Je, kwa matendo haya ni imani za kishirikina?

Tuseme, ukipuuza tu suala hilo, kuna madhara yoyote? Halafu, kuna uhusiano gani kati ya Wadigo na hiki unachoripoti? Umefanya uchunguzi na kugundua Wadigo kadhaa hufanya hayo au ni huyo tu? Ni mazingira yepi yanasababisha wewe kuona hiyo ni tabia ya Wadigo?

Kauli yangu haimaanishi Wadigo hawawezi kuwa hivyo, bali ninahoji uhalali wa wewe kuona Wadigo watatoa majibu kama vile wao wapo hivyo.
 
Huu ni mji wa wadigo, tatizo liko wapi, unahofia nini? Mfano Ukienda Tarime vijijini, wote ni wakurya or at least by 99%, sasa ukisem wanafanya hivi kuna kosa gani? Nataka kujua wana imani gani na kufagia usiku?
Mfano mwingne, Wafanyabiashara kabla ya kuanza biashara say ya duka, anakwenda kwa mganga "kupiga deki" i.e kufukuza mabaya na kukaribsha bahati ya biashara, wanaamini hivyo, sasa kufagia usiku kenye giza kunahusishwa na nini?
 
Nadhani uko sahihi ingawa mengine umezidisha ka "chumvi"... πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ Ila Kilinge nimekisikia sana. Kuna Kilinge karibu na shamba langu. Ni kichaka kikubwa kiko kwenye kichuguu. Wenyeji wanaifanya ni sehemu ya kuagulia. wanaweka kuku , vyakula aina mbali mbali. Wanawake wanaogeshwa hapo wakiwa wamejifunga vikanga, ten wanaogoeshwa na wanauume kwa kumwagiwa maji na maneno ambayo siyafahamu.
Wakiweka kuku nawachukua nakula..... lkn nilikuja kugunda kuwa huyo "mganga huwa anarudi baadaye kuangalia kama kuku bado yupo, anakuta hayupo ...next time ananiomba awahifadhi kwangu kusudi mteja asione kuwa kuku ni wa kula.....
 
Jamii 'modern' Tz?
Yes, kuna watoto wamezaliwa kwenye familia tajiri hawajui hata lugha zao, wanajua Kiswahili, kiingereza na Kifaransa.... nineona na kuishi na familia za namna hiyo. Watoto wamesoma tangu chekechea International ones up to University abroad. Hao wako modernized by western culture na hivyo haya mambo y kimila hawayajui. These can be termed as "modern", "digital" children so to say! all in all kama unakubali kuwa "modern" is associated with Western style of life (kama tunakubaliana na definition hiyo anyway) If you have another definition of modern, I will be interested to note it!
 
Dini yangu ya nguvu za Giza haina upumbavu kama huo. Hizo ni tabia za MTU tu kama ambavyo wewe unaamka usiku kuangalia nani anafagia nje saa 10 ilhali ulitakiwa uwe kazini au umelala.
Come on kijana, yakipigwa makelele nje at those odd hours of night, mtu unayejitambua lazima uamke kujua kuna nini nje, what is going on! simple!
 
Retired sio mchawi namjua .. Na kwakweli si jambo la kawaida kwa mtu kufagia uwanja alfajiri pasipo na mwanga wa kutosha ama kukata matawi ya miti nyimbani kwako na kwenda kutafuta kivuli kwa jirani
Mshana Jr naishi na hawa watu, nasema ninachokiona. Leo nimeamka kufanya kazi kwenye computer, mtu anafagia! Giza totoro!
Kuna ngoma ya mashetani, zinapigwa kila leo naona...... wanachinja mbuzi wanakunywa damu naona..... najichanganya nao, ILA HAWASEMI NINI WANAFANYA MAANA WANAKUJUA KUWA WEWE SI MWENZAO NI WA "KUJA". HAWATAKI UJUE MILA ZAO. Naambiwa na vijana wa humu

Ukimuuliza Msambaa KOMA NDUGU ni nini hawakwambiii! Naomba utafute maana yake nini unijibu hapa rafiki
 
mwezi mchanga ni nini? kumchanganyikia ni nini? haya ni maneno ya ushirikina/false beliefs and the like, seems unayajua haya mambo vizuri
mwezi mchanga mtu anayeanza kurukwa na akili
 
kuna imani iliyopo miongoni mwetu sisi watu wa tanga ukijumlisha na dini ila inakuwa sio kama tumaamrishwa mfano watu wanadai baada ya swala ya alfajiri tusirudi kulala tena utafute kazi uanze kufanya mi nilipokuwa nikaa kuna wamaa naenda msikitini unakuta wanafagia na wala sio waislamu ila wadigo kwa kula mchana ndo wanapenda ila kuamka mapema
 
Ah kama hivyo sawa.

Mwezi mchanga ni yule mtu ambaye kichaa kinamjia kwa vipindi. Kuna muda kinashika kasi kuna muda kinatulia.

Ndiyo maana nimekuambia pengine huyo mama ni mwezi mchanga na kinamchanganyia randomly hata huo usiku unaomuona anafagia mwenzako anakua hayuko sawa.
 
Koma ndugu ina tafsiri zaidi ya moja ... Na mojawapo ni maana yake ni kuua ndugu(kuua undugu) hii hutokea pale ndugu wawili wa karibu wa jinsia tofauti wanapopendana kwa kujua ama kwa kutojua
Kama hao ndugu waliingia kwenye mahusiano kwa kujuana kama ni ndugu na wakafikia kutaka kuaona kabisa basi ndugu wengine hujulishwa na tambiko/kafara la kuua undugu hufanyika na ni lazima liambatane na damu hasa ya mbuzi

Kama waliingia kwenye mahusiano bila kujua wao ni ndugu ikija kujulikana basi hufanya pia kafara la kuwafungua toka muunganiko wa kindugu ama kuzika rasmi yale mahusiano
Kafara hizi hufanyika ili kukinga na kuua laana zote za malipizi, hasira uchungu nk
 
Nadhani uko sahihi ingawa mengine umezidisha ka "chumvi"... [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] Ila Kilinge nimekisikia[emoji23]

Tena hapo nimekupa juu juu tuu.. Hivi unajua ule ufagio hunenewa na kufanyiwa featuring kabla ya kufagia? Na wakati wa kufagia kuna formula yake na manuizi yake?[emoji23] Itafakari kazi ya fagio
 
Sasa, huoni kuna tatizo hapo kwenye kuwasilisha? Posti yako ilisema kuwa hapo ni mji kwa Wadigo? Huoni uliacha kigezo muhimu sana katika kisa chako?
 
Kwanini tusiwaze kuwa ni usafi ulipitiliza...?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…