Je, kwa maono yako unaionaje dunia mwaka 2100 (Maisha, Teknolojua, Mazingira, Imani, n.K)

Je, kwa maono yako unaionaje dunia mwaka 2100 (Maisha, Teknolojua, Mazingira, Imani, n.K)

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kwangu naona dunia kwa mwaka 2100 wengi humu tutakuwa tupo kwenye makazi yetu ya kudumu.

Naiona dunia hapa kwetu tutaanza utaratibu wa mazishi kwa kuchomwa moto kwasababu ya changamoto ya ardhi.

Naiona dunia miaka hio, mambo ya ushoga, usagaji, kubadili jinsia yatakuwa katika kiwango cha juu mno na yataruhusiwa na kuonekana vitu vya kawaida.

Naiona dunia ikitumia maroboti kwenye kazi na watu wengi kukosa ajira.

Naziona nchi za ulaya, wazawa (wazungu) wakiwa wachache sana huku maharamia wakiijaza nchi (Waarabu, Wahindi, Waafrika)

Naiona Tanzania baadhi ya makabila yakiwa yamefutika kabisa baada ya vizazi kuchanganywa sana.
 
Makabila na lugha nyingi zitakufa.

Kwenda nchi nyingine itakuwa rahisi tu kama kupanda Daladala.

Big deal itakuwa kwenda Mars na Mwezini.
 
Hata walio kuwepo miaka ya mwanzoni ya wa 1900 walidhani mwaka wa 2000 ndio utakaokua mwisho wa dunia

Hata sisi tulivyokua tupo shuleni tulikua miaka ya 1990 tuliambiwa kabisa 2000 Ni mwisho wa dunia hivyo tujiandae!

Badala yake miaka 20 imekwisha pita baadae bila ya yale tulioambiwa kutokea.

Na hata hoja yako hii ndugu mleta mada Ni ya kusadikika tuu, Kwanza miaka Mia Ni midogo mnoo Katika ulimwengu

Hata bwana Yesu aliwaambia wafuasi wake ya kua kizazi kile kisingepita bila ya kushuhudia mwisho wa dunia, badala yake miaka 2000 na kuzidi imekwisha piata bila ya kutokea hayo.
 
Kwa kasi ya sasa, allowing for corrections,Tanzania itakuwa na watu zaidi ya milioni 300.

Kama bado itakuwepo.
 
Kuna wapuuzi walidhani 2020 kutakua na flying cars.. Badala yake ndio tunakutana na vipochi hivi vinauzwa hapo Mlimani city.. can't wait 2100 tukiwa mbinguni tutashuhudia nn.

images (20).jpeg
 
TEKNOLOJIA.

Ubongo kuunganishwa na computer, microchips. Utafiti umekwisha anza.

Mawasiliano kufanyika kielektroniki kati ya ubongo wa mtu mmoja na mwingine bila ya uhitaji wa maongezi ya mdomo.

Mazingira ya uzalishaji mali na kibiashara kuboreshwa zaidi. Matumizi ya mifumo ya uzalishaji yenye kujiendesha yenyewe (automatic) zikiwemo robots n.k. yatashamiri zaidi kuliko hivi sasa. Uwepo wa mifumo maalumu ya utambuzi ikiwemo ya miamala ya kibiashara itakayowezeshwa kuwatambua watu na mahali popote watakapokuwepo.

Miundombinu ya usafiri kuboreshwa zaidi. Matumizi ya vyombo vya usafiri vyenye kujiendesha vyenyewe (self-driving). Petroli na dizeli kupitwa na wakati. Teksi zinazopaa (flying taxis) zitatumika kwa wingi. Majaribio yake yanaendelea hivi sasa.
 
By 2100 deposits zote za mafuta, gas na coal zitakua exhausted. Can u imagine a world without oil, gas and coal?

Bilionea wa miaka hiyo atakua ni mtu atakaegundua mbadala wa oil, gas and coal katika nyanja zote za matumizi.
 
Kutakuwa na matumizi ya umeme kama source of power
 
By 2100 deposits zote za mafuta, gas na coal zitakua exhausted. Can u imagine a world without oil, gas and coal?

Bilionea wa miaka hiyo atakua ni mtu atakaegundua mbadala wa oil, gas and coal katika nyanja zote za matumizi.

Nina uhakika mbadala utakuwa umepatikana.
 
Na hata hoja yako hii ndugu mleta mada Ni ya kusadikika tuu, Kwanza miaka Mia Ni midogo mnoo Katika ulimwengu
Ndugu mtoa mada amezungumzia Ni kwa namna gani unawaza ikifika 2100 dunia Itakuwa? Kuna mabadiliko ya Kitechnolojia etc. Mfano Unaweza sema kwamba Kuna kipindi Ndege itakuwa ni ishu ya Kawaida sana, yaana unaweza panda ndege chap ukafika Turin, then Kesho yake ukageuza zako Tz; Hii kitu nimeizungumzia kwa Maendeleo ya Technolojia na ugunduzi kwenye nyanja ya Usafirishaji.
SIo habari ya mwisho wa dunia.
 
Back
Top Bottom