Je, kwa takwimu hizi, Ki Aziz ni mchezaji mzuri au wa kawaida?

Je, kwa takwimu hizi, Ki Aziz ni mchezaji mzuri au wa kawaida?

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
13,628
Reaction score
20,992
WALE WANAOSEMA AZIZ KI NI WA KAWAIDA....SOMA HII PROFILE YKE JIBU BAKI NALO MWENYEWE


PROFILE STEPHANE AZIZ KI.

▪️Name - Stephane Ki Aziz
▪️Date of birth - March 6, 1996.
▪️Citizenship - Burkinafaso
▪️Position - Attacking midfielder
▪️Age - Twenty six years old
▪️Height - 1,75 Meter

Ki aziz alilelewa katika klabu ya Rayo Vallecano (Uth19) Spain kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka 2015.

Alijiunga na klabu ya CD Rogue de Lepe hukohuko Spain kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2016.

Baada ya msimu mmoja aliondoka na kwenda nchini Cyprus , akajiunga na klabu ya Omonia mwaka 2017.

Mwaka 2018 akiwa na miaka (22) alijiunga na klabu ya Nea Selamis ambapo alicheza mwaka mmoja akaamua kuondoka Ulaya na kurejea nchini Ivory Coast,

Aziz ki Akajiunga na klabu ya ligi kuu Ivorycoast Academie De FAD FC,

Mwaka 2020 ndipo alijiunga na klabu ya ASEC Mimosas . Hapa ndipo nyota yake ilipoanza kung'aa upya.

Kwani katika misimu miwili aliyoitumikia klabu hiyo amefanikiwa kufunga mabao (8) kwenye michuano ya (CAF) na Assists (5)

KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
👕 08 - Games
🎯 03 - Assists
⚽ 04 - Goals

KLAB BINGWA AFRIKA
👕 10 - Games
🎯 02 - Assists
⚽ 04 - Goals

AZIZ KI Msimu huu amefanikiwa kufunga mabao matatu kwenye kombe la shirikisho.

⚽ vs Simba Sc🇹🇿
⚽ Vs Simba Sc 🇹🇿
⚽ Vs RS Berkane 🇲🇦

Jumla amefunga magoli kumi na mbili kwenye mashindano yote msimu huu (2021-22) katika michezo (26)

👕 26 - Michezo yote msimu huu.
⚽ 11 - Ngazi ya klabu 🇨🇮
🎯 05 - Assists overall
⚽ 01 - Timu ya taifa 🇧🇫

UPEKEE ;
Anaweza kucheza wings zote mbili, pia kiungo mshambuliaji namba (10) na kiungo mchezeshaji namba (8).

➡Kushoto ndio mguu anaoutumia zaidi.
 
Wachambuzi wa kibongo wanasifia sana wachezaji ila uwanjani huyu Aziz K ni wa kawaida sana
 
Ni mchezaji wa kawaida Sana ila ni mchezaji mkubwa kwa timu ambazo ziko chini ya timu 20 kwa ubora wa vilabu barani Afrika.
Na ndio maana zile timu zilizoko ndani ya 20 bora zilituma offer zao za pesa ya viberiti zikatupiliwa mbali, kwa maana iyo ni mchezaji mkubwa kulinganisha na aina ya wachezaji wanaosajiliwa na vilabu vingine vinavyovizia wachezaji waliomaliza mikataba au kuachwa ili wapate mserereko wa kutoa pesa ndogo kwa wachezaji wabovu
 
Na ndio maana zile timu zilizoko ndani ya 20 bora zilituma offer zao za pesa ya viberiti zikatupiliwa mbali, kwa maana iyo ni mchezaji mkubwa kulinganisha na aina ya wachezaji wanaosajiliwa na vilabu vingine vinavyovizia wachezaji waliomaliza mikataba au kuachwa ili wapate mserereko wa kutoa pesa ndogo kwa wachezaji wabovu
Kama kambole et?
 
Na ndio maana zile timu zilizoko ndani ya 20 bora zilituma offer zao za pesa ya viberiti zikatupiliwa mbali, kwa maana iyo ni mchezaji mkubwa kulinganisha na aina ya wachezaji wanaosajiliwa na vilabu vingine vinavyovizia wachezaji waliomaliza mikataba au kuachwa ili wapate mserereko wa kutoa pesa ndogo kwa wachezaji wabovu
Na kama zilituma ofa yenye pesa ya viberiti basi ni mchezaji wa kawaida Sana. Maana kununua mchezaji mwenye thamani ya mil 150 halafu we ukamnunua kwa bln 1 nao ni aina fulani ya ushamba vilevile
 
Na kama zilituma ofa yenye pesa ya viberiti basi ni mchezaji wa kawaida Sana. Maana kununua mchezaji mwenye thamani ya mil 150 halafu we ukamnunua kwa bln 1 nao ni aina fulani ya ushamba vilevile
Ushamba huo walionao ndo umewafanya mtoke kapa msimu huu bila ata kikombe cha kunywea maji, Na huo ni ushamba unaolipa kama unasajili mchezaji mwenye thamani ndogo kwa bei kubwa na akakupa matokeo chanya kwa 100% basi ni haki yake kununuliwa kwa bei iyo, tofauti na unanunua mchezaji kwa bei ndogo na anakupa matokeo hasi sijui ni nani apo anaekuwa mshamba kati ya hao wawili
 
Msimu huu sio mzuri kwetu aisee, ubingwa tumekosa na kwenye usajili mapicha picha.
 
Naona kuna baadhi ya watu kama wamenuna/wamepaniki hivi kwenye huu uzi! Sijui shida iko wapi hasa.
 
Habari wanajf

Habari kubwa na inayotingisha vichwa vya wengi wa wadau wa soka ni usajili wa kiungo mshambuliaji Azizi Ki anayeichezea team ya Taifa ya Burkina faso ambaye inasemekana amesajiliwa na Yanga akitokea club ya ASEC Mimosas.kwa Takwimu yake ya 2021/2022 amecheza michezo 26 amefunga mabao 10 na assist 4 kutokana na takwimu zake hizi zimeibua mijadala mikubwa sana mtandaoni wapo ambao wanasema ni mchezaji mzuri na wengine wakisema mchezaji wa kawaida na wengine wakaenda mbali sana nakusema mbona takwimu za chama ni kubwa alizozitengeneza pale msimbazi kuliko za huyu mchezaji na wengine wakisema mbona saido ana number kubwa sana katengeneza msimu Huu ikiwa hata ligi haijaisha bado ni kubwa kuliko za Azizi Ki.


Nami nataka nichangie kuhusu Huu mjadala kwa namna ambavyo ninalijua soka by the way sijabahatika sana kumuona mechi alizocheza huyu mchezaji binafsi si muumini sana wa takwimu ni muumini sana wakumuona mchezaji uwanjani, mfano nikimuweka Iniesta na lampard wote hawa wanacheza nafasi moja ila ukiangalia takwimu zao Lampard kamzidi sana Iniesta kitakwimu kuanzia magoal mpaka assist Tena by far je nikikuliza Kati yao yupi Bora najua wengi watasema Iniesta je kwanini Iniesta na si Lampard? Jibu mnalo kwa maana Hii mchezaji anapimwa kwa vitu vingi sana ukiacha Takwimu zake kwa upande huu mzozo wa Azizi Ki kwenye nafasi yake ya kiungo mshambuliaji anatakiwa apimwe kwa chance created kuliko assist zake ngoja niwape mfano hiv kwa mfano chama angekuwa amecheza msimu huu nzima unadhani angekuwa ana number za assist kubwa kuliko msimu wake wa mwisho wa Simba kwa viwango hivi Vya Mugalu na John boko? Wanatumia hoja ya kuwa na assist mdogo kwa Azizi Ki wawe wanafikiri vitu kama hivi.

Je ligi yetu na ya burkina faso iko vip upande wa Quality?

NB: kwa upande wangu kea mechi mbili nilizobahatika kumuona huyu kijana nimemuona ni mchezaji mzuri anauwezo wa kucheza pembeni, katikati pia sometimes anakaba na anajua kuichezesha team tusibase kwa kuangalia Takwimu pekee
 
Back
Top Bottom