Mwakyembe alipokua wizara ya sheria na Katiba wizara ilikua ipo ipo tu kama wizara ya wasanii fulani hici.
Sass hivi kapelekwa wizara ya Habari na Utamaduni Wizara imekua ya kisanii zaidi kuliko usanii.
Kwa uongo wako hata wa kundi lako wanaona aibu kukuunga mkono. Nikupe chache tu. Kwa kipindi Dk. Mwakyembe kama Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo;
1. Simba imefika robo fainali Klabu Bingwa Afrika
2. Taifa Stars imefuzu AFCON 2019 tangu ilipoganya hivyo 1980.
3. Taifa Stars imefuzu mara ya pili kucheza CHAN.
4. Tanzania imepeleka timu NNE mashindano ya Afrika ya Klabu Bingwa (Simba na Yanga) na Shirikisho (Azam na KMC).
5. Tanzania kwa mara ya kwanza ilikuwa mwenyeji wa Maahindano ya Vijana ya Under 20 Afrika.
6. Ngorongoro Heroes wametwaa ubingwa wa CECAFA huko Burundi.
7. Timu ya vijana ya Taifa ya Wanawake ya mpira wa miguu imechukua Ubingwa wa Kombe la COSAFA.
8. Timu ya Taifa ya Wanawake imechukua ubingwa wa CECAFA Senior Challenge na kisha nafasi ya pili mtawalia.
9. Diamond imechukua tuzo kedekede Afrika, Ulaya, Amerika na duniani kwa ujumla.
10. Mwakinho amempiga Mfilipino na kuingia kwenye anga za kiduni!
Na mengine mengi ambayo sijayataja hapa kwasababu nafasi ni ndogo. Je dogo, ulitaka afanye yapi zaidi ya haya?