Je, kwa maono yako unaionaje dunia mwaka 2100 (Maisha, Teknolojua, Mazingira, Imani, n.K)

Je, kwa maono yako unaionaje dunia mwaka 2100 (Maisha, Teknolojua, Mazingira, Imani, n.K)

Kwangu naona dunia kwa mwaka 2100 wengi humu tutakuwa tupo kwenye makazi yetu ya kudumu.

Naiona dunia hapa kwetu tutaanza utaratibu wa mazishi kwa kuchomwa moto kwasababu ya changamoto ya ardhi.

Naiona dunia miaka hio, mambo ya ushoga, usagaji, kubadili jinsia yatakuwa katika kiwango cha juu mno na yataruhusiwa na kuonekana vitu vya kawaida.

Naiona dunia ikitumia maroboti kwenye kazi na watu wengi kukosa ajira.

Naziona nchi za ulaya, wazawa (wazungu) wakiwa wachache sana huku maharamia wakiijaza nchi (Waarabu, Wahindi, Waafrika)

Naiona Tanzania baadhi ya makabila yakiwa yamefutika kabisa baada ya vizazi kuchanganywa sana.
Huku Polepole anahubiri mwisho wa dunia ni 2042😆😆
 
By 2100 deposits zote za mafuta, gas na coal zitakua exhausted. Can u imagine a world without oil, gas and coal?

Bilionea wa miaka hiyo atakua ni mtu atakaegundua mbadala wa oil, gas and coal katika nyanja zote za matumizi.
Kwasasa dunia Ina deposit ya kiasi gani mpaka utabiri 2100 iwe umekwisha? Kwenye pwani yetu msumbiji hapo tuna deposit ya cubic metres millions kadhaa na bado hazijaanza kutumika. Achilia mbali na hapo bado sehemu kibao tu
 
Ujinga wa waafrika wengi utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa na labda kuanza kuelekeza nguvu kwenye technology.

I think hibernation technology itakuwa tayari hivyo kuwezesha volunteers kufanya interstellar travels.
Maybe pia kugunduliwa uwepo wa wormholes hivyo kuwezesha binadamu au probes kufanya interstellar travels in short time.
 
Kabisa, ila unahitaji miundombinu (sehemu za kucharge Tanzania, Dunia nzima.) Ni kazi kubwa.
Ni kweli ila ukiachana na miondombinu.

Kwa huku waafrika ni ngumu kumiliki tesla sababu ya bei yake mfano tesla moja inacost dollar 40,000 ni kama million 86 za kitanzania.

Hivyo nadhani mpaka 2100 bado tutakuwa tunatumia oil kwa huku africa japo itakuwa cheap kidogo.
Labda kama elon musk aanze kutengeneza affordable tesla cars kwa africans au company nyingine iingie kati.
 
Kutakuwa na matumizi ya umeme kama source of power
- Unajua kwamba umeme pia unatokana na oil, gas, na coal? More than 60% ya umeme wa marekani unatokana na hizo products hapo juu whereas renewable energy sources ( wind, solar, geothermal, nk) kwa pamoja zinaproduce 17% tu ya jumla ya umeme. Nimetumia mfano wa US sababu ni developed country.

- Tatizo sio upatikanaji wa umeme shida ni upatikanaji wa umeme wa kutosha kukidhi mahitaji ya watu wote barabarani, maofisini, na majumbani. Na kumbuka miaka inavyokwenda kila kitu kinageuka kuwa electronic hivyo matumizi ya umeme lazima yaongezeke.

- Na sio umeme peke yake those products have a wide range of uses.
 
Wala siwaziii dunia ambayo sintokuwepo..

Umri Wangu wakuishi Duniani Ni mchache sana
 
Kwasasa dunia Ina deposit ya kiasi gani mpaka utabiri 2100 iwe umekwisha? Kwenye pwani yetu msumbiji hapo tuna deposit ya cubic metres millions kadhaa na bado hazijaanza kutumika. Achilia mbali na hapo bado sehemu kibao tu
Hakuna deposit isiyo na mwisho, deposits zote zina mwisho. Mimi sijatoa utabiri bali ni research ambayo imeshafanyika.

Hizo cubic metres millions unazoziona nyingi lakini miner anaplan kuziextract in the shortest period possible ili apige faida maradufu. Ukizingatia consumption ya fossils fuel inaongezeka kila kukicha.
 
Ndugu mtoa mada amezungumzia Ni kwa namna gani unawaza ikifika 2100 dunia Itakuwa? Kuna mabadiliko ya Kitechnolojia etc. Mfano Unaweza sema kwamba Kuna kipindi Ndege itakuwa ni ishu ya Kawaida sana, yaana unaweza panda ndege chap ukafika Turin, then Kesho yake ukageuza zako Tz; Hii kitu nimeizungumzia kwa Maendeleo ya Technolojia na ugunduzi kwenye nyanja ya Usafirishaji.
SIo habari ya mwisho wa dunia.
Naona ninyi ndio hamjamuelewa vema mchangiaji....
Mantiki yake kubwa( kama sijamwelewa tofauti) ni kwamba 2100 iko karibu sana kiasi kwamba tusitarajie mabadiliko makubwa kwenye hizo nyanja kama ambavyo wengi wanaamini mabadiliko kutokea sana..
Miaka 80 ijayo ni kidogo,, yaani ni kugusa tu kufikia tena unaweza kushangaa kwetu Tanzania bado CCM iko madarakani
 
Utakuja kushangaa baadhi ya nchi bado zinahangaika na ukosefu wa madawati.
Kwa kasi ya sasa, allowing for corrections,Tanzania itakuwa na watu zaidi ya milioni 300.

Kama bado itakuwepo.
 
uwezekano mkubwa sana miaka 100 kutokea sasa kifo hakitakuwepo tena.

tanzania itakuwa kama ilivyo china ya leo, kiuchumi hata kimaendeleo.
itakuwa ni miongomwa nchi chache zenye ushawishi zaidi duniani, baada ya nigeria na china yenyewe,maana itakuwa ni nchi ya 2 kwa idadi ya kubwa ya watu weusi duniani.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]zaidi ni kwamba, watakaokuja kusoma nilichoandika hapa wataniona nabii mbeba maono kama einstain.
 
Note my words; nitakuwa nipo kwenye watu wakukumbukwa kitaifa na kidunia.
Wewe ni Jiwe??
Maana jiwe ndo atakumbukwa kwa ukatili, ubaguzi wa misingi ya kabila, kanda, roho mbaya, chuki, utawala wa rushwa, wizi wa fedha za umma, ufisadi uliokubuhu....hebu mengine waongezee
 
Miaka 80 ijayo ni kidogo,, yaani ni kugusa tu kufikia tena unaweza kushangaa kwetu Tanzania bado CCM iko madarakani
Mtoa mada amezungumzia Dunia; Unaionaje Dunia in 2100?? Kwenye maelezo yake akaonyesha kwamba ni kwenye namna Mabadiliko yatakavyokuwa; Brother 80 Years unasema ni ndogo???, Hizi Technolojia Unanazoziona hazina 80 years ndugu yangu;
Serious Digital computer zimeanza kutengenezwa hapo early 40's ( Sio computer ya kwanza, hapa nazungumzia Modern/ Digital) Internet imekuwa 1960 tu which is almost 60 years back, Hizi Smart phone ni za 90' Infact zimeanza kutumiaka official 94 ambayo ni sawa na 27 years tu hapo nyuma;
Smart Tv ni product za early 2000's

Internet evolution imefungua milango ya Speed ya mambo kufanyika katika dunia hii kuliko unavyoweza kuwaza; Sasa ukisema Miaka 80 ni midogo napata shida sana, Most of technological Advance unazozifahamu zina less than or within 80 years hiyo unayoisema.
 
Watu wataacha kusali,makanisa na misikiti itafungwa,vibibi vizee na vibabu vitakuwa vikisema tuliwasikia babu zetu wakilitaja Jina la mwenyezi Mungu
 
Technology ya kuresist kuzeeka itakuwa imegunduliwa.
Kwani bado haijagunduliwa?

Hata hivyo mazingira tunayoishi ni chanzo kikubwa sana cha uzee (ageing). Kuna uwezekano mkubwa wa watu kuzeeka mapema zaidi hapo baadaye kuliko hivi sasa.
 
Back
Top Bottom