vya kuwa kiongozi hapa nchini? Kwanini?

Sio lazima kuwa dini maana nchi yetu sio ya kidini na tushawahi kuwa na viongozi wasiokua na dini mfano kingunge. Ila viongozi wengi wanajifungamanisha tu dini wakijua population kubwa ni waumini wa dini na bado Afrika tunawachakulia atheists kama watu wabaya au mashetani fulani hivi
 
Sawa mkuu nime kuelewa.
 
Kuwa na dini sio miongoni mwa vigezo muhimu vya kuaminika kuwa mojawapo wa viongozi wakuu wa mihimili ya nchi yetu hasa Serikali Kuu na Bunge

Hii inatokana na sababu kuu ya kwamba katiba ya Tanzania inatambua kuwa mfumo wa utawala wa nchi yetu ni wa kisekula, yaani "secular state" ama usiofungamana na dini yoyote ile.

Viongozi wengi waliopo ndani ya mfumo huu wana imani zao binafsi za kidini, lakini hili si kigezo chenye nguvu kuwa wale wasiokuwa na dini hawawezi kufikiriwa endapo wataamua kugombea nafasi za uongozi wa juu wa nchi yetu. Ni takwa la kikatiba kuwa mtu yeyote mwenye sifa, na sifa ya kidini haitwaji kuwa ni sehemu ya sifa husika.
 
Mfano wako haukidhi kutengeneza swali unalouliza, jipange upya.
 
Kwa hapa Tanzania Ni lazima uwe mkatoliki au muislamu ndio ulambe shavu.

Wengine wote ni wasindikizaji.
 
Sawa
 
Ni makosa makubwa Sana KWA wanasiasa kuapa kwa vitabu vya dini inafaa waape kwa katiba.
Maana yote wanayoyaapa hawana hata moja wanalotekeleza zaidi ya kuongopea wananchi.
Pana mmoja aliwadanganya watu atawapeleka Ulaya
 
Ni makosa makubwa Sana KWA wanasiasa kuapa kwa vitabu vya dini inafaa waape kwa katiba.
Maana yote wanayoyaapa hawana hata moja wanalotekeleza zaidi ya kuongopea wananchi.
Pana mmoja aliwadanganya watu atawapeleka Ulaya
Ha ha ha ha ha, Birmingham.

Ila ulicho andika ndugu ni kweli kabisa.
 
Kwa nchi zenye dini ni sawa ila taifa letu halina dini, wananchi wana imani zao tofauti. Hata kama unaabudu wanyama unapewa uongozi ili mradi tu uilinde katiba ya nchi.
 
Si nasiki Kingunge hakuwa na dini au? Na mboma alikuwa kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…